Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Tuesday, January 20, 2015

JAMII YA KIHADZABE SASA YAJENGEWA MABWENI MAWILI KWA WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA - LENGO LIKIWA NI KUIKWAMUA JAMII HIYO KIELIMU MKOANI SINGIDA




Na, Doris Meghji  Jumanne Januari 20,2015
wananchi wa Munguli wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Singida wakati wa kukabidhi mabweni mawili kwa ajili ya watoto Arobaini wa jamii ya Kihadzabe jamii ambayo bado inaishi kwa kutegemea matunda,nyama na asali wilayani Mkalama (picha na Doris Meghji)
Kijiji cha Munguli - wilaya ya Mkalama





Miss Singida akimvalisha mtoto mmoja wa kihadzabe nguo ya shule shati na sketi katika zoezi la kuwaelekeza watoto hao jinsi ya kuvaa uniform zao (picha na Doris Meghji)
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akimsikiliza Miss Singida Doris Mollel akitoa ahadi ya kuwajengea watoto hao maktaba ya kisasa jamii hio ya kihadzabe lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za mkuu wa mkoa wa Singida katika kuikomboa jamii hiyo ya Kihadzabe.(Picha na Doris Meghji)

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akimvisha shati la shule mtoto Kone Pascal mtoto huyo alipewa jina hilo pale mkuu wa mkoa wa Singida alipofanya ziara ya kwanza kutembelea kijiji hicho na kukuta wanawake hawapo wamebaki wanaume tu kwenye mkutano wake kumbe kulikuwa ni kuzaliwa kwa Mtoto Kone Pascal na ndipo walipo mpa jina la Kone mtoto huyo(picha na Doris Meghji)

Hii ni Nyumba ya Kuishi ya Matron na Patroni watakao kuwa wakiwaangalia wanafunzi wa darasa la kwanza wapatao arobaini wa jamii ya Kihadzabe Kata ya Munguli wilaya ya Mkalama mkoani Singida iliyozinduliwa rasmi na mkuu wa mkoa wa singida Januari 15,2015.
Hizi ndizo nguo za shule kwa watoto hao wakike na wakiume arobaini wa jamii ya kihadzabe walizoshonewa na halmashauri ya wilaya ya Mkalama ikiwa ni jitihada za serikali ya mkoa wa Singida katika kuikwamua jamii hiyo.(Picha na Doris Meghji)

watoto wakiume wa kihadzabe wakivaa viatu siku hiyo walipokabidhiwa mabweni na vifaa mbali mbali vya kuishi katika mazingira hayo ya shule katika mmoja ya bweni la wanafunzi hao wa darasa la kwanza la jamii hiyo ya kihadzabe (Picha na Doris Meghji)
Mwenyekiti wa jamii hiyo ya Kihadzabe Edward mashimba  akiishukuru serikali ya mkoa wa Singida kupitia vyombo vya habari kwa kuwajengea mabweni watoto wao na kuwapatia elimu ni mwenyekiti wa jamii hiyo(Picha na Doris Meghji)

Bweni la watoto wa kike katika shule ya Msingi Munguli kwa ajili ya watoto hao wakike wa jamii ya kihadzabe wilayani Mkalama litakalochukuwa watoto ishirini jamii ambayo bado inaishi maisha ya kijima mkoani Singida

Mmoja ya bweni la kuwalaza watoto hao wa darasa la kwanza wa jamii ya kihadzabe wilayani Mkalama Kijiji cha Munguli mkoa wa Singida

Hadi siku hiyo ya kukabidhiwa mabweni shuleni hapo ni watoto 23 tu ndio waliofika siku hiyo hivyo mkuu wa mkoa wa singida  Dkt. Parseko Kone amewaagiza watendaji kuanzia ngazi ya kitongoji  kijiji hadi  wilaya  kuhakikisha watoto walengwa ndio wananufaika na mpango huo wa kuiendeleza jamii ya kihadzabe na sio vinginevyo

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa mabweni  hayo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya mkalama Bravo Lyapembile,  amesema jumla ya shilingi milioni 59,077,080/= zimetuka kwa ajili ya kujenga mabweni hayo mawili nyumba ya watumishi,jiko vitanda na ununuzi wa magodoro ununuzi wa mahitaji ya wanafunzi hao ambazo ni nguo viatu mashuka bila kusahau ununuzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 500
Mwisho.

No comments:

Post a Comment