Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Tuesday, June 16, 2015

WANANCHI WA MKOA WA SINGIDA WAJITOKEZA KWA WINGI LEO KUMDHAMINI _ MH. EDWARD LOWASSA KATIKA NAFASI YA UGOMBEA URAIS

Na, Doris Meghji  Jumanne Juni 16,2015
Singida
Mgombea Urais wa CCM Mh. Edward Lowassa akihutubia wananchi na wakazi wa mkoa wa Singida katika ofisi za chama hicho leo katika zoezi la kutafuta wadhamini wa kudhamini kugombea nafasi hiyo ndani ya chama hicho (Picha na Doris Meghji)

Zaidi ya wanachama 22,elfu  wa CCM wamejitokeza  leo kumdhamini  Mgombea  wa nafasi ya urais wa Chama hicho MH. Edward  Lowassa  mkoani Singida
Mh. Edward Lowassa akipanda jukwaani tayari kwa kuhutubia umati wa wananchi na wanachama wa mkoa wa singida waliojitokeza kumdhamini leo katika kinyang’aniro hicho.(Picha na Doris Meghji)

Katika ziara hiyo mkoani hapa Mgombea nafasi hiyo ya urais  Mh. Edward Lowassa amewashukru wananchi na viongozi wa CCM  mkoa wa Singida kwa kujikitokeza kwa wingi na kuonyesha kuwa na imani kubwa kwake kwa kumdhamini kwa idadi hiyo ya wanachama wa chama hicho.
Baadhi ya wananchi walijitokeza leo kumsikiliza na kudhamini Mh. Edward Lowassa leo katika kinyang’anyiro cha  kugombea nafasi ya urais ndani ya CCM (Picha na Doris Meghji)

Mgombea huyo amezieleza sababu zake za kugombea nafasi hiyo kwa lengo  kubwa la  kuwaongoza watanzania kutoka katika wimbi la umaskini licha ya utajiri wa rasilimali zilizopo katika nchi hii.
Mh. Edward Lowassa akieleza sababu za yeye kugombea nafasi hiyo ya urais ndani ya CCM kwa wakazi wa mkoa wa singida leo katika viwanja vya CCM mkoa.(picha Doris Meghji)

Mh. Lowassa anasema “Nagombea nafasi hii kwa kwababu nimechukizwa na kuchoshwa na umaskini katika nchi yetu, toka 1962 baba wa taifa alisema tuna maadui  wakubwa watatu maradhi,ujinga na umaskini leo umaskini umekithiri  kana kwamba hatuko kwenye nchi yenye rutuba na yenye rasilimali nyingi  sana  za utajiri kiasi hiki na wananchi wake kuendelea kuwa  maskini  mi nakataa kabisa” alisisitiza Mgombea  Lowassa.

Wananchi wakimsikiliza mh. Edward Lowassa leo katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)

Aidha amesema Mwenyezi  Mungu akibari  na kupata ridhaa wa jambo hilo ataendesha nchi mchaka mchaka atafanya hivyo katika elimu kilimo, ajira kwa vijana na maeneo mengine kwa rasilimali nyingi  zilizopo katika nchi hii.
Wananchi wakimsikiliza mh. Edward Lowassa leo katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)
Hata hivyo amewataka wajiandikishe kwa wingi katika daftari la kudumu la wapiga kura ili iwape fursa ya kumchagua kiongozi huyo Oktoba 25 mwaka huu.


Mh. Edward Lowassa akihutubia wananchi wa mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)
Mh. Edward Lowassa akiwa ni mgombea wa 15 kufika katika mkoa wa singida kutafuta wadhamini watakao mdhamini kwa nafasi hiyo kwa chama cha mapinduzi ambapo wilaya Singida mjini wadhamini 5272,Iramba 4201,Singida vijijini 4018,Ikungi 3122,Manyoni wadhamini 3920 huku wilaya ya Mkalama wadhamini 2225 wamejitokeza kumdhamini Mgombea huyo.

Viongozi wakimpokea Mh. Edward Lowassa katika zoezi hilo la kutafuta wadhamini (picha na Doris Meghji)
Wajumbe wa NEC mkoa wa Singida na Simiyu wakisalimia wananchi pamoja na mbunge viti Maalum mkoa wa Singida Diana Chilolo leo katika zoezi la kumdhamini mgombea urais kwa tiketi ya CCM ( Picha na Doris Meghji)
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida Vijijini Narumba Hanje akiwasalimia wananchi waliojitokeza kumsikiliza Mgombea Edward Lowassa.(Picha na Doris Meghji)
Magdalena Ndwete katibu wa CCM wilaya Singida mjini akitoa taarifa ya idadi ya wadhamini waliojitokeza kudhamini mgombea huyo (Picha na Doris Meghji)
Mgana Msindai Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida akimkaribisha mh. Edward Lowassa kuongea na wananchi wa mkoa wa Singida leo katika viwanja vya ofisi ya CCM mkoa.(Picha na Doris Meghji)
Mwisho.






No comments:

Post a Comment