Wananchi wakimsubiri
Mh.Lazaro Nyalandu katika viwanja vya Ndege mkoani Singida (Picha na Doris Meghji)
|
Monday, June 29, 2015
WAZIRI NYALANDU AWASILI SINGIDA - KUTAFUTA WAHDAMINI WA KUMDHAMINI KWA NAFASI YA URAIS - MKOANI SINGIDA
JANUARY MAKAMBA APATA WADHAMNINI 8300 WALIOMDHAMINI KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS KWA TIKETI YA CCM - MKOANI SINGIDA
Na, Doris Meghji Jumatatu Juni 29, 2015
Singida
Mh. January Makamba akiwasalimia
wanachama wa CCM mkoa wa Singida wakati akipita mkoani hapo kutafuta wadhamini
wa kudhamini kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM (Picha na Doris Meghji) |
Watanzania wanataka mabadiliko
wasipoyapata CCM watayapata nje ya CCM ni kauli ya Mwl Julias Kambarage Nyerere
mwasisi wa CCM inaraudiwa tena na January Yusuf Makamba mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM
mkoani Singida
Mh. Makamba (MB) mgombea wa nafasi ya
urais amesema hayo wakati akitafuta wadhamini wanachama CCM kumdhamini kwa nafasi hiyo ya urais kwa kuwataka wanaccm kumchagua
yeye kijana katika kinyang’anyiro hicho pale atakapo chaguliwa kupeperusha
bendera ya CCM kwa nafasi hiyo.
Mgombea nafasi ya urais Mh. January
Makamba akinyanyua fomu ya udhamini mbele ya wanachama wa CCM waliofika
kudhamini katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji) |
Aidha amesema amejipima na kuona nafasi
hiyo anaiweza vizuri. Katika kuelezea nia yake ya kugombea nafasi hiyo amesema
“nchi imekuwa na uongozi wa kizazi
cha kilichopita kwa miaka 50 kazi kubwa imefanyika ya maendeleo kwa miaka
50 iliyopita na imefanya vizuri lakini
sasa na miaka hamsini ijayo inahitaji viongozi wa kiazazi kipya,inahitaji
uongozi wa kisasa na sio uongozi wa kisiasa uongozi wenye mtazamo mpya, fikra
mpya na uongozi wa majawabu mapya ya changamoto zinazoikabili nchi yetu yeye
ndio mwenye majawabu ya changamoto hizo alisistiza Mgombea Makamba.
Katika kurudia kauli ya Mwl Julius Kambarage Nyerere alipohutubia
mkutano mkuu mwaka 1995 Chimwaga mkoani Dodoma kwamba watanzania
wanataka mabadilio wasipoyapota CCM watayatafuta nje ya CCM hadi sasa ni miaka
15 tangu Mwl atoe kauli hiyo na bado watanzania wanataka mabadiliko,
vijana wanataka mabaliko na kila siku wanayasema na wanayadai mabadiliko wasipoyapata ccm watayatatufa nje ya ccm hivyo ccm inayonafasi ya
kufanya madadiliko ni kwa kumteua
mgombea ambaye akisimama ataashiria mabadiliko na mgombea wa namna hiyo ni yeye
alisisiza Mh. Makamba
Baadhi ya wakinamama wa chama cha
mapinduzi waliojitokeza kudhamini
mgombea wa nafasi ya urais Mh. Makamba kwa tiketi ya CCM mkoani Singida ( Picha
na Doris Meghji) |
Katika zoezi hilo la kutafuta wadhamini
jumla ya wadhamini 8300 wanachama wa ccm waliojitokeza kudhamini mgombea huyo
ambapo wilaya ya singida mjini wadhamini 6500,Singida vijijini 600 huku wilaya
ya mkalama wagombe 1200 na kufanya idadi hiyo ya wadhamini nje ya wadhamamini
45 wanaohitajika kwa mujibu wa taratibu za chama hicho.
Wanachama wa CCM wakimlaki Mh. Makamba
mara alipowasili katika maeneo ya viwanja vya ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris
Meghji) |
Bi Ramona
Makamba mke wa Mgombea urais kwa tiketi ya CCM akiwasalimia wanachama wa CCM
waliofika kumdhamini mume wake ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris
Meghji) |
Bi Ramona
Makamba mke wa Mgombea urais kwa tiketi ya CCM akiwasalimia wanachama wa CCM
waliofika kumdhamini mume wake ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris
Meghji) |
Jorum Alute
mwenyeiti Mstaafu akimsemea neno Mh. Makamba mbele ya wanaccm mkoa wa Singida waliofika kudhamini mgombea
huyo kwa nafasi ya urais wa CCM ( Picha na Doris Meghji) |
Saturday, June 27, 2015
MH. MIZENGO PETER PINDA AMEWAASA WANACCM KUTOBAGUANA KWA MISINGI YA HUYU WA FULANI NA HUYU WA FULANI KATIKA LA KUFATUTA WADHAMINI - MKOANI SINGIDA
Na, Doris Meghji Jumaosi Juni 27,2015
Singida
Mh. Mizengo Peter Pinda amewataka
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuepuka kishawiwshi cha kubaguana kwa msingi
wa huyu ni fulani na huyu ni wa fulani kwa kuwa kishawishi hicho haina tija kwa wanachama hao.
Kauli hiyo ameitoa juzi majira ya saa
sita adhuhuri katika viwanja vya ccm mkoa wa Singida kwenye zoezi la kuwatafuta
wadhamini wa kumdhamini kwenye kinyang’anyiro cha uombea wa nafasi ya
urais wa chama hicho.
Aidha amewataka wanachama wa chama hicho
kutobaguana kwa misingi ya huyu ni wa
fualani na huyu wa fualani “mimi nita mwendea tu hata kama yeye ni wa fualni
kwangu mimi naamini wote ni wanaccm tu” alizitiza Mh. Pinda
Hivyo katika kuwatafuta wadhamini wa
kudhamini kugombea nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM jumla ya wadhamini 45
wamejitokeza kumdhamini katika nafasi hiyo mkoa wa Singida
Baadhi ya wanachama wa chama cha
mapinduzi waliojitokeza kudhamini na
kumsikiliza Mh. Mizengo Peter Pinda katika kinyanganiro cha urais (Picha na
Doris Meghji) |
Mh. Pinda amewashukru wanachama
waliojitokeza kudhamini akisema kama ccm itamuona anafaa na kutaka apeperushe
bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu
atashukuru na kazi yake itakuwa ni kuitekeleza ilani ya chama hicho
ambayo ndio muongozo mkuu.
Baadhi ya wanachama wa chama cha
mapinduzi waliojitokeza kudhamini na
kumsikiliza Mh. Mizengo Peter Pinda katika kinyanganiro cha urais (Picha na
Doris Meghji) |
Mh. Mizengo Peter Pinda ni mmoja kati ya
watia nia 39 ya wagombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM.
Saturday, June 20, 2015
NI WADHAMINI 1905 WAJITOKEZA KUMDHAMINI MH. MEMBE MTIA NIA KATIKA UGOMBEA NAFASI YA URAIS KWA TIKETI YA CCM- MKOA WA SINGIDA
Na, Doris Meghji Jumamosi
Juni 20,2015
Singida
Mh. Bernard Membe akihutubia wakazi na
wananchi wa manispaa ya singida baada ya kudhaminiwa na wanaccm 1905 katika
mchakato wa kutafuta wadhamini wa kumdhanini nafasi hio ya rais(Picha na Doris
Meghji)
Jumla ya wanachama 1905 wa CCM wamejitokeza kumdhamini mgombea wa
nafasi ya Urais Mh.Bernard Membe mkoani
Singida ambapo katika kutoa shukurani zake za dhati mgombea huyo amesema siku akipata kuwa rais wa jamuhri ya Muungano
wa Tanzania kupitia chama hicho atataka
akumbukwe kwa kuleta utawala bora ulio wakweli na unaondoa dhuluma, unaoleta
adilifu,unazozingatia miiko ya uongozi na mengine mengi ikiwa ni pamoja na kutoa
adhabu watoa rushwa na mafisadi nchini.
