kuku wakikusanywa kwa ajili ya kusafilishwa -katika soko kuu la singida |
Na, Doris Meghji Jumanne Oktoba 29,2013
Singida
Wafanyabiashara wa kuku soko kuu manispaa
ya singida wameiomba serikali ya manispaa hiyo kuwajengea mabanda ya kuhifadhia
kuku wao kabla ya kuwasfisha kwa kuwa mabanda yalioko sasa hataoshelezi
ukilinganisha na idadi za kuku wanaonunuliwa na kuandaliwa kusafirisha kuku hao
baadhi ya mabanda ya kuhifadhia kuku- kabla ya kuwasafirisha |
Akiongea kwa niaba ya wafanya biashara
wa kuku hao manispaa ya singida Kijana Abdulilah Monko ametoa ombi hilo leo
katika soko kuu la singida kwa kuomba serikali na mamlaka ya manispaa ya
singida kuwajengea mabanda yatakayokidhi mahitaji ya wafanyabiashara hao katika
kipindi cha kukusanya kuku kwa ajili ya kuwasfirisha kwenda Dar- es salaam kwa
ajili ya kuuzwa
kijana Abdulilai Monko mmoja wa wafanyabiashara wa kuku soko kuu la singida akiandaa tenga la kubebea kuku |
“sisi tunatoa ushuru wa shilingi elfu
18,000/= kwa kila tenga hivyo ushuru huu watutengenezee mabanda na suala la
upatikanaji wa maji kipindi cha kuwaandaa kuwasafirisha kuku wetu,maana huwa
tunasafirisha mara mbili kwa wiki”alisisitiza kijana Monko.
Kwa mujibu wa kijana Monko ameelezea
kuwa tenga mmoja huweza kupakia kuku 70 hadi 80 kwa tenga.
Aidha kuhusu suala la hali ya biashara
hiii amesema biashara sio mbaya wala nzuri ni kutoka na mzunguko wa fedha
kutokuwa mzuri kwa kuwa hivi sasa wanakusanya kuku kwa shilingi 7000/= hadi
800/= na wao kuuza shilingi elfu 10,000/= hadi 13,000/= kwa kuku mmoja
Hata hivyo biashara ya kuku ni moja ya
zao la biashara la mkoa wa singida kwa kuwa na kuku wengi wakienyeji.
Mmoja wa vijana wa mkoa wa Singida aliyejikita katika biashara ya kuku ( Picha na Doris Meghji) |
Ni eneo ambalo kuku wa kieneji wanapatikana ndani ya manispaa ya Singida ( Picha na Doris Meghji) |
Huyu ni mfanyabiashara maarufu wa kuku wa kienyeji soko kuu la Singida ( Picha na Doris Meghji) |
Ni vijana na biashara ya kuku wa kienyeji mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji) |