Na, Doris Meghji Ijumaa Januari 16,2015
Mkalama – Singida
Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone akipanda mti katika siku ya upandaji miti kimkoa katika shule ya Sekondari Nkito wilaya ya Mkalama (Picha na Doris Meghji) |
Mkuu wa
mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone ameziagaiza mamlaka za serikali za mitaa mkoani Singida
kutumia sheria ndogo walizojiwekea
katika hifadhi ya mazingira ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kupanda miti kumi
kwa kwaya za vijijini na miti mitano kwa kaya za mijini kila mwaka usimamiwe
kimamilifu ili kuikinga mkoa huo dhidi ya jangwa.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akihutubia siku ya upandaji miti kimkoa katika shule ya sekondari ya Nkinto wilaya ya Mkalama (Picha na Doris Meghji) |
Mkuu wa mkoa huyo ameziagiza mamlaka
hizo za serikali za mitaa jana katika siku ya upandaji miti kimkoa katika kijiji cha Nkinto halmashauri ya
wilaya ya Mkalama inayoadhimishwa kila Januari kumi na tano mkoani hapa
Mmoja wa wananachi wa kijiji cha Nkinto akipanda mti katika siku ya upandaji miti kimkoa wilayani Mkalama (Picha na Doris Meghji) |
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama na wananchi na wakazi wa kijiji Nkinto wakipanda miti katika shule ya sekondari Nkinto(Picha na Doris Meghji) |
Aidha amesema katika kukabiliana na hali
ya kuenea kwa jangwa ametaka hatua mbali mbali zichukuliwe na serikali kwa
kuanzisha kampeni mbali mbali za upandaji miti mfano ni kampeni ya Misitu ni Mali,Moto na
Mazingira,uhamasishaji wa kila kaya kupanda miti isiopungua kumi na taasisi
zenye matumizi makubwa ya miti zimeagizwa kuanzishwa mashamba yao ya miti,huku
kuunda programu ya kukuza na kueneza misitu Tanzania chini ya wizara ya maliasili na
utalli na kushirikisha wananchi katika kuhifadhi uoto wa asili kupitia mradi wa
PFM (Particpatory Forest Management)
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akimwelekeza mwanafunzi wa shule a Msingi Nkinto kupanda mti kwenye siku ya upandaji miti kimkoa wilayani Mkalama (Picha na Doris Meghji) |
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa Dkt. Kone ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa
Singida kuifadhi uoto wa asili kwa kuwa miti mingi wanayopanda inakufa hivyo amewaomba
watu binafsi na vijiji watenge maeneo ya
hifadhi za misitu ya uoto wa asili kwa kuwa huota haraka. Ametoa
wito wa hifadhi za misitu ya asili kutumika kwa shughuli za ufugaji nyuki,ili
kuongeza kipato cha wananchi kutokana na zao hilo la asali.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akitia msisitizo juu ya faida za misiti kwa wananchi wa kijiji cha Nkinto wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida (picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo mkoa wa singida una jumla ya
vijiji 230 vyenye misitu ya asili vya ukubwa wa hekta zipatazo laki tano ishirini miatatu ishrini na tano
nukta arobaini na tano (520,325.48)
Afisa Maliasili Mkoa wa Singida Bwana Charles Kidua akitoa taarifa fupi ya upandaji miti siku ya upandaji miti kimkoa wilaani Mkalama(picha na Doris Meghji) |
Awali afisa maliasili mkoa wa Singida
Charles Kidua akisoma taarifa fupi ya siku ya upandaji miti kimkoa amezitaja
mbinu mbali mbali ambazo idara ya maliasili mkoa wa singida imejipanga za
upandaji miti ni kwa kila wilaya kutenga maeneo kwa ajili ya ukarabati kwa
upandaji miti maeneo yaliyolengwa yasiyotumika kwa shughuli za kilimo kuanzia
eka moja na kuendelea,wananchi wataweza kushiriki katika upandaji na utunzaji wa miti
na kutoa fursa ya elimu ya upandaji miti kwa jamii nzima.
Aidha kwa suala uhamasishaji amesema suala la kuzihamasisha taasisi za kidini na
zisizo za kiserikali kupanda miti angalau isiopungua mitano kwenye maeneo ya
kuabudia na za kufanyia shughuli zao tayari viongozi wa taasisi hizo
zimejulishwa huku mbinu ya kuanza kutoa zawadi kwa taasisi za kiserikali na zisizo za
kiserikali na watu binafsi wanaopanda
miti kwa wingi.
Katikati ni mkuu wa wilaya ya Mkalama Edward Ole Lenga akifurahiya watumbuizaji katika siku hio ya upandaji miti kimkoa (picha na Doris Meghji) |
Amesema pamoja na na upandaji miti
unaenda sambamba na uhifadhi wa uoto wa asili uliopo amesma upandaji miti pekee
hautoweza kupambambana na mabadiliko ya hali ya tabia nchi bila kuhifadhi uoto
wa asili.hivyo mkoa umetomia njia shrikishi jamii katika kuhifadhi misitu ya
asili iliyopo ambao ni misitu ya Mgori,Minunghe na Sekenke Tulya pia ukiwepo
msitu wa watu binafsi mfano wa msitu wa Sombi katkika kijiji cha Msikii wenye
hekta 40.
Amesema licha ya juhudi hizo za
kuhifadhi misitu ya asili wapo watu wachache wanataka kukwamisha juhudi hizo
wakiwemo wahamiaji haramu katika msitu wa Minung’he na sehemu ya msitu wa Mgori.
Viongozi na baadhi ya wananchi wakichukuwa miti kwa ajili ya kupanda katika eneo la shule ya Sekondari ya Nkinto wilaya ya Mkalama (Picha na Doris Meghji) |
Jumla miti mia tano arobani (540)
imepandwa jana katika shule ya msingi Nkito wilayani Mkalama mkoa wa Singida na kauli mbiu ya siku ya upandaji miti kitaifa ni
MISITU NI UHAI;KATA MTI PANDA MITI” kauli mbiu ambayo mkuu wa mkoa wa Singida
haijambaliki kwa kusema kata mti panda miti kwa kutaka kauli hiyo iwe panda
miti kata tawi kwanini ukate mti.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment