Na, Doris Meghji Ijumaa Oktoba 11,2013
Singida
Jeshi la polisi mkoani singida kupitia
dawati la Jinsia linakabiliwa na changamoto mbali mbali katika kutekeleza
majukumu yake
ikiwa pamoja na umbali na ukubwa wa eneo, mila potofu na uwelewa mdogo wa sheria
miongoni wa jamii mkoani humo.
Hayo yamejidhiirisha wazi wakati wa
mahojiano na Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi mkoa wa singida SSP Cordula
Lyimo kwa niaba ya kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa singida ACP Geofrey
Kamwela juu ya dawati la jinsia linavyofanya kazi mkoani hapo.
Aidha Afisa Mnadhimu huyo wa Jeshi la
Polisi ameyataja makosa mbali mbali ambayo jamii imkekuwa ikiyafanya na kuripotiwa katika dawati hilo kuwa ni
kubaka,kumpa mimba mwanafunzi,kulawiti ,kutupa watoto, shambulio la aibu
,kujeruhi, kutishia kuua kwa maneno ,kutelekeza famila na mauaji
Kwa mujibu wa Afisa Lyimo amesema makosa
mengi ya mauji husababishawa zaidi na wivu wa kimapenzi,imani za kishirikina na
hofu ya kutambulika baada ya kubaka.
Katika kufuatilia kesi za ubakaji
amesema kesi nyingi za ubakaji zinashindwa kumalizika vizuri na kuishia kufutwa
kutokana na ushrikiano duni toka kwa wahusika walifanyiwa kitendo au mashahidi
Hata hivyo Afisa huyo wa jeshi la polisi
amesema jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia limejipanga vyema kuendelea
kutoa elimu kwenye vitongoji,vijiji kata,tarafa na wilaya kwa kutumia askari kata,askari wa dawati la
jinsia na mtandao wa wanawake wa jeshi la polisi,ikiwa ni pamoja na kuwaomba
wananchi kuondoa dhana ya mila na desturi zinazoumiza wananchi .
jumla ya makosa 47 ya ukatili la kijinsia
yameripotia katika dawati la jinsia mkoani singida katika kipindi ya Januari
hadi Mei mwaka huu.
No comments:
Post a Comment