Na, Doris Meghji Ijumaa
Disemba 13 ,2013
Singida
Wanawake wametakiwa kutumia elimu ya
ujasilimali ili kujikwamua kiuchumi kwa kuwa wanawake ndio walezi wakuu wa
familia nchini
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya
Singida Bi Hanna Churi amewaasa wanawake hao katika mafunzo ya ujasilimali yaliondaliwa
kwa wanawake na wanachama wa jumuhiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT)
wilaya ya singida mjini kwa uwezeshaji toka shirika la kazi duniani (ILO) kupitia
mpango wa kazi nje nje yanayofanika katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya wananchi
manispaa ya Singida
Bi Hanna Churi na mwenyekiti wa muda katika mafuzo ya ujasiliamali yaliofanyika chuo cha maendeleo ya wananchi manispaa ya singida (picha na Doris Meghji) |
Aidha Bi Churi amewataka wanawake hao kutumia
fursa ya mafunzo ya ujasiliamali yakayowawezesha kutumia mbinu mbali
mbali katika kubuni miradi na kutafuta masoko ikiwa ni pamoja na kuimarisha
mahusiano ndani ya jamii
BAADHI YA WASHIRIKI WA MAFUZNO YA UJASILIAMALI - UKUMBI WA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI (FDC) SINGIDA ( picha na Doris Meghji) |
Kwa mujibi wa Afisa Maendeleo wa Jamii
huyo anasema “ kwa kupitia mafunzo haya ya siku tatu hii itawasidia kujenga na
kuimarisha mahusiano kati yenu na kuwa na sauti mmoja ndani ya jamii kwa kukutwanishwa
pamoja katika mafunzo haya ya ujasiliamali alisisitiza Bi Churi
AFISA MTENDAJI KATA YA UTEMINI BI EVA MBELWA NA KIJANA ANTONIA KATIKA MAFUNZO YA UJASILIAMALI - YALIOANDALIWA NA UWT SINGIDA MJINI (picha na Doris Meghji) |
Awali akisoma taarifa ya uandaaji wa
mafuzo hayo ya ujasiliamali Katibu wa
UWT wilaya ya mjini Bi Margaret K. Malecela ameeleza lengo la kuandaa mafunzo kwa
wanawake na wanachama wa jumuiya hiyo ni kuwaendeleza wanawake katika
kujikwamua kiuchumi na kujenga taifa lisilotegemezi kupitia elimu hiyo ya
ujasiliamali
Naye diwani wa kata ya Utemini ambapo
mafunzo hayo yanafanyika Mh. Bartazari Kimario ameweataka wanawake hao
kuyatumia mafunzo hayo vizuri ili yawasaidie katika kuliendeleza taifa hili la
Tanzania kwa kuwa wanawake ndio tegemeo la familia na taifa kwa ujumla.
Bi REHEMA SHILLA NA BAADHI YA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UJASILIAMALI YALIYOANDALIWA UWT -WILAYA YA SINGIDA MJINI ( picha na Doris Meghji) |
Katika kuendesha mafunzo hayo ya
ujasiliamali Mwezaji Lilian Nkida na Godwin Hillary toka shirika la kazi
duniani (ILO) kupitia mpango wa kazi nje nje wamesema mafunzo hayo yatalenga maeneo
makuu manne ambayo ni kujitambua, kubadilika kimtazamo,kubuni wazo la biashara
na kuanzisha biashara yako.
WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UJASILIAMALI - YALIYOANDALIWA NA UWT -SINGIDA MJINI NA KUWEZESHWA NA ILO - KITENGO CHA KAZI NJE NJE.(picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo kupitia mpango huo wa
serikali unaosimamamiwa na shirika la kazi duniani ILO zaidi ya vijana na wazee
800 wamepata mafuzo hayo mkoani Singida
Lilian Nkinda mwezeshaji wa mafunzo ya wanawake wa UWT- Singida mjini Kutoka ILO kitengo cha kazi nje nje(Picha na Doris Meghji) |
Zaidi ya washiriki 25 toka wilaya ya
singida ya mjini wamehudhuria mafunzo haya ya siku tatu yalionza jana na
kumalizika kesho katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya wananchi manispaa ya singida
KIJANA GODWIN HILLARY MWEZESHAJI WA MAFUZO YA UJASILIAMALI TOKA SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO) KITENGO CHA KAZI NJE NJE(picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo kupitia mpango huo wa
serikali unaosimamamiwa na shirika la kazi duniani ILO zaidi ya vijana 700
wamepata mafuzo hayo mkoani Singida
MWISHO
No comments:
Post a Comment