Na Evarista Lucas,
Singida
Alhamis Des 06,2013
Wadau wa sekta ya madini katika Halmashauri ya wilaya ya Singida, wameitaka wizara ya madini na nishati Tanzania kuboresha maeneo muhimu ya huduma kwa wachimbaji wadogo Mkoani hapa.
Wakitoa
maoni yao mapema leo katikasiku ya mwisho ya warsha ya Wadau wa madini
iliyofanyika katika ukumbi wa mikuta no wa Halmashauri ya Singida;
wamesema ili sekta hii iwe na mafanikio ni lazima miundo mbinu yote
ikiwemo maji, bara bara, umeme, mipango miji/vijiji na huduma za afya iboreshwe ili kukidhi mahitaji ya wachimbaji wadogo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida Ndg Mnyampanda na mwezeshaji Dr Mataro Sabai wakifuatilia jambo.Picha na Doris Meghji |
Uanzishwaji
wa vituo vya madini darasa ambavyo vitatumika katika kutoa elimu kwa
wachimbaji katika hatua zote za uchimbaji, uaandaji na uchenjuaji wa
madini ili kurahisisha kazi yao na kuepuka gharama za kuyasafirisha nje ya mkoa kwa ajili ya kuyatengeneza.
Sanjari na hayo; wadau hao wamependekeza kuwa licha ya
kuboresha maeneo hayo nyeti, kuwepo na uwiano wa kijinsia katika
shughuli za uchimbaji wa madini na umiliki wa vitalu vya machimbo.
Akifafanua
juu ya hili mmoja wa wadau hao Bwana Elia Digha amesema; uwiano huu
utawekwa kwa wizara kuwwawezesha haswa wanake ili nao wapate kushiriki
katika uchimbaji wa madini kwa kuwapatia mitaji na mafunzo.
Wadau wakifuatilia wa sekta ya nishati na madini wakifuatilia mjadala.Picha na Doris Meghji |
Digha amesema wanawake wengi wamekuwa wakiogopa kufanya kazi za uchimbaji kwa kuwa kazi kama hiyo inahitaji ujasiri.
Aidha; wadau hao wameongeza kusema kuwa ili wachimbaji hao wadogo waweze kufanikiwa watahitaji kupewa taarifa za mara kwa masoko haswa bei za madini ili kuepusha suala la kuuza madini kwa bei ya chini.
Warsha hiyo ya siku tatu ambayo iliyoshirikisha madiwani, watendaji wa halmashauri na serikali kuu na wafanyabiashara ; ilifunguliwa Desemba 3mwaka huu hapa mkoani singida na
kumalizika leo; ikiwa na lengo la kuwashirikisha wadau wa sekta ya
madini katika kutoa maoni na kuandaa mpango katika kuchangia maendeleo
ya wilaya kwa kupitia Sekta ya madini amabapo wilaya zitanufaika na
shughuli za uchimbaji wa madini kwa kujiongezea pato.
Washiriki wa mafunzo ya ugatuaji wa madaraka sekta ya Nishati na Madini wakiwa katika mjadala ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Singida.Picha na Doris Meghji |
Wadau wa Nishati na Madini wakifuatilia mjadala |
Mpango huu wa maendeleo ya Sekta ya madini kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 – 2015/2016 umekuwa ni muafaka kwa Mkoa wa Singida ambapo ugunduzi wa madini umefanyika katika
maeneo mbali mbali ya Wilaya hususani maeneo ya Mpambaaambapo madini
yaliyogunduliwa na pamoja na dhahabu, shaba na fedha, mchanga, kokoto na
mawe.
I LIKE YOUR BLOG AND STORIES. KEEP INTOUCH MA DIA
ReplyDelete