Martinez alijibabatiza mpira na kuudondoshea kwenye nyavu za timu yake sekunde ya 69 katika jitihada za kuokoa mpira uliopigwa Wayne Rooney.
United inapanda kileleni baada ya Shakhtar kufungwa 4-0 na Bayer Leverkusen ikitimiza pointi saba baada ya mechi tatu.
Kikosi cha Man Utd: De Gea, Rafael/Smalling dk59, Jones, Evans, Evra, Valencia, Carrick, Giggs, Kagawa, Hernandez/Young dk80 na Rooney.
Real Sociedad: Bravo, Carlos Martinez, Mikel Gonzalez, Martinez, De la Bella, Vela, Zurutuza/Castro dk75, Markel, Prieto/Pardo dk68, Griezmann na Seferovic/Agirretxe dk75.
Katika mechi nyingine zilizochezwa usiku huu, CSKA Moskva imelala 2-1 mbele ya Manchester City. Mabao ya City yalifungwa na Sergio Aguero dakika za 34 na 42, yote pasi za Negredo, wakati bao la wenyeji lilifungwa na Tosic dakika ya 32, pasi ya Honda.
Mabao mawili ya Cristiano Ronaldo dakika ya nne na 29 yameipa Real Madrid ushindi wa 2 - 1 dhidi ya Juventus, ambayo bao lake lilifungwa na Llorente dakika ya 22.
Galatasaray imeifumua mabao 3 - 1 Kobenhavn, mabao yake yakifungwa na Felipe Melo dakika ya 10, Wesley Sneijder dakika ya 38 na Didier Drogba dakika ya 45, wakati bao pekee la wapinzani wao limefungwa na Claudemir dakika ya 88.
Anderlecht imefungwa nyumbani 5-0 na PSG, Zlatan Ibrahimovic akifunga mabao manne dakika za 17, 22, 36 na 62, lingine likifungwa na Cavani dakikya 51, wakati Benfica imelazimishwa sare ya 1 - 1 nyumbani na Olympiakos Piraeus.
Mabingwa watetezi, Bayern Munich wameendeleza umwamba, baada ya kuifumua Viktoria Plzen 5-0, mabao ya Ribery dakika ya 25 na 61, Alaba dakika ya 37, Schweinsteiger dakika ya 64 na Gotze dakika ya 90. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment