Na, Doris Meghji Jumatatu Juni 29, 2015
Singida
Mh. January Makamba akiwasalimia
wanachama wa CCM mkoa wa Singida wakati akipita mkoani hapo kutafuta wadhamini
wa kudhamini kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM (Picha na Doris Meghji) |
Watanzania wanataka mabadiliko
wasipoyapata CCM watayapata nje ya CCM ni kauli ya Mwl Julias Kambarage Nyerere
mwasisi wa CCM inaraudiwa tena na January Yusuf Makamba mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM
mkoani Singida
Mh. Makamba (MB) mgombea wa nafasi ya
urais amesema hayo wakati akitafuta wadhamini wanachama CCM kumdhamini kwa nafasi hiyo ya urais kwa kuwataka wanaccm kumchagua
yeye kijana katika kinyang’anyiro hicho pale atakapo chaguliwa kupeperusha
bendera ya CCM kwa nafasi hiyo.
Mgombea nafasi ya urais Mh. January
Makamba akinyanyua fomu ya udhamini mbele ya wanachama wa CCM waliofika
kudhamini katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji) |
Aidha amesema amejipima na kuona nafasi
hiyo anaiweza vizuri. Katika kuelezea nia yake ya kugombea nafasi hiyo amesema
“nchi imekuwa na uongozi wa kizazi
cha kilichopita kwa miaka 50 kazi kubwa imefanyika ya maendeleo kwa miaka
50 iliyopita na imefanya vizuri lakini
sasa na miaka hamsini ijayo inahitaji viongozi wa kiazazi kipya,inahitaji
uongozi wa kisasa na sio uongozi wa kisiasa uongozi wenye mtazamo mpya, fikra
mpya na uongozi wa majawabu mapya ya changamoto zinazoikabili nchi yetu yeye
ndio mwenye majawabu ya changamoto hizo alisistiza Mgombea Makamba.
Katika kurudia kauli ya Mwl Julius Kambarage Nyerere alipohutubia
mkutano mkuu mwaka 1995 Chimwaga mkoani Dodoma kwamba watanzania
wanataka mabadilio wasipoyapota CCM watayatafuta nje ya CCM hadi sasa ni miaka
15 tangu Mwl atoe kauli hiyo na bado watanzania wanataka mabadiliko,
vijana wanataka mabaliko na kila siku wanayasema na wanayadai mabadiliko wasipoyapata ccm watayatatufa nje ya ccm hivyo ccm inayonafasi ya
kufanya madadiliko ni kwa kumteua
mgombea ambaye akisimama ataashiria mabadiliko na mgombea wa namna hiyo ni yeye
alisisiza Mh. Makamba
Baadhi ya wakinamama wa chama cha
mapinduzi waliojitokeza kudhamini
mgombea wa nafasi ya urais Mh. Makamba kwa tiketi ya CCM mkoani Singida ( Picha
na Doris Meghji) |
Katika zoezi hilo la kutafuta wadhamini
jumla ya wadhamini 8300 wanachama wa ccm waliojitokeza kudhamini mgombea huyo
ambapo wilaya ya singida mjini wadhamini 6500,Singida vijijini 600 huku wilaya
ya mkalama wagombe 1200 na kufanya idadi hiyo ya wadhamini nje ya wadhamamini
45 wanaohitajika kwa mujibu wa taratibu za chama hicho.
Wanachama wa CCM wakimlaki Mh. Makamba
mara alipowasili katika maeneo ya viwanja vya ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris
Meghji) |
Bi Ramona
Makamba mke wa Mgombea urais kwa tiketi ya CCM akiwasalimia wanachama wa CCM
waliofika kumdhamini mume wake ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris
Meghji) |
Bi Ramona
Makamba mke wa Mgombea urais kwa tiketi ya CCM akiwasalimia wanachama wa CCM
waliofika kumdhamini mume wake ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris
Meghji) |
Jorum Alute
mwenyeiti Mstaafu akimsemea neno Mh. Makamba mbele ya wanaccm mkoa wa Singida waliofika kudhamini mgombea
huyo kwa nafasi ya urais wa CCM ( Picha na Doris Meghji) |
No comments:
Post a Comment