Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Thursday, October 3, 2013

DC EDWAERD OLE LENGA - AKATAA TAARIFA YA BARABARA YA WILAYA YA MKALAMA KUJADILIWA KWENYE KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOANI SINGIDA

Na, Doris Meghji  Jumatatu  Septemba 24,2013
Singida

Singida Mkuu wa wilaya ya Mkalama Edward Lenga amekiomba kikao cha 35 cha bodi ya barabara(ROADBOARD) mkoani Singida  kutojadili  taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara ya Wilaya hiyo kutokana taarifa hiyo kuwa ya ni ya kupika kwa kuandaliwa na mkurugenzi wa wilaya ya Iramba na sio mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama .

Akitoa ombi hilo kwa mwenyekiti wa kikao hicho cha bodi ya barabara mkoa wa Singida ambaye ni mkuu wa mkoa wa singida DKT. Parseko Kone  mara baada ya taarifa ya  miradi ya barabara wilaya ya Mkalama kusomwa mbele ya mweneyekiti na wajumbe wa kikao hicho mkuu wa wilaya ya mkalama Bwana Edward Lenga alisema “hakuna kujadili habari juu ya Mkalama asilimia 53 fedha zimetumika kwa kazi gani? Wakati hakuna miradi yoyote ya barabara inayotekelezwa wilayani mkalama? Alisema mkuu huyo wa wilaya 

Hivyo mkuu huyo wa wilaya amekiomba kikao hicho cha bodi ya barabara kuunda kamati ili iende kutembelea na kuangalia miradi hiyo ya barabara iliyoonyeshwa kwenye taarifa hiyo. 

Awali akiosoma taarifa hiyo ya wilaya ya mkalama Mbele ya wajumbe wa kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya mkalama bwana Hassan Mwachibuzi  alisema katika mwaka wa fedha 2013/2014 wilaya ya mkalama imeidhinishiwa jumla ya shilingi milioni 879,981757.00 kwa ajili ya ukarabati na matengezo ya kawaida,matengenezo ya sehemu korofi ,matengenezo ya sehemu maalum na matengenezo ya madaraja kwa kipindi hicho cha fedha.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya mkalama, mkurugenzi halmashauri  wa wilaya ya mkalama amesema katika ya kipindi cha Julai – Agosti 2013 toka mfuko wa barabara iliidhinishwa jumla ya shilingi milioni 464 431,450.00 kwa mwaka wa fedha 2012/2013 hadi kufikia Agosti 30, 2013 sawa na asilimia 100 ya bajeti hivyo hadi sasa jumla ya shilingi million 246,032,563.00 ya fedha zimetumika sawa na  asilimia 53 za matengenezo ya barabara iliyopokelewa wilayani humo.

 Hata hivyo kikao hicho kimeridhia kuundwa kwa kamati itakayokwenda  kupitia miradi ya barabara ya wilaya ya mkalama na kuwataka wajumbe wa kikao hicho toka Mkalama kuainisha miradi ya barabara wanazotilia shaka lengo ilikiwa ni kurahisisha utekelezaji wa kamati hiyo kwa kuwa wananchi wanazihitaji barabara hizo kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla. 

Wilaya ya mkalama ni moja kati ya wilaya zalizoundwa hivi karibuni ambapo wilaya hiyo umeundwa toka wilaya ya Iramba mkoani singida .

Mwisho 

No comments:

Post a Comment