Na, Doris Meghji Jumaosi Juni 27,2015
Singida
Mh. Mizengo Peter Pinda amewataka
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuepuka kishawiwshi cha kubaguana kwa msingi
wa huyu ni fulani na huyu ni wa fulani kwa kuwa kishawishi hicho haina tija kwa wanachama hao.
Kauli hiyo ameitoa juzi majira ya saa
sita adhuhuri katika viwanja vya ccm mkoa wa Singida kwenye zoezi la kuwatafuta
wadhamini wa kumdhamini kwenye kinyang’anyiro cha uombea wa nafasi ya
urais wa chama hicho.
Aidha amewataka wanachama wa chama hicho
kutobaguana kwa misingi ya huyu ni wa
fualani na huyu wa fualani “mimi nita mwendea tu hata kama yeye ni wa fualni
kwangu mimi naamini wote ni wanaccm tu” alizitiza Mh. Pinda
Hivyo katika kuwatafuta wadhamini wa
kudhamini kugombea nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM jumla ya wadhamini 45
wamejitokeza kumdhamini katika nafasi hiyo mkoa wa Singida
Baadhi ya wanachama wa chama cha
mapinduzi waliojitokeza kudhamini na
kumsikiliza Mh. Mizengo Peter Pinda katika kinyanganiro cha urais (Picha na
Doris Meghji) |
Mh. Pinda amewashukru wanachama
waliojitokeza kudhamini akisema kama ccm itamuona anafaa na kutaka apeperushe
bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu
atashukuru na kazi yake itakuwa ni kuitekeleza ilani ya chama hicho
ambayo ndio muongozo mkuu.
Baadhi ya wanachama wa chama cha
mapinduzi waliojitokeza kudhamini na
kumsikiliza Mh. Mizengo Peter Pinda katika kinyanganiro cha urais (Picha na
Doris Meghji) |
Mh. Mizengo Peter Pinda ni mmoja kati ya
watia nia 39 ya wagombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM.
No comments:
Post a Comment