Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Monday, June 15, 2015

WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA -

Na, Doris Meghji  Jumapili Juni 14,2015
Singida- Manispaa

Joseph Mchina Mkurugenzi wa manispaa ya Singida akitembelea  leo kituo cha kuandikisha wapiga kura mtaa wa Utemini (Picha na Doris Meghji)

Zoezi la uandiishaji wa  wananchi katika daftari la kudumu la kupiga kura awamu ya mwisho ndani ya manispaa ya Singida imeanza leo ikizihusisha jumla ya kata nne za manispaa hiyo
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura leo kituo cha mtaa wa utemini shule ya msingi utemini (Picha na Doris Meghji)


Katika zoezi hilo leo  yametolewa maelekezo  kwa waandikishaji wa vituo vya  hivyo kuhakikisha wanawaandikisha wananchi wa mtaa husika na si vinginevyo ikiwa ni pamoja na vijana ambao wenye  umri mdogo kuhitaji vithibitisho vya vyeti vyao vya kuzaliwa au kupata barua toka kwa mwalimu mkuu alipomalizia darasa la saba lengo likiwa kudhibiti mamluki katika zoezi hilo.
Mohamed Kipamila mmoja wa waandikishaji katika kituo cha mtaa wa saba saba akimhoji kijana wakati wa zoezi hilo leo katika shule ya msingi saba saba.(Picha na Doris Meghji)

Akitoa maelekezo hayo msimamizi mkuu wa zoezi la uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu la kupiga kura na  mkurugenzi wa manispaa ya Singida Joseph Mchina anasema  “ninamelekezo aina mbili wale wananotakiwa kujiandikisha katika kituo hii ni wale wanaishi mtaa wa utemini na sio nje ya mtaa wa  utemini. kila mtaa nimepeleka mashine hivyo hakuna haja mtu wa saba saba kuja kujiandikishia hapa utemini,la pili wale vijana wenye umri mdogo nihahtaji uthibitisho wa umri wao.
Wananchi na wakazi wa mtaa wa Stesheni walivyojitokeza leo katika kituo cha SIDO kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura (Picha na Doris Meghji)

Ninahitaji cheti cha kuzaliwa,au barua toka kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi alipomalizia darasa la saba au barua toka kwa mwenyekiti wake wa mtaa ndio nimruhusu kujiandikisha maana kuna vijana nawaona ni hapa ni  wadogo hawana umri huo wa miaka 18.” Asisitiza Mkurugenzi Mchina.
Zoezi la uandikishaji likiendelea katika Kituo cha Saba Saba (Picha na Doris Meghji)

Katika zoezi hilo la awamu ya mwisho ya kujiandikisha ndani ya manispaa ya Singida inahusisha kata ya Utemini, Mandewa,Mughanga na Mitunduruni  hivyo mkurugenzi wa manispaa hiyo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari hilo la kudumu
Hivi ndivyo kazi ikifanyika leo katika zoezi la uandiishaji mtaa wa Saba saba (Piha na Doris Meghji)

Hata hivyo zoezi hilo linatarajiwa kumalizika tarehe 20 mwezi huu kwa manispaa ya Singida na mkoa kwa ujumla.
Kituo cha SIDO cha uandikisha wakazi wa mtaa wa stesheni walivyojitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura leo majira ya saa sita adhuhuri.(Picha na Doris Meghji)

Mtendaji wa mtaa wa sabasaba Anneth Mayengela akiita majina ya watu wanaotakiwa kuandiishwa kwa muda huo(Picha na Doris Meghji)

Wakazi wa mtaa wa saba saba kata ya utemini waliofika kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura (Picha na Doris Meghji)
Vijana wakisubiri kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura (picha na Doris Meghji)

MWISHO.


No comments:

Post a Comment