Na, Doris
Meghji Jumanne Julai 23,2013
Singida
Serikali mkoani
singida imeziagiza mamlaka za serikali za mitaa kuongeza juhudi katika
kuwawasidia wananchi wake kwa halmashauri
hizo kununua mashine tano za kupura zao la mtama ikiwa ni moja ya jitihada za kutatua
changamoto zinazolikabili zao
hilo kwa uzalishaji kuleta
tija likiwa ni zao la kipaumbele mkoani Singida
Mkuu wa mkoa wa
Singida Dr. Parseko Kone ametoa agizo hilo katika kikao cha wadau wa maendeleo
kikao ambacho kililenga kuwawezesha wananchi kupunguza upotevu wa zao la mtama
baada ya mavuno kutokana na teknolojia duni zinazotumika katika kupura na
kuhifadhi zao hilo.
“nimefuatilia
wananchi wa singida wanapata shida sana wakati wa kuvuna mtama au uwele kwa
kupiga ualika watu katika kupura mtama, watu ishirini (20) wanapura gunia mmoja
kwa siku moja ili kuwasaidia wananchi kuachana na adha hiyo ya kupura mtama
tutafute namna ya kupata hizo mashine ambayo mmoja inauzwa shilling milioni 2
kwa kila halmashauri kununua mashine tano(5) na kuziweka makao makuu ya kata
iliyovuna vizuri mazao hayo ya mtama na uwele” alisisitiza Dr. Kone.
Aidha amesema
kupatikana kwa mashine hizo zenye uwezo wa kupura mtama gunia 10 kumi kwa saa
kutasaidiwa wananchi kutumia muda na kuhifadhi mazingira kwa kuwa upuraji wa
mtama kwa njia ya kawaida
utumia matawi ya mti, hivyo matawi ishrini hutumika kupura gunia mmoja la mtama
kwa siku.
Kwa upande wake
katibu tawala msaidizi wa uchumi na uzalishaji Bi Aziza Mumba amezitaja
changamoto mbali mbali zinazolikabili zao hilo kuwa ni upatikanaji mdogo
wambegu bora,athari za magugu hatari yanayoitwa viduha, ndege waharibifu aina
quelea quelea ikiwa ni pamoja na teknologia
duini zinazotumika katika kupura na kuhifadhi mtama inayosababisha upotevu
mkubwa wa mtama kwa kupoteza asilimia 30 ya mazao baada ya mavuno.
Aidha kwa mujibu
wa bi Mumba amesema katika kuogenzea thamani mazao hayo ya mtama na uwele
juhudi mbali mbali zinaendelea,suala la uenezaji wa matumizi ya mashine za
kupura mtama ili kumpuguzia mkulima uzito wa kazi za kilimo.
Mkoa wa singida
katika kipindi cha msimu wa kilimo mwaka 2010/2011 hadi 2011/2012 zaidi ya tani
476090 zilivunwa za mazao ya mtama na uwele
MWISHO.
No comments:
Post a Comment