Katibu - TLB Mwl. Boniface Kitiku siku ya Fimbo nyeupe |
Na, Doris Meghji Jumatano Oktoba 16,2013
Singida
Serikali nchini
Tanzania imeombwa kuingiza fimbo nyeupe kuwa moja kati ya alama za
barabarani, lengo likiwa ni kuwasaidia wasiona wanapotumia fimbo hizo kwenye barabara hizo nchini.
Akito maoni hayo katibu wa chama cha
wasiona manispaa ya Singida (Tanzania Legue for Blind)(TLB) Mwalimu Boniface Kitiku alipokuwa akifanya mahojiano na Karibu
Singida Blog katika siku ya fimbo nyeupe ikiwa ni moja ya changamoto
zinazowakabili walemavu hao katika manispaa ya Singida
Katibu - Tanzania League for Blind- Singida Municipal Council |
“Madereva wengi na watembea kwa miguu
bado hawazijua fimbo nyeupe hivyo kwa niaba ya chama cha wasiona tunaomba
serikali iweke fimbo nyeupe iwe kati ya moja za alama za barabarani kwa kuwa madereva na watu wengine bado hawajazitambua fimbo njeupe, hii uwapa ugumu na
kutojiamini kwa wasiona kutumia fimbo hizi bila kuwa mtu wa kumsaidia barabarani”alisisitiza
Mwalimu huyo.
Aidha ameiomba serikali kufanya juu
chini kutafuta wataalamu hapa nchini ili wavitumie vyuo vya ufundi stadi vya
VETA vitengeneze fimbo hizo nyeupe lengo likiwa ni kuwafikia wasiona wengi kwa bei
nafuu ukilinganisha na sasa fimbo hizo huagizwa toka nje ya nchi yetu na fimbo
moja huuzwa shilingi 18000/= hiyo ikiwa ni mipango ya muda mrefu na mipango
ya muda mfupi ni kuiomba serikali kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kuziagiza fimbo hizo kwa wingi ili kuisadia jamii hiyo
ya walemavu ya wasiona nchini.
Mmoja wa walimu wa chuo cha wasiona - Manispaa ya Singida |
Hata hivyo ameongela pia suala la
upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia na
kufundishia vya walemavu hao huagizwa toka nje ya nchini hivyo kuwa gharama
kubwa kwa mutu wenye ulemavu kuendelezwa kielimu hasa elimu ya sekondari nchini
katibu wa TLB mkoa wa Singida |
Hii imejiidhirisha wazi toka kwa
wanafunzi wanawake toka chuo cha wasiona manispaa ya Singida wakiongelea suala
la wao kutengwa kwa kutoendelezwa kielimu mara baada ya kumaliza elimu yao ya
msingi.
Siku ya fimbo nyeupe uadhimishwa Oktoba 18 kila
mwaka, kitaifa siku hii ya fimbo nyeupe inaadhimisha mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment