Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Wednesday, November 20, 2013

KUFUNGWA KWA MABUCHA 32 SOKO KUU MANISPAA YA SINGIDA

Na, Doris Meghji Jumatano Novemba 20,2013
Singida
Manispaa ya singida imeendelea kuwataka wafanyabiashara wa nyama katika mabucha 32 nyama yalioko soko kuu singida kutekeleza  amri ya manispaa hiyo kwa kuhakiksha wanafanya usafi wa mabucha yao ikiwa ni pamoja na kupima afya zao katika kutoa huduma hiyo ndani ya  manispaa Singida
 
Baadhi ya Mabucha ya soko kuu la Singida yakiwa yamefungwa

Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida  Joseph Mchina amesema hayo alipotembelewa na karibu Singida Blog kutaka kupata maelezo ya kufunga mabucha hayo 32 ya  soko kuu la manispaa ya singida kwa kipindi cha wiki mbili sasa
Joseph Mchina Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida - akiwa Ofisini kwake akiongea na karibusingida.blog
 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mchina amesema wamefunga mabucha hayo kutokana hali ya uchafu wa mazingira  uliokithiri kwenye mabucha hayo alisema “manispaa ilitoa siku 7  kwa wafanyabiashara hao wanyama wafanye usafi katika mabucha yao kwa kuweka maru maru (Tiles) kwenye sakafu na kuta za bucha zao,dirisha la kioo, kupata rangi,kuvaa sare nyeupe na kupima afya zao kwa wafanyabiashara hiyo ya nyama kwenye soko hilo baada ya siku saba kuisha na wao kukaidi amri na agizo la manispaa ikabidi tufunge mabucha ” kwa kuokoa afya za walaji na wakazi wa manispaa alisisitiza Mkurugenzi Mchina 
Mkurugenzi  wa Manispaa ya Singida Ndg.Joseph Mchina akiwa ofisini kwake


“Baada ya kufunga sasa ndio unaona malalamiko sisi tunachokitaka ni wao kufuata tulichoagiza atakayeweza kufanya hivyo nitatuma wataalam wangu wakakague na wakiridhika anaruhusiwa kuchinga na kuuza nyama kwenye mabucha hayo”alisema Mkurugenzi Mchina
mabucha - soko kuu singida yakiwa yamefungwa na kutoa huduma


Aidha kwa upande wa watumiaji wa kitowewo hicho ikiwa pamoja na wajasiliamali wanaouza chakula (Mama ntilie) katika maeneo mbali mbali ya manispaa hiyo amesema  kuna mabucha mnne ambayo wameyakaguliwa mitaani ndio yanayotoa huduma hiyo ya kuuza nyama kwa wakazi wa manispaa yake kwa sasa na kuwa ongezoko la uchinjaji wa ng’ombe umeongezeka ukilinganisha na kipindi cha nyuma kabla ya mabucha kufungwa


Mkurugenzi huyo amewataka wafanyabiashara hao kuzingatia kanuni na taratibu za usafi wa mazingira na kanununi za usafi wa vyakula kwa kuvaa sare kupima afya zao na kujikinga magonjwa ya kuambukiza  kwa biashara hiyo katika manispaa yake ikiwa ni pamoja na kulipa ushuru wa manispaa 
baadhi ya wamiliki wa mabucha soko kuu manispaa ya Singida


Awali wakitoa malalamiko yao baadhi ya wafanyabiashara akiwemo bwana  Zuberi Haji mfanyabiasha wa nyama katika kibanda namba 1 amesema kufungiwa mabucha kumewaathiri kwa kiasi kubukwa kwa kuwa yeye huuza ngombe wawaili kwa siku hivyo ameomba kuruhusiwa kufanyabiashara kwa kuwa yeye amekwisha karabati bucha lake.
Zuberi Haji mmiliki wa Bucha namba 1 soko kuu Singida

Wakati huo huo bwana Omary Ghambuna miliki wa mabucha mawili katika soko hilo amesema yeye ameathirika sana hasa katika suala la kipato kwa kufungwa mabucha hayo, kwakuwa kipato chake kinategemea shuhuli hiyo ya uuzaji wa nyama 
 
Omary Ghambuna kulia akiwa na wenzake katika mabucha ya soko kuu Singida

 Hata hivyo wameomba manispaa iwaruhusu watu waliokwisha karabati vibanda vyao na kufuata mashariti ,kuendelea na biashara kuliko kusubiri vibando vyote vikarabatiwe na kufanyiwa usafi kwa kuwa sio wote wenye uwezo wa kufanya hivyo 
akionyesha jinsi alivyokarabati bucha lake Zuberi Haji soko kuu manispaa ya Singida


Kwa upande wa manispaa kukosa mapato wafanyabiashara hao wamesema manispaa itakosa mapato kwa kuwa wao hulipa shilingi 10,000/= ya ushuru wa manisapaa  kwa mwezi na uwepo wao  urahisha wakazi na wajasiliamli kama akina mama ntilie kuendesha biashara zao kwa kutumia kitoweo cha nyama  kama suala la mtori,ndizi hutegemea kitoweo hicho ambacho ni bei rahis ukilinganisha na samaki, kwa kuwa bei ya kilo moja ya nyama ni shilling 5000/= huku bei ya kilo moja ya samaki ni shilingi 8000/=
Omary Ghambuna na wenzake akielezea juu ya suala hilo la kufungiwa mabucha na manispaa




Wiki mbili sasa tangu mabucha hayo 32 kufungwa, mabucha yamefungwa rasmi Novemba 8 mwaka huu  kwa uchafu uliokithiri kwa kuwataka wamiliki wa mabucha hayo kufanya usafi ikiwa ni pamoja na kukarabati vibanda hivyo kwa kuzingatia kanununi na taratibu za usafi wa mazingira na kanuni za afya ya vyakula ndani ya manispaa ya Singida.
Bucha namba  1  ukarabati wa kuweka vyoo katika bucha hilo




No comments:

Post a Comment