|
Mh. Bernard Membe akihutubia wakazi na
wananchi wa manispaa ya singida baada ya kudhaminiwa na wanaccm 1905 katika
mchakato wa kutafuta wadhamini wa kumdhanini nafasi hio ya urais(Picha na Doris
Meghji)
Mh. Bernard Membe ameweka hayo adharani juzi wakati akitafuta wadhani wa
kumdhani katika kugombea kinyang’anyiro hicho cha nafasi ya urais kwenye
viwanja vya ofisi ya CCM mkoa wa Singida
|
Mh. Bernard Membe akisalimiana na baadhi
ya viongozi wa CCM wilaya singida wakati akiwasili katika viwanja ya ofisi ya
CCM mkoa wa Singida (Picha Doris Meghji) |
Membe amesema katika suala ilo la utawala bora atahakiisha
anarekebisha vipengele vya sheria vinavyowalinda wala rushwa na mafisadi nchini
hasa katika kipengele cha anayetoa na kupokea rushwa wate wakawa wakosaji.
Mh. Membe akinong’ona jambo na mmoja ya
watu watu waliojitokeza kudhamnini mtia nia huyo(Picha na Doris Meghji)
Aidha katika kutafuta wadhamini hao mtia nia Membe amesema lengo
la kutia nia hiyo katika kinyang’anyiro hicho amejiona sifa za kugombea nafasi hiyo anazo na anafaa
kuwa rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM.
|
Magdalena Ndwete katibu wa CCM wilaya Singida
mjini akisoma idadi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kudhamini mtia nia Membe
mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji) |
Vijana wa boda baoda akiongoza msafara
wa mtia nia Membe wakati akiwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Singida (Picha
na Doris Meghji) |
Mh. Bernard Membe mtia nia wa nafasi ya
urais kwa tiketi ya CCM akisubiri kupanda jukwahani kwa ajili ya kutoa shukrani
kwa waliojitokeza kudhamini mkoa wa Singida (Picha Doris Meghji) |
Wananchi na wakazi wa manispaa ya
Singida wakimsubiri Mtia nia ya kugombea nafasi ya urais Mh. Bernard Membe
waziri wa Wizara ya mambo ya nchi na ushirikiano wa Kimataifa (Picha na Doris
Meghji) |
Mh. Bernard Membe akiongozana na
viongozi na wadhamini waliojitokeza kudhamini mtia nia huyo katika ofisi ya CCM
mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo kwa mujibu wa
Mangula, mgombea wa CCM atakaeteuliwa kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi
Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 atakuwa na sifa hizi :
1. Awe na uwezo mkubwa wa kuliongoza taifa kwa kuzingatia uzoefu
wake katika uongozi wa shughuli za serikali, umma na taasisi.
2. Awe mwadilifu, mwenye hekima
na busara.
3. Awe na angalau elimu ya chuo
kikuu au inayolingana na hiyo.
4. Awe ni mtu mwenye upeo
mkubwa wa kuweza kudumisha muungano, amani, umoja na mshikamano wa kitaifa
uliopo.
5. Awe mwepesi wa kuona mbali
na asiyeyumbishwa, mwenye uwezo wa kufanya maamuzi ya busara kuhusu masuala
nyeti ya kitaifa kwa wakati unaofaa.
6. Awe na upeo mkubwa na uwezo
usiotiliwa shaka kuhusu masuala ya kimataifa na anayeweza kuwa kiongozi imara
atakayetuunganisha na mataifa mengine.
