Na, Doris Meghji Jumatatu Juni 10,2015
Singida
Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) imesema
uchauguzi mkuu wa kuchagua rais, wabunge na madiwani utafanyika kama
ulivyopangwa Oktoba 25 mwaka 2015.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa
tume hiyo taifa (NEC) Jaji Damian Lubuva
mkoani Singida katika ziara yake ya kutembelea na kuaona jinsi zoezi la kuandikisha wananchi katika daftari
la kudumu la kupiga kura jimbo la Singida mjini.
“uchaguzi utafanyika siki hiyo ya
Jumapili Oktoba 25 mwaka huu kama ulivyopangwa hii ni kutokana na wenzetu wa
Zanzibar walikwisha tangaza na kukamilisha maandalizi kwa wao kufanya uchaguzi
siku hiyo ya Jumapili Oktoba 25 .Hatuwezi nchi moja kufanya uchaguzi siku mbili
tofauti alisistiza Jaji Lubuva”
Hii ni katika kutolea maelezo kutoka kwa
baadhi ya wabunge kuhoji juu ya uchaguzi kufanyika siku hiyo ya Jumapili na sio
siku nyingine katika juma ispokuwa Jumapili
Hivyo amesema Tume ya uchaguzi imeliona
hilo na kuahidi kulifanyia kazi katika chaguzi zingine zijazo kwa kupanga siku
za uchauguzi kufanyika siku nyingine na sio siku za Ijumaa, Jumamosi na
Jumapili kwa kuwa ni siku ambazo wananchi wa Tanzania wanakwenda katika nyumba zao za ibada.
Hapo aliendelea kuwahakikishia
watanzania kuwa uchaguzi wa mwaka huu utafanyika siku hiyo ya jumapili
mwenyekiti huyo wa NEC.
Aidha kwa upande mwingine Mwenyekiti huyo
wa NEC ameliomba jeshi la polisi nchini kuimarisha ulinzi na usalama kwa
maafisa wa TUME katika vituo ikiwa ni baada ya tukio lililo wapata maafisa wa TUME
hiyo wilayani Mumba mkoani Mbeya kwa kuvamiwa na watu wanaodhanini ni
majabamzai na kwajeruhi maafisa hao.
Naye msimamizi wa uchaguzi jimbo la
singida mjini mkurugenzi wa manispaa ya Singida Joesph Mchina amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la
kudumu la wapiga kura linaendela vizuri kwa kuwa awamu ya kwanza wamefanikiwa
kuandikisha wananchi kwa wastani wa asilimia 86 katika daftari hilo liliohusisha
kata nne za Mtipa Uhamaka Mwankoko na Mtamaa
hivyo anatoa wito kwa wananchi wa
maeneo ya awamu ya pili ambazo ni kata ya Minga,Mungu Maji,Unyambwa na … kujitokeza kwa wingi kwenda
kujiandikisha ikiwa ni moja ya haki yao kidemokrasia kwa kuwapa tiketi ya
kuchagua viongozi watakao waongoza katika uchaguzi mkuu ujao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment