Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Friday, December 13, 2013

WANAWAKE NA VIJANA WAPATIWA ELIMU YA UJASILIAMALI- MANISPAA YA SINGIDA

Na, Doris Meghji  Ijumaa  Disemba 13 ,2013

Singida


Wanawake wametakiwa kutumia elimu ya ujasilimali ili kujikwamua kiuchumi kwa kuwa wanawake ndio walezi wakuu wa familia nchini

Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Singida Bi Hanna Churi amewaasa wanawake hao katika mafunzo ya ujasilimali yaliondaliwa kwa wanawake na wanachama wa jumuhiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT) wilaya ya singida mjini kwa uwezeshaji toka shirika la kazi duniani (ILO) kupitia mpango wa kazi nje nje yanayofanika katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya wananchi manispaa ya Singida 

Bi Hanna Churi na mwenyekiti wa muda katika mafuzo ya ujasiliamali yaliofanyika chuo cha maendeleo ya wananchi manispaa ya singida (picha na Doris Meghji)


Aidha Bi Churi amewataka wanawake hao kutumia fursa ya  mafunzo ya ujasiliamali yakayowawezesha kutumia mbinu mbali mbali katika kubuni miradi na kutafuta masoko ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano ndani ya jamii 
 
MH. DIWANI WA KATA YA UTEMINI BARTAZAR KIMARIO, KATIKATI MGENI RASMI BI HANNA CHURI AFISA MAENDELEO YA JAMII MANISPAA YA SINGIDA KWENYE MAFUNZO YA UJASILIAMALI - WANACHAMA WA UWT - SINGIDA MJINI ( picha na Doris Meghji)




BAADHI YA WASHIRIKI WA MAFUZNO YA UJASILIAMALI - UKUMBI WA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI (FDC) SINGIDA ( picha na Doris Meghji)

Kwa mujibi wa Afisa Maendeleo wa Jamii huyo anasema “ kwa kupitia mafunzo haya ya siku tatu hii itawasidia kujenga na kuimarisha mahusiano kati yenu na kuwa na sauti mmoja ndani ya jamii kwa kukutwanishwa pamoja katika mafunzo haya ya  ujasiliamali alisisitiza Bi Churi
AFISA MTENDAJI KATA YA UTEMINI BI EVA MBELWA NA KIJANA ANTONIA KATIKA MAFUNZO YA UJASILIAMALI - YALIOANDALIWA NA UWT SINGIDA MJINI (picha na Doris Meghji)

Awali akisoma taarifa ya uandaaji wa mafuzo hayo ya ujasiliamali  Katibu wa UWT wilaya ya mjini Bi Margaret K. Malecela ameeleza lengo la kuandaa mafunzo kwa wanawake na wanachama wa jumuiya hiyo ni kuwaendeleza wanawake katika kujikwamua kiuchumi na kujenga taifa lisilotegemezi kupitia elimu hiyo ya ujasiliamali 
KATIBU WA UWT WILAYA YA SINGIDA MJINI BI MARGARET MALECELA AKIWA NA MWENYEKITI WA MUDA NA MGENI RASMI WA KUFUGUA MAFUZO HAYO HANNA CHURI AKIWA PAMOJA NA DIWANI WA KATA YA UTEMINI MH. BARTAZARI KIMARIO (picha Doris Meghji)
Naye diwani wa kata ya Utemini ambapo mafunzo hayo yanafanyika Mh. Bartazari Kimario ameweataka wanawake hao kuyatumia mafunzo hayo vizuri ili yawasaidie katika kuliendeleza taifa hili la Tanzania kwa kuwa wanawake ndio tegemeo la familia na taifa kwa ujumla.
Bi REHEMA SHILLA NA BAADHI YA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UJASILIAMALI YALIYOANDALIWA UWT -WILAYA YA SINGIDA MJINI ( picha na Doris Meghji)


Katika kuendesha mafunzo hayo ya ujasiliamali Mwezaji Lilian Nkida na Godwin Hillary toka shirika la kazi duniani (ILO) kupitia mpango wa kazi nje nje wamesema mafunzo hayo yatalenga maeneo makuu manne ambayo ni kujitambua, kubadilika kimtazamo,kubuni wazo la biashara na kuanzisha biashara yako.
WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UJASILIAMALI - YALIYOANDALIWA NA UWT -SINGIDA MJINI NA KUWEZESHWA NA ILO - KITENGO CHA KAZI NJE NJE.(picha na Doris Meghji)

Hata hivyo kupitia mpango huo wa serikali unaosimamamiwa na shirika la kazi duniani ILO zaidi ya vijana na wazee 800 wamepata mafuzo hayo mkoani Singida
Lilian Nkinda mwezeshaji wa mafunzo ya wanawake wa UWT- Singida mjini Kutoka ILO kitengo cha kazi nje nje(Picha na Doris Meghji)


Zaidi ya washiriki 25 toka wilaya ya singida ya mjini wamehudhuria mafunzo haya ya siku tatu yalionza jana na kumalizika kesho katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya wananchi manispaa ya singida 

KIJANA GODWIN HILLARY MWEZESHAJI WA MAFUZO YA UJASILIAMALI TOKA SHIRIKA LA KAZI DUNIANI  (ILO) KITENGO CHA KAZI NJE NJE(picha na Doris Meghji)

Hata hivyo kupitia mpango huo wa serikali unaosimamamiwa na shirika la kazi duniani ILO zaidi ya vijana 700 wamepata mafuzo hayo mkoani Singida

MWISHO

Wednesday, December 11, 2013

Safari ya mwisho ya Nelson Mandela katika misa maalum

Wakuu wa nchi mbalimbali duniani wawasili Afrika ya kusini kwa ajili ya safari ya mwisho ya Nelson Mandela

Raisi wa Marekani Barack Obama na mkew Michel Obama wakiwasili Afrika kusini kwa ajili ya kuhudhuria safari ya mwisho ya Nelson Mandela

Askofu Desmond Tutu mshind wa tuzoya nobeli ya amani

Katibu mkuu mstafu wa Umoja wa Mataifa Koffi Atta Anan akiwa na Askofu Desmond Tutu wakati wa misa maalum ya kumuombea Nelson Mandela


Baadhi ya wageni waalikwa katika misa ya kumuombea nelson Mandela katika uwanja wa FNB(Soccer city)

Raisi wa Marekani Barack Obama na mkewe wakifuatilia jambo wakati wa misa maalum



Pamoja na hali ya hewa kuwa mbaya watu walifuatilia misa waliwa na miavuli


Winnie Mandela na Graca Michael wakiomboleza msiba








Winnie Madikizela mandela pamoja na familia yake wakiwasili katika uwanja wa FNB kwa ajili ya misa maalum ya kumuaga baba wa taifa la Afrika Kusini Nelson Mandela



Friday, December 6, 2013

Na Evarista Lucas,
Singida
Alhamis Des 06,2013
Wadau wa sekta ya madini katika Halmashauri ya wilaya ya Singida, wameitaka wizara ya madini na nishati Tanzania  kuboresha maeneo muhimu ya huduma kwa wachimbaji wadogo Mkoani hapa.
Wakitoa maoni yao mapema leo katikasiku ya mwisho ya warsha ya Wadau wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikuta no wa Halmashauri ya Singida; wamesema ili sekta hii iwe na mafanikio ni lazima miundo mbinu yote ikiwemo maji, bara bara, umeme, mipango miji/vijiji na  huduma za afya iboreshwe ili kukidhi mahitaji ya wachimbaji wadogo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida Ndg Mnyampanda na mwezeshaji  Dr Mataro Sabai wakifuatilia jambo.Picha na Doris Meghji
Uanzishwaji wa vituo vya madini darasa ambavyo vitatumika katika kutoa elimu kwa wachimbaji katika hatua zote za uchimbaji, uaandaji na uchenjuaji wa madini ili kurahisisha kazi yao na kuepuka gharama za  kuyasafirisha nje ya mkoa kwa ajili ya kuyatengeneza.
Sanjari na hayo; wadau hao wamependekeza kuwa licha  ya kuboresha maeneo hayo nyeti, kuwepo na uwiano wa kijinsia katika shughuli za uchimbaji wa madini na umiliki wa vitalu vya machimbo.
Akifafanua juu ya hili mmoja wa wadau hao Bwana Elia Digha amesema; uwiano huu utawekwa kwa wizara kuwwawezesha haswa wanake ili nao wapate kushiriki katika uchimbaji wa madini kwa kuwapatia mitaji na mafunzo.
Wadau wakifuatilia wa sekta ya nishati na madini wakifuatilia mjadala.Picha na Doris Meghji
Digha amesema wanawake wengi wamekuwa wakiogopa kufanya kazi za uchimbaji kwa kuwa kazi kama hiyo inahitaji ujasiri.
Aidha; wadau hao wameongeza kusema kuwa ili wachimbaji hao wadogo waweze kufanikiwa watahitaji kupewa taarifa za mara kwa  masoko haswa bei za madini ili kuepusha suala la kuuza madini kwa bei ya chini.
Warsha hiyo ya siku tatu ambayo iliyoshirikisha madiwani, watendaji wa halmashauri na serikali  kuu na wafanyabiashara ; ilifunguliwa Desemba 3mwaka huu hapa mkoani singida  na kumalizika leo; ikiwa na lengo la kuwashirikisha wadau wa sekta ya madini katika kutoa maoni na kuandaa mpango katika kuchangia maendeleo ya wilaya kwa kupitia Sekta ya madini amabapo wilaya zitanufaika na shughuli za uchimbaji wa madini kwa kujiongezea pato.
Washiriki wa mafunzo ya ugatuaji wa madaraka sekta ya Nishati na Madini wakiwa katika mjadala ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Singida.Picha na Doris Meghji
 
Wadau wa Nishati na Madini wakifuatilia mjadala
Mpango huu wa maendeleo ya Sekta ya madini kwa kipindi cha mwaka  2014/2015 – 2015/2016 umekuwa ni muafaka kwa Mkoa wa Singida ambapo ugunduzi wa madini umefanyika  katika maeneo mbali mbali ya Wilaya hususani maeneo ya Mpambaaambapo madini yaliyogunduliwa na pamoja na dhahabu, shaba na fedha, mchanga, kokoto na mawe.
MWISHO

Wednesday, November 20, 2013

KUFUNGWA KWA MABUCHA 32 SOKO KUU MANISPAA YA SINGIDA

Na, Doris Meghji Jumatano Novemba 20,2013
Singida
Manispaa ya singida imeendelea kuwataka wafanyabiashara wa nyama katika mabucha 32 nyama yalioko soko kuu singida kutekeleza  amri ya manispaa hiyo kwa kuhakiksha wanafanya usafi wa mabucha yao ikiwa ni pamoja na kupima afya zao katika kutoa huduma hiyo ndani ya  manispaa Singida
 
Baadhi ya Mabucha ya soko kuu la Singida yakiwa yamefungwa

Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida  Joseph Mchina amesema hayo alipotembelewa na karibu Singida Blog kutaka kupata maelezo ya kufunga mabucha hayo 32 ya  soko kuu la manispaa ya singida kwa kipindi cha wiki mbili sasa
Joseph Mchina Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida - akiwa Ofisini kwake akiongea na karibusingida.blog
 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mchina amesema wamefunga mabucha hayo kutokana hali ya uchafu wa mazingira  uliokithiri kwenye mabucha hayo alisema “manispaa ilitoa siku 7  kwa wafanyabiashara hao wanyama wafanye usafi katika mabucha yao kwa kuweka maru maru (Tiles) kwenye sakafu na kuta za bucha zao,dirisha la kioo, kupata rangi,kuvaa sare nyeupe na kupima afya zao kwa wafanyabiashara hiyo ya nyama kwenye soko hilo baada ya siku saba kuisha na wao kukaidi amri na agizo la manispaa ikabidi tufunge mabucha ” kwa kuokoa afya za walaji na wakazi wa manispaa alisisitiza Mkurugenzi Mchina 
Mkurugenzi  wa Manispaa ya Singida Ndg.Joseph Mchina akiwa ofisini kwake


“Baada ya kufunga sasa ndio unaona malalamiko sisi tunachokitaka ni wao kufuata tulichoagiza atakayeweza kufanya hivyo nitatuma wataalam wangu wakakague na wakiridhika anaruhusiwa kuchinga na kuuza nyama kwenye mabucha hayo”alisema Mkurugenzi Mchina
mabucha - soko kuu singida yakiwa yamefungwa na kutoa huduma


Aidha kwa upande wa watumiaji wa kitowewo hicho ikiwa pamoja na wajasiliamali wanaouza chakula (Mama ntilie) katika maeneo mbali mbali ya manispaa hiyo amesema  kuna mabucha mnne ambayo wameyakaguliwa mitaani ndio yanayotoa huduma hiyo ya kuuza nyama kwa wakazi wa manispaa yake kwa sasa na kuwa ongezoko la uchinjaji wa ng’ombe umeongezeka ukilinganisha na kipindi cha nyuma kabla ya mabucha kufungwa


Mkurugenzi huyo amewataka wafanyabiashara hao kuzingatia kanuni na taratibu za usafi wa mazingira na kanununi za usafi wa vyakula kwa kuvaa sare kupima afya zao na kujikinga magonjwa ya kuambukiza  kwa biashara hiyo katika manispaa yake ikiwa ni pamoja na kulipa ushuru wa manispaa 
baadhi ya wamiliki wa mabucha soko kuu manispaa ya Singida


Awali wakitoa malalamiko yao baadhi ya wafanyabiashara akiwemo bwana  Zuberi Haji mfanyabiasha wa nyama katika kibanda namba 1 amesema kufungiwa mabucha kumewaathiri kwa kiasi kubukwa kwa kuwa yeye huuza ngombe wawaili kwa siku hivyo ameomba kuruhusiwa kufanyabiashara kwa kuwa yeye amekwisha karabati bucha lake.
Zuberi Haji mmiliki wa Bucha namba 1 soko kuu Singida

Wakati huo huo bwana Omary Ghambuna miliki wa mabucha mawili katika soko hilo amesema yeye ameathirika sana hasa katika suala la kipato kwa kufungwa mabucha hayo, kwakuwa kipato chake kinategemea shuhuli hiyo ya uuzaji wa nyama 
 
Omary Ghambuna kulia akiwa na wenzake katika mabucha ya soko kuu Singida

 Hata hivyo wameomba manispaa iwaruhusu watu waliokwisha karabati vibanda vyao na kufuata mashariti ,kuendelea na biashara kuliko kusubiri vibando vyote vikarabatiwe na kufanyiwa usafi kwa kuwa sio wote wenye uwezo wa kufanya hivyo 
akionyesha jinsi alivyokarabati bucha lake Zuberi Haji soko kuu manispaa ya Singida


Kwa upande wa manispaa kukosa mapato wafanyabiashara hao wamesema manispaa itakosa mapato kwa kuwa wao hulipa shilingi 10,000/= ya ushuru wa manisapaa  kwa mwezi na uwepo wao  urahisha wakazi na wajasiliamli kama akina mama ntilie kuendesha biashara zao kwa kutumia kitoweo cha nyama  kama suala la mtori,ndizi hutegemea kitoweo hicho ambacho ni bei rahis ukilinganisha na samaki, kwa kuwa bei ya kilo moja ya nyama ni shilling 5000/= huku bei ya kilo moja ya samaki ni shilingi 8000/=
Omary Ghambuna na wenzake akielezea juu ya suala hilo la kufungiwa mabucha na manispaa




Wiki mbili sasa tangu mabucha hayo 32 kufungwa, mabucha yamefungwa rasmi Novemba 8 mwaka huu  kwa uchafu uliokithiri kwa kuwataka wamiliki wa mabucha hayo kufanya usafi ikiwa ni pamoja na kukarabati vibanda hivyo kwa kuzingatia kanununi na taratibu za usafi wa mazingira na kanuni za afya ya vyakula ndani ya manispaa ya Singida.
Bucha namba  1  ukarabati wa kuweka vyoo katika bucha hilo