7. Asiwe mtu mwenye hulka ya
kidikteta au fashisti, bali awe mtu anayeheshimu katiba, sheria, utawala bora
na kanuni zilizopo.
8. Awe ni mtu anayeweza kutetea
wanyonge na haki za binadamu.
9. Awe mzingatiaji makini na
asiye mtu anayejitafutia umaarufu binafsi.
10. Awe mtu wa mstari wa mbele
kuzitekeleza sera na ilani ya CCM na awe ni mpenda haki na jasiri wa kutetea
maslahi ya umma, kupambana na dhuluma na uonevu.
11. Mtu asiyetumia nafasi yake
ya uongozi kujilimbikizia mali.
12. Awe ni mtu anayekubalika na
wananchi
13. Awe ni mtu makini katika
kuzingatia masuala ya uwajibikaji.
Mwisho.
Tuesday, June 16, 2015
MATUKIO KATIKA PICHA - KATIKA ZOEZI LA KUMDHAMINI MH. EDWARD LOWASSA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM LEO
PICHA NA DORIS MEGHJI
Baadhi ya wadhamini wanachama wa CCM wakiendelea kusaini katika fomu ya udhamini kwa ajili ya kumdhamini Mgombea Edward Lowassa (Picha na Doris Meghji) |
Hivi ndivyo wananchi na wanachama wa CCM walivyojitokeza leo kudhamini Mgombea urais Mh. Edwaerd Lowassa leo katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji) |
Wana CCM wakimsubiri Mh. Edward Lowassa kwa ajili ya kumdhamini mgombea huyo mkoani Singida leo katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida( Picha na Doris Meghji) |
baadhi ya wanachama wanawake wa ccm waliofika katika zoezi la kumdhamini Mh. Mgombea Urasi Edward Lowassa (Picha na Doris Meghji) |
Baadhi ya wazee wakimsubiri Mgombea wa nafasi ya urais leo Mh. Edward Lowassa katika viwanja va CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji) |
Mh. Edward Ngoyai Lowassa akiwasalimia leo wananchi waliofika kumlaki katika zoezi la kutafuta wadhamni wa CCM kwenye ugombea urais kwa tiketi ya CCM.( Picha na Doris Meghji) |
Mh. Edward Lowassa akisalimia wananchi n na viongozi wa wanachama wa CCM mkoa wa Singida leo katika ofisi za CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji) |
Bi Sarah Nalingigwa mmoja wa wanachama wa CCM mkoa wa Singida akimsumbili mgombea urais kwa Tiketi CCM Mh. Edward Lowassa kwenye zoezi la udhamnini leo katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida (picha na Doris Meghji) |
WANANCHI WA MKOA WA SINGIDA WAJITOKEZA KWA WINGI LEO KUMDHAMINI _ MH. EDWARD LOWASSA KATIKA NAFASI YA UGOMBEA URAIS
Na, Doris Meghji Jumanne Juni 16,2015
Singida
Mgombea Urais wa CCM Mh. Edward Lowassa
akihutubia wananchi na wakazi wa mkoa wa Singida katika ofisi za chama hicho
leo katika zoezi la kutafuta wadhamini wa kudhamini kugombea nafasi hiyo ndani ya chama hicho (Picha
na Doris Meghji)
|
Zaidi ya wanachama 22,elfu wa CCM wamejitokeza leo kumdhamini
Mgombea wa nafasi ya urais wa
Chama hicho MH. Edward Lowassa mkoani Singida
Mh. Edward Lowassa akipanda jukwaani
tayari kwa kuhutubia umati wa wananchi na wanachama wa mkoa wa singida
waliojitokeza kumdhamini leo katika kinyang’aniro hicho.(Picha na Doris Meghji) |
Katika ziara hiyo mkoani hapa Mgombea
nafasi hiyo ya urais Mh. Edward Lowassa
amewashukru wananchi na viongozi wa CCM mkoa wa Singida kwa kujikitokeza kwa wingi na
kuonyesha kuwa na imani kubwa kwake kwa kumdhamini kwa idadi hiyo ya wanachama
wa chama hicho.
