Na, Doris Meghji Jumatano Oktoba 09,2013
Singida
Suala uongezaji wa hali ya kipato ni
hitaji la kila mtanzania ili kuboresha maisha yake,ni jambo jema hasa kwa
mtazania kutumia njia halali za kujiongeza kipato hicho.Hili limejidhiirisha
wazi kwa baadhi ya wakazi wa mkoa wa Singida hasa wanaoishi ndani ya manispaa
hii ya Singida
Nalisema hili kwani limejiidhiirisha kwa
ongezeko la ujenzi
mbali mbali wa nyumba za kuwapangisha wanafunzi wa taasisi za elimu zilizoko
ndani ya manispaa hii.
Hii nina lenga kwa taasisi ya uhasibu na
utumishi wa umma hizi ni taasisi mbili tu ninazoweza kutolea mfano kwa wananchi
wa manispaa hii hasa wenye viwanja na nyumba karibu na maeneo ya taasisi hizo
kwa kujihakikishia kipato kutokana na malipo ya kuwapangisha wanafunzi hao wa
taasisi hizo kila mwaka wa masomo unapoaanza kwa kweli hili limabadilisha hadhi
na hali ya kipato cha wanasingida kwa kuwa chumba kimoja hupangisha wanfunzi
wawili hadi wanne kwa kila mwanfuzi kulipa 150,000/= kwa muhula.
Ni moja ya nyumba za kupangisha wanafunzi -pembeni ujenzi wa nyumba zingine ukiendelea ndani ya manispaa ya singida |
Hivi sasa ujenzi wa hostel au nyumba za
kuwapangisha wanafuzi hao umeongezeka kila kukucha kwani ndio limekuwa
suluhishao la kipato kwa baadhi ya wananchi wa manispaa hiii kwa fursa hiyo
kuwafikia mlangoni mwao.
Kweli hii inaweza kuwa fursa nzuri kwa
wakazi wa manispaa ya singida kwa kipato kuongezeka Je kwa upande wa wanafunzi
wanaliiongeleaje suala hilo la kupangisha nyumba kwa ajili ya wao kuishi katika
kipindi hiki cha masomo?
Wanafunzi wanasema nini juu ya uwepo wa
hoteli hizo za watu binafsi? Kijana Laurance mmoja wa wanafunzi wa chuo cha
uhasibu anashukuru kwa uwepo wa hosteli hizo kwani ni hosteli hizo za watu
binafsi zinavyumba vikubwa na ziko kwenye muonekano mzuri kwa wanafunzi kuishi.
Aidha amesema “kwa kipindi hiki hosteli
zimeongezeka hadi kufikia kupangisha wanafunzi wawili kwa chumba kwa bei ya
shilingi 150,000/= kwa muhula kweli sijasikia lawama yoyote toka kwa
wanafunzi.alisema kijana Laurance.
Je taasisi husika zinalichukuliaje suala
hili la wanafunzi wao kupanga nyumba kwa watu binafsi katika kipindi hiki cha
masomo?
Kwa mujibu wa Bwana Emmanuel Kingu
meneja wa taasisi ya uhasibu tawi la Singida amesema ujenzi wa nyumba hizo toka
kwa watu binafsi kumekuwa msaada mkubwa kwa taasisi hiyo kwani imesaidia kusajili
kiasi kukubwa cha wanafunzi kutokana na uwepo wa nyumba hizo katika manispaa hii
kwani tawi lake linauwezo wa kuwahudumia wanafunzi 120 tu, katika kipindi cha
mwaka wa masomo 2012 tawi hilo liliweza kusajili zaidi ya wanafunzi 3200
Aidha meneja huo amesema kutokana na
mpango au sera za nchi ya (Public Private
Partnership) ambapo serikali imeachia shughuli zingine ifanywe na watu binafsi
suala hilo la ujenzi wa hostel au mabweni kwa ajili ya wanafunzi kuishi katika
kipindi chote cha masomo yao zinafanywa na watu binafsi katika tawi lake.
Hadi sasa zaidi ya nyumba au hosteli 20
zimejengwa na kupangisha wanafuzi hao manispaa ya singida.
No comments:
Post a Comment