Na,Doris Meghji Alhamisi Oktoba 10,2013
Singida
Wananchi wa mkoa wa singida wataanza
kuonja matunda mafaniko ya ujenzi wa hospitali ya rufaa mara baada ya serikali
ya mkoa huo kununua vifaa tiba kwa majengo matatu yaliokamilika katika mradi
huo wa ujenzi wa hospitali rufaa mkoani hapa
Tumaini hilo limekuja kwenye kikao cha
ushauri cha mkoa wa singida kilichofanyika Septemba 25 katika ukumbi wa VETA ndani
ya manispaa ya Singida
Mkuu wa mkoa wa singida Dr. Parseko Kone
ametoa tumani hilo kwa kuleta hoja na kuomba ridhaa ya kikao hicho kuridhia
kukopa kiasi cha shilling milioni 500 toka katika mfuko wa Bima ya afya (NHIF)
ukiwa ni mpango wa serikali ya mkoa wa
singida kuanza kutoa huduma kwa kutumia majengo yaliyokamilika ambayo ni jengo
la wagonjwa wanje (OPD) jengo la uchunguzi wa wanawake na watoto (OBS) na jengo
la kufanyia uchunguzi wa magonjwa mengine (DIAGNOSTIC) kwa fedha hizo kununulia
vifaatiba,vifaa vingine na samani za majengo yote matatu
Kwa Mujibu wa mkuu huyo wa mkoa ameelezea juu ya uanzishwaji
wa mradi huo wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ni kutokana na sababu mbali mbali
ambazo ni ongezeko la wagonjwa,uchakavu wa miundo mbinu ya maji na umeme, eneo dogo
la kiwanja ilipo hospitali ya mkoa,kukosekana kwa idara muhimu na vifaa ili
kutoa huduma bora za kibingwa katika kutekeleza sera za wizara ya afya na
ustawi wa jamii
Kukamilika kwa mradi huo wa hospitali ya
rufaa kutasaidi kutoa huduma bora za tiba na kinga kwa wananchi wa mkoa wake,
ikiwa ni pamoja na kutoa huduma zote za rufaa kwa wananchi wa mkoa wa singida
na mikoa jirani hivyo kupunguza gharama za rufaa.
Kukamilika kwa ujenzi wa hospitali hiyo
ya rufaa kutagharimu kiasi cha shilingi 150,000,000,000/= za kitanzania kwa
ujenzi wa majengo 37 yenye uwezo wa vitanda 1000
Mradi wa ujenzi wa hospitali ya rufaa
ulianza kutekelezwa mwaka wa fedha mwaka 2008/2009 kwa serikali kutoa zaidi ya
shilling billion 2 na mwaka wa fedha 2009/2010 kiasi cha shilingi billion
2,027,436,000/=
Mwisho
No comments:
Post a Comment