Baadhi ya wananchi walijitokeza leo
kumsikiliza na kudhamini Mh. Edward Lowassa leo katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya urais
ndani ya CCM (Picha na Doris Meghji) |
Mgombea huyo amezieleza sababu zake za
kugombea nafasi hiyo kwa lengo kubwa la kuwaongoza watanzania kutoka katika wimbi la
umaskini licha ya utajiri wa rasilimali zilizopo katika nchi hii.
Mh. Edward Lowassa akieleza sababu za
yeye kugombea nafasi hiyo ya urais ndani ya CCM kwa wakazi wa mkoa wa singida
leo katika viwanja vya CCM mkoa.(picha Doris Meghji)
|
Mh. Lowassa anasema “Nagombea nafasi hii
kwa kwababu nimechukizwa na kuchoshwa na umaskini katika nchi yetu, toka 1962
baba wa taifa alisema tuna maadui wakubwa watatu maradhi,ujinga na umaskini leo
umaskini umekithiri kana kwamba hatuko
kwenye nchi yenye rutuba na yenye rasilimali nyingi sana za
utajiri kiasi hiki na wananchi wake kuendelea kuwa maskini mi nakataa kabisa” alisisitiza Mgombea Lowassa.
Wananchi wakimsikiliza mh. Edward
Lowassa leo katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji) |
Aidha amesema Mwenyezi Mungu akibari na kupata ridhaa wa jambo hilo ataendesha nchi
mchaka mchaka atafanya hivyo
katika elimu kilimo, ajira kwa vijana na maeneo mengine kwa rasilimali nyingi zilizopo katika nchi hii.
Wananchi wakimsikiliza mh. Edward
Lowassa leo katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo amewataka wajiandikishe kwa
wingi katika daftari la kudumu la wapiga kura ili iwape fursa ya kumchagua
kiongozi huyo Oktoba 25 mwaka huu.
Mh. Edward Lowassa akihutubia wananchi
wa mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji) |
Mh. Edward Lowassa akiwa ni mgombea wa
15 kufika katika mkoa wa singida kutafuta wadhamini watakao mdhamini kwa nafasi
hiyo kwa chama cha mapinduzi ambapo wilaya Singida mjini wadhamini 5272,Iramba
4201,Singida vijijini 4018,Ikungi 3122,Manyoni wadhamini 3920 huku wilaya ya Mkalama wadhamini 2225 wamejitokeza kumdhamini Mgombea huyo.
Viongozi wakimpokea Mh. Edward Lowassa
katika zoezi hilo la kutafuta wadhamini (picha na Doris Meghji) |
Wajumbe wa NEC mkoa wa Singida na Simiyu
wakisalimia wananchi pamoja na mbunge viti Maalum mkoa wa Singida Diana Chilolo
leo katika zoezi la kumdhamini mgombea urais kwa tiketi ya CCM ( Picha na Doris
Meghji) |
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida
Vijijini Narumba Hanje akiwasalimia wananchi waliojitokeza kumsikiliza Mgombea
Edward Lowassa.(Picha na Doris Meghji) |
Magdalena Ndwete katibu wa CCM wilaya
Singida mjini akitoa taarifa ya idadi ya wadhamini waliojitokeza kudhamini
mgombea huyo (Picha na Doris Meghji) |
Mgana Msindai Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Singida akimkaribisha mh. Edward Lowassa kuongea na wananchi wa mkoa wa Singida
leo katika viwanja vya ofisi ya CCM mkoa.(Picha na Doris Meghji) |
Mwisho.
Subscribe to:
Posts (Atom)