Na, Doris Meghji Jumamos 12, 2013
Singida
Serikali na taasisi za dini zimeombwa
kuasaidia watu wenye ulemavu kwa kuwa jamii haikubali kuishi na watu wenye
ulemavu na kuona kama ni balaa ndani ya famila zao kwa kuwaficha katika upataji
wa huduma muhimu za afya na elimu kwa
watu wenye ulemavu mkoani hapa
Idd Hassan Kinguju Katibu wa SHIVYAWATA Mkoa wa Singida |
Katibu wa Shirikisho la vyama vya
walemavu Tanzania (SHIVYAWATA) mkoa wa Singida Bwana Idd Hassan Kinguju ametoa
ombi hilo jana alipohojiwa kuhusu siki ya
mtoto wa kike duniani.
mmoja wa wanafunzi wa chuo cha wanaweke walwmavu cha wasiona mkoa wa Singida |
Kwa mujibu wa katibu huyo amesema katika
kupata elimu walemavu wana shule chache na sio za bweni hivyo ni vigumu kupata
elimu kwa watu wenye ulemavu hivyo ameiomba serikali kutengeneza mazingira
rafiki kwa watu wenye ulemavu kiuchumi ili kuendesha shughuli zao za kila siku
katibu wa SHIVYAWATA - Mkoa wa Singida |
Hata hivyo bwana Kinguju ameendelea kutoa
wito kwa jamii isiwafiche watu wenye ulemavu kwa kuona watu wenye ulemavu ni
balaa bali waone ni zawadi toka kwa Mwenyezi Mungu
mwalimu toka chuo cha walemavu wanawake wasiona - mkoa wa singida |
Kwa upande wa wanafunzi wa chuo cha
wasiona mkoani singida baadhi ya wanafunzi wenye wanelalamikia suala la wao
kutoendelezwa kielimu bara baada ya kumaliza elimu yao ya msingi katika shule
hizo maalum kwa kulazimishwa kwenda kuolewa kutokana na ulemavu wao
Wasichana hao wa chuo cha wasiona wameiomba jamii na
serikali kuwajengea mazingira rafiki ya wao kendelea na elimu ya sekondari na
sio kuishia katika ngazi hiyo ya elimu kwakuwa wao ni kama wasichana wengine.
Kwa kipindi cha mwaka 2012 wasiona 50 tu
ndio walioko kwenye cha cha wasiona mkoani singida.
Kauli mbiu ya siku ya mtoto wa kike
duniani “Chochea ubunifu kuboresha elimu kwa mtoto wa kike” siku ya mtoto wa
kikie duniani huazimishwa Oktoba 11 kila mwaka.
Baadhi ya walemavu albino na walemavu wa viongo na wasiona katika wakiserebuka katia ukumbi wa VETA singida |
No comments:
Post a Comment