Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Sunday, December 29, 2013

UFAULU WA WANAFUNZI DARASA LA SABA SINGIDA WAONGEZEKA

Na   Evarista Lucas
Singida
Desemba 28, 2013

Imeelezwa kuwa; kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 2013 kimeongezeka kwa asilimia 17.56 ikilinganishwa na kiwango cha ufaulu cha asilimia 23.16 kwa mwaka 2012.

Hayo yamesemwa mapema leo katika kikao cha bodi ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza mwaka 2014; na Afisa Elimu mkoa wa Singida Bibi Fatuma Kilimia wakati akiwasilisha muhtasari wa matokeo ya darasa la saba  mwaka 2013 mapema leo katika ukumbi wa RC Mission mjini Singida.

Aidha Kilimia ameongeza kusema kuwa, licha ya kuongezeka kwa kiwango hicho cha ufaulu kwa asilimia 17;  bado kuna changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na kuathiri utoaji taaluma bora hapa mkoani.

Amesema, ili kuzikabili changamoto hizo; sekta ya elimu imeazimia kuendesha mafunzo ngazi ya Klasta na Kata ya masomo yenye utata na kusoma, kuandika na kuhesabu kwa kutumia njia ya ‘Lesson Study’ kwa kutumia Walimu bingwa,na  kubaini Walimu Wakuu wasiowajibika ipasavyo na kuwavua Madaraka.

Sanjari na hayo ni Halmashauri kuwawezesha Wakaguzi ili shule zikaguliwe kwani ukaguzi ndiyo kioo cha taaluma na pia kusikiliza na kutatua kero za Walimu.

Kwa upande mwingine imefahamika kuwa walimu wengi wamekuwa hawafanyi kazi zao kwa ufasaha kutokana na changamoto mbali mbali zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku na kubwa zaidi ikiwa ni madeni.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wajumbe wakikao hicho  cha bodi ya uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2014 wamesema; walimu wengi wamezidisha mikopo hali inayowafanya washindwe kufanya kazi ya ufundishaji kwa ufasaha kwa kutumia muda wao mwingi kuwaza namna ya kulipa madeni yanayowakabili.

Akichangia katika mada katika kikao hicho; mjumbe na mwenyekiti wa huduma za jamii Halmashauri ya wilaya ya Singida Bwana Elia Digha amesema ni jukumu la wakuu wa Wilaya na wakurugenzi kuhakikisha kuwa walimu wanafanya kazi yao ipasavyo na kuepuka mikopo mikubwa zaidi,

Digha amesema; walimu wengi wamekuwa wakichukua mikopo mikubwa ambayohuongezeka riba pale wanaposhindwa kulipa deni na kujikuta na deni kubwa kuliko kiasi walichokopa. Akisisitiza hilo; Digha amesema ukopaji huo hufikia hatua mbaya ya kuwalazimu walimu(Wakopaji) kuaccha kadi zao za Benki kwa wadeni wao kitendo kinachowaathiri hadi kwenye utendaji kazi wao.

Kwa upande  wake diwani wa Itigi Bwana Alli Minja  amesema ni suala la ukopaji ni la mtu binafsi na si kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuwazuia kukopa, minja amesema kuwa walimu wengi wanaokopa ni kwa tamaa zao ni kuwa kuwazuia ni kazi ngumu labda kuwapeleka nyumba za ibada wakaombewe ili pepo hilo la ukopaji litoke.

Amesema , haitoshi kudhibiti viwango vya mikopo kwa walimu kutoka katika asasi mbali mbali za serikali kwaani bado kuna watu binafsi wanaondesha shughuli hiyo ya ukopeshaji na walimu hukimbilia huko kukopa.
 
MWISHO

Saturday, December 21, 2013

Askari Singida auwawa

Na Evarista Lucas
Singida ,
Desemba 21,2013
Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida Zakaria William mwenye namba D.6466 D/SGT  amepoteza maisha papo hapo mapema jana baada ya kupigwa risasi iliyopenya shingoni mwake na mtu anayesadikiwa ni jambazi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mapema leo katika ofisi yake; Kamanda wa Polisi mkoani Singida Bwana Geofrey Kamwela amesema tukio hilo la kusikitisha limetokea majira ya saa nne na nusu  za usiku katika kijiji cha Tambukareli katika kata ya Majengo iliyopo wilayani Manyoni mkoani hapa.

Kamanda Kamwela ameeleza kuwa;  tukio hilo limetokea wakati askari huyo akiwa  katika doria na askari wenzie walipopata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa katika nyumba moja ya mali ya Stanley Mpaki (Almaarufu kama Babu Mpaki) mfanyabiashara na mkulima anaishi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.

Baada ya kupata taarifa hizo marehemu na wenzie walifika katika nyumba hiyo ambapo  baadhi ya askari waliingia ndani ili kuwakamata watuhumiwa na  marehemu alikuwa amebaki nje ambapo alipigwa risasi na mmoja kati ya majambazi hao aliyetoroka kusikojulikana na kupoteza maisha papo hapo.

Katika nyumba hiyo watu wanne wamekamatwa ikiwa ni pamoja na bunduki aina ya SMG yenye namba UA ikiwa na risasi ishirini na tano ndani ya magazine moja na bastola moja ya kienyeji yenye uwezo wa kutumia risasi za shotgun pamoja na risasi saba.

Aidha; Kamanda Kamwela amewataja majambazi waliokamatwa  ktika tukio hilo ni pamoja na Joseph Hemed mwenye umri wa miaka ishirini na tisa mkulima na mkazi wa Siuyu, Ikungi; Juma Ramadhan miaka ishirini mkulima na mkazi wa Kizota, Dodoma; Abdallah Hamis ini na moja, miaka ishirmkulima na mkazi wa Milera Ikungi na Stanley Mpaki miaka ishirini na minane mkazi wa Itigi ambao walitambuliwa kuwa ni wahalifu wazoefu kutokana na kuhusika kwao katika matukio mbali mbali ya uhalifu wa kutumia silaha.

Sanjari na hayo Kamanda Kamwela amesema Jeshi la polisi Mkoani hapa linaendelea na uchunguzi wake juu ya tukio hilo  ikiwa ni pamoja na kumsaka mtuhumiwa aliyetoroka na uchunguzi utakapoakamilika watuhumiwa hao watafikishwa  mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Kwa upande wa Jeshi la Polisi  mkoa wa Singida hili ni tukio la pili ambalo limepelekea askari wake wawili kupoteza maisha wakiwa kazini, ambapo askari wa kwanza  alipoteza maisha katika oparesheni tokomeza majangiri huko Manyoni baada ya kushambuliwa na majangiri.

Kwa upande mwingine  Kamanda Kamwela amesema umilikaji silaha kinyume cha sheria ndiko kunakopelekea kuibuka kwa vitendo vya ujambazi na kuwashukuru  raia wema wote ambao wamekuwa wakitoa  ushirikiano kwa jeshi la polisi na kuongeza kuwa uhai wa askari marehemu Zakaria umepotea kutokana na silaha haramu.

Pia;  Kamanda Kamwela ametoa wito kwa wananchi wote kuendelea  na moyo wa kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhusu uhalifu au wahalifu na matishio mengine ya usalama ili yafanyiwe kazi haraka na kuepusha madhara kwa watu na mali.
 

MWISHO

Friday, December 20, 2013

Habari zilizotufikia punde, Rais Kikwete atengua uteuzi wa mawaziri wanne leoDisemba 20, 2013

Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amesema kwamba Rais Kikwete amekubali kutengua nyadhifa za mawaziri wanne kufuatia ripoti ya 'Operesheni Tokomeza' iliyotolewa mapema leo bungeni. 

Mawaziri hao waliotenguliwa nyadhifa zao ni: Mhe. David Mathayo David  alyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki  aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Emmanuel Nchimbi  aliyekuwa waziri wa Mambo  ya ndani ya nchi na Mhe. Shamsi Vuai Nahodha aliyekuwa waziri wa Ulinzi. 

Mhe. Hamis Kagasheki alitangaza kujiuzulu mapema kabla uamuzi huo uliotangazwa na Waziri Mkuu

Wednesday, December 18, 2013

HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI YAPITISHA BAJETI YA MWAKA 2014/2015



Na, Doris Meghji Jumatano Disemba 17, 2013
Singida

 Halmashuri ya Ikungi imepitisha leo  jumla  shilingi billion 25, 696,823,389/= ikiwa ni  makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi  kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 ikiwa ni bajeti ya kwanza tangu kuanzishwa kwa halmashauri hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi DC.Msambia Mwenyekiti wa halmashuri ya wilaya ya Ikungi,Selestine Iyunde ,Ally Nkanghaa makamu Mwenyekiti na mwenyekiti wa ccm Wilaya ya Ikungi Hasan Tati kaikia kiko cha bajeti (Picha na Doris Meghji)


Akitoa taarifa hiyo Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Diwani kata ya Mtunduru Mh.Ally Nkanghaa akisoma taarifa hiyo kwenye baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Singida
 
Makamu Mwenyekiti wa halmashuri ya wilaya ya Ikungi Mh. Ally Nkanghaa akisoma taarifa ya makadiriao ya bajeti ya mwaka 2014/2015( Picha na Doris Meghji)
Makamu mwenyeikiti wa halmashauri hiyo ya Ikungu ametaja makadirio hayo kuwa ni shilingi billion 15,426,684,431/= kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa halmashuri hiyo i,shilingi billion 1,992,180,869/=ikiwa ni ruzuku ya matumizi ya kawaida,shilingi billion 7,544,787,045/= ruzuku ya miradi ya maendeleo huku vyanzo ya ndani ikiwa shilingi milioni 723,171,044/= na kufanya jumla shilingi billion 25,696,823,389/= kwa kipindi cha mwaka 2014/2015
Baadhi ya madinwani wa halmashuri ya wilaya ya Ikungi wakisikiliza hoja za kikao hicho cha bajeti Halmashauri ya wilaya ya Ikungi (Picha na Doris Meghji)


Kwa mujibu wa Makamu mwenyekiti huyo amesema “bajeti hii ni nzuri tatizo ni fedha kuchelewa kufika kwa wakati kama kipindi cha fedha kilichopita tulipitisha bajeti ya billion 16 fedha hazikuja na zilikuja billion 4 tu tena kwa kuchelewa husababisha kutotekelezwa miradi ya  wananchi hivyo tunaomba serikali kuu kuleta fedha kwa wakati”alisisitiza Mh. Nkanghaa.
baadhi ya wataalam wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi katika kikao hicho cha Bajeti (Picha na Doris Meghji)


Aidha katika kuleza juu ya mapato ya ndani amesma  halmashauri ya wilaya ya Ikungi imebuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na asilimia 000.3% ya mapato toka katika migodi ya madini iliyopo kwenye halmashauri ya wilaya ya Ikungu,mnara ya simu ya kampuni za simu za Voda com,Aitel,na Tigo vyanzo vingine ni toka katika mazao ya misitu kama mkaa,mbao huku asilimia 3% ya kodi za ardhi ya michango ya kodi ya viwanja na mashamba
Christana Mughwahyi mbunge viti Maalum Chadema akifuatilia kikoa cha bajeti cha halmashauri ya wilaya ya Ikungi(Picha na Doris meghji)


Naye mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu amesema suala la kuchangia miradi ya maendeleo kwa wananchi ni hiari hivyo amewataka wananchi wake kutolazimishwa kuchangia miradi hiyo ya maendelo kwa kuwa wanalipa kodi. “kwa kuwa mmeita michango maana yake ni hiari ukilazimisha sio michango hiyo ni kodi na kodi zina sheria zake za kuongoza."alisema Mbunge Lissu 
Mh. tundu Lissu akichangia hoja ya bajeti ya halmashuri ya wilaya ya Ikungi katika baraza la madinaini (picha na Doris Meghji)


Christowaja Mtinda mbunge wa viti Maalum (CHADEMA)  naye ameendelea kusisitiza suala la wananchi kutolazimishwa kuchangishwa michango mbali mbali ya miradi ya maendeleo kwa kuwa wananchi wanalipa kodi, hivyo serikali inawajibu wa kutekeleza miradi hiyo kupitia kodi wanazolipa wananchi wa halmashauri hiyo.
Mbunge Viti maalum Chadema Mh.Christowaja Mtinda akichanjia bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya Ikungi (Picha na Doris Meghji)


Hata hivyo baraza hilo limebitisha zaidi ya shilingi billion 25, 696/= kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 kwa ombi la fedha hizo kufika kwa wakatia lengo likiwa ni utekezaji wa miradi ya wananchi kwa wakati.
diwani wa viti maalum Hellena Hamisi Misughaa  akichangia bajeti hiyo ya halmashuri ya Wilaya ya Ikungi (Picha na Doris Meghji)

Mwisho

Tuesday, December 17, 2013

AJALI

Na  Doris Meghji Jumanne Disemba 17,2013
Singida

Ajali imetokea leo majira ya saa 6 mchana katika eneo la Manguanjuki takribani km 3 karibu na mzani wa kupimia magari katika Manispaa ya Singida, ajali hiyo imehusisha gari la kubeba mizigo aina ya VOLVO lenye namba za usajili T 477 BDX ambapo mmiliki wake hakujulikana mara moja. Shuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa ajali hiyo imetokana na mwendokasi na hivyo kupoteza mwelekeo na kupinduka, katika ajali hiyo hapakuwa na majeruhi.
Gari aina ya VOLVO lenye namba za usajiri T477 BXD likiwa limepinduka eneo la Manguanjuki karibu na eneo la mizani katika Manispaa ya Singida(Picha na Doris Meghji)

Shuhuda wa ajali hiyo Ndg Njiku akiongea na karibusingida.blogspot




Baadhi ya mashuhuda wakitazama ajali hiyo leo 17/12/2013(Picha na Doris Meghji)

Monday, December 16, 2013

SEKTA YA MADINI NA UGATUAJI



Na, Doris meghji  Jumanne Disemba 17,2013
Singida – Sekta ya Madini
Bendera za halmashauri ya wilaya ya Singida (picha na Doris Meghji)


Halmashauri ya wilaya ya Singida zinatarajiwa kunufaika kutokana na mpango sera ya ugatuaji (Decentralization by Devolution) wa sekta ya madini nchini kwa serikali kuzitaka halmashauri kuzingiza shughuli za uchimabaji wa madini kwenye mipango yako kwa maendeleo ya wilaya hizo
 
MMWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA MH. DIWANI MNYAMPANDA KATIKA WARSHA YA WADAU SEKTA YA MADINI (Picha na Doris Meghji)
Kunufaika kwa halmashauri ya wilaya ya Singida kunakuja kutokana mpango wa kuingiza shughuli za madini katika mfumo wa mpango wa maendeleo ya halmashuri, hivyo kuipa fursa sekta ya madini kushiriki kikamilifu kutoa mchango wake katika maendeleo ya halmashauri
Dr. Mataro Sabai Mshauri mkuu EBF mwezeshaji wa warsha ya wadau wa sekta ya madini halmashuri ya wilaya singida Picha na Doris Meghji)


Kijiji cha Mpambaa ndani ya halmashauri ya wilaya ya Singida kutainufaisha halmashauri hiyo kwa uwepo wa wachimbaji wadogo wa madini katika eneo hilo kupitia sera ya ugatuaji katika sekta ya madini nchini
wadau wa sekta ya madini  halmashauri ya wilaya ya Singida katika warsha ya ugatuaji wakitoa maoni katika vikundi (picha na Doris Meghji)


haya yamejitokeza katika warsha ya wadau wa sekta ya madini wilayani singida yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashuri ya wilaya ya Singida chini ya uwezeshaji wa Dr Mataro Sabai mshauri mkuu toka kampuni ya Economic and Business Foundation (T) LTD ya jijini Dar- es- salaam ikiwa ni mpango wa maendeleo ya sekta ya madini katika kipindi cha  2014/15  hadi 2015/16.
mmoja ya kundi la wadau wa sekta ya madini katika warsha ya wadau wa madini halmashuri ya wilaya ya singida wakijadili mambo ya kuandaa mipango na muongozo


Kwa mujbu wa sera hiyo ya ugatuaji lengo la serikali kupeleka sera hiyo ya sekta ya madini ni kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinaingizwa kwenye mipango ya halmashauri ili iweze kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya wilaya 
kundi lingine la wadau wakijadili mambo muhimu ya kuweka katika mipamgo na muogozo wa ugatuaji (picha na Doris Meghji)


Aidha ushirikishwaji wa sekta ya madini katika maendeleo ya wilaya kutaharakisha maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa huduma hususini zinazotakiwa kwa maendeleo ya wachimbaji wadogo
mmoja wa washiriki katika kundi bajeti akiwasilisha bajeti ya kuendesha sekta ya madini katika mipango ya maendeleo ya halmashauri (Picha na Doris Meghji)
 

Kwa upande wa washiriki na wadau wa warsha hiyo maoni mbali mbali ya ugatuaji ya sera katika sekta ya madini yametoliwa ni pamoja na malengo ya kuwepo kusajili na kuwatambua wachimbaji wadogo,kuwa sheria ndogo za kijiji zinazowezesha kijiji na halmashauri husika kunufaika na shughuli za uchimbaji madini na kuimarisha huduma za jamii katika maeneo ya wachimbaji madini na inayozunguka migodi.
washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia uwasilishwaji wa mipango mbali mbali katika ugatuaji wa sekta hiyo kwa halmashuri(Picha na Doris Meghj)

Kwa upande wa mikakati wadau wa sekta ya madini katika warsha hiyo amependekeza upatikanaji wa huduma za mawasilino za uhakika katika maeneo ya madini,bara bara za uhakika zinazopitika majira yote ya mwaka kwenda kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo wa mpambaa na maeneo ya masoko ya madini ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za afya maeneo ya wachimbaji 



Aidha suala la mafunzo kwa wachimbaji wadogo 70 halikusaulika katika warsha hiyo kwa wachimbaji wadogo kupatiwa mafunzo juu ya jinsi ya kuendesha shughuli za madini kwa tija na namna ya kupata mitaji kutoka kwenye vyombo vya fedha
wadau wakifuatila mambo ya kuweka katika mipango na muongozo wa ugatuaji wa sekta ya madini katika halmashauri ya wilaya ya singida (picha na Doris Meghji)



Hata hivyo kwa wakati huu shughuli za madini kwa kiasi kikubwa zinafanyika nje ya mfumo wa mipango halmashuri, na  maeneo ya madini kutohudumiwa ipasanyvo kwa kuwa shughuli hizo kisheria ziko nje ya uwezo wa halmashuri. Hivyo ugatuaji huo utasidia kusogeza huduma karibu na jamii kwa halmashauri husika kutoa huduma hizo kwa wadau wa sekta hiyo.
mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya singida Mh.  Nyampanda Diwani wa kata ya Mtinko akifunga warsha ya wadau sekta ya madini (picha na Doris Meghji)

Madini ya dhahabu,shaba,fedha,mchanga mawe na kokoto yamegundilika katika halmashauri hiyo hasa katika eneo la Mpambaa 
Mwisho.

Sunday, December 15, 2013

Safari ya mwiso ya Nelson Rolihlahla Mandela

Oprah Winfrey pamoja na waombolezaji wengine wakifuatilia maziko ya Rais mzalendo wa kwanza wa Afrika kusini Nelson Mandela kijiji Qunu katika jimbo la Eastern