Na, Doris Meghji Jumatatu Oktoba 07,2013
Singida.
Maadhimisho ya wiki ya UWT Wilaya ya Singida Mjini
Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya
ya singida mjini yaombwa kufanya makongano mbali mbali katika vyuo na taasisi
za elimu zilizopo ndini ya manispaa ikiwa ni moja ya njia ya kuzungumza na
vijana vyuoni katika suala zima la kuwafundisha maadili kwa wanafunzi hao.
Mwenyekiti wa UWT_wilaya ya Singida Mjini Bi Consolatha Mzilay akimkaribisha mgeni Rasmi kufungua kongamano |
Katibu wa UWT_Singida Mjini Bi Margaret Malecela akisoma risala ya kongamano kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg.Selestin Yunde |
Akitoa ombi hilo katika kuchangia mada rais wa chuo cha uhasibu tawi la Singida
Bi Marium Suleiman mara baada ya mada ya “Kujitambua
kama kijana wa kike kuwa ndio Taifa la kesho ”iliyotolewa na Bi Yagi
Kiaratu Diwani viti maalum Manispaa ya Singida na katibu wa uwt wilaya ya
Ikungi rais huyo ameiomba jumuhiya hiyo kutembelea taasisi ya uhasibu lengo
likiwa ni kuwabadilisha vijana hasa wasichana katika suala zima la maadili ili waweze
kubadilika kwa kutumia makongamano kama haya.
Wajumbe wakifuatilia mjadala |
“Jitihada mbali mbali tumefanya katika
kukabiliana na tatizo la uvaaji usiokuwa wa maadili wa wanafunzi wetu, kwa
kipindi hiki wanafunzi haruhusiwi kuvaa suruali au nguo zozote zenye kuonyesha
mauongo ya mwanamke kwa wasichana na
wavulana pia katika ofisi za uongozi wa chuo na hawaruhusiwi kuingia
darasani wakiwa wamevaa nguo hizo.lakini
bado tunahitaji nguvu kutoka kwenu mama zangu tungependa makongamano kama haya
hasa ya maadili ili wanafunzi waweze kubadilika nakujitambua kwa kuwa chuo
chetu kimekuwa na sifa mbaya katika manispaa hii na kwa watu wanaoishi maeneo
karibu na taasisi hiyo alisisitiza rais wa chuo hicho cha uhasibu.
Hata hivyo katika kujadili mada hiyo
wasichana toka katika chuo cha wasioona watoa kilio chao cha kuatili kwa watoto
walemavu kwa kufanyiwa ubaguzi majumbani kwa kutothamini hasa pale wanapomaliza
sekondari na kutakiwa kwenda kuolewa badala ya kendeleza kielimu hivyo wameomba
wazazi na walezi kutowabagua watoto na wasichana wenye ulemavu.
Aidha kwa upande wake Katibu wa UWT
wilaya Singida Mjini Bi Margaret Malecela alieleza lengo la kuandaa kongamano
hilo la Vijana katika kuadhimisha wiki ya UWT mwaka huu ni kuwajenga na
kuwaelimisha vijana wa kike kuijua na kuitambua jumuhiya hiyo ya wanawake
ambapo jumla ya wasichana sitini toka katika vyuo vya uhasibu,VETA,Wasiona
Maendeleo ya wananchi,na Sekondari ya Misuna walishriki katika kongamano hilo.
Wiki ya Umoja wa wanawake Tanzania huanza
kuaadhimisha Septemba 28 hadi Oktoba 04 kila mwaka.
No comments:
Post a Comment