Na, Doris Meghji Jumamosi
Juni 20,2015
Singida
Mh. Bernard Membe akisalimiana na baadhi
ya viongozi wa CCM wilaya singida wakati akiwasili katika viwanja ya ofisi ya
CCM mkoa wa Singida (Picha Doris Meghji) |
Membe amesema katika suala ilo la utawala bora atahakiisha
anarekebisha vipengele vya sheria vinavyowalinda wala rushwa na mafisadi nchini
hasa katika kipengele cha anayetoa na kupokea rushwa wate wakawa wakosaji.
Magdalena Ndwete katibu wa CCM wilaya Singida
mjini akisoma idadi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kudhamini mtia nia Membe
mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji) |
Vijana wa boda baoda akiongoza msafara
wa mtia nia Membe wakati akiwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Singida (Picha
na Doris Meghji) |
Mh. Bernard Membe mtia nia wa nafasi ya
urais kwa tiketi ya CCM akisubiri kupanda jukwahani kwa ajili ya kutoa shukrani
kwa waliojitokeza kudhamini mkoa wa Singida (Picha Doris Meghji) |
Wananchi na wakazi wa manispaa ya
Singida wakimsubiri Mtia nia ya kugombea nafasi ya urais Mh. Bernard Membe
waziri wa Wizara ya mambo ya nchi na ushirikiano wa Kimataifa (Picha na Doris
Meghji) |
Mh. Bernard Membe akiongozana na
viongozi na wadhamini waliojitokeza kudhamini mtia nia huyo katika ofisi ya CCM
mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo kwa mujibu wa
Mangula, mgombea wa CCM atakaeteuliwa kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi
Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 atakuwa na sifa hizi :
1. Awe na uwezo mkubwa wa kuliongoza taifa kwa kuzingatia uzoefu
wake katika uongozi wa shughuli za serikali, umma na taasisi.
2. Awe mwadilifu, mwenye hekima
na busara.
3. Awe na angalau elimu ya chuo
kikuu au inayolingana na hiyo.
4. Awe ni mtu mwenye upeo
mkubwa wa kuweza kudumisha muungano, amani, umoja na mshikamano wa kitaifa
uliopo.
5. Awe mwepesi wa kuona mbali
na asiyeyumbishwa, mwenye uwezo wa kufanya maamuzi ya busara kuhusu masuala
nyeti ya kitaifa kwa wakati unaofaa.
6. Awe na upeo mkubwa na uwezo
usiotiliwa shaka kuhusu masuala ya kimataifa na anayeweza kuwa kiongozi imara
atakayetuunganisha na mataifa mengine.
7. Asiwe mtu mwenye hulka ya
kidikteta au fashisti, bali awe mtu anayeheshimu katiba, sheria, utawala bora
na kanuni zilizopo.
8. Awe ni mtu anayeweza kutetea
wanyonge na haki za binadamu.
9. Awe mzingatiaji makini na
asiye mtu anayejitafutia umaarufu binafsi.
10. Awe mtu wa mstari wa mbele
kuzitekeleza sera na ilani ya CCM na awe ni mpenda haki na jasiri wa kutetea
maslahi ya umma, kupambana na dhuluma na uonevu.
11. Mtu asiyetumia nafasi yake
ya uongozi kujilimbikizia mali.
12. Awe ni mtu anayekubalika na
wananchi
13. Awe ni mtu makini katika
kuzingatia masuala ya uwajibikaji.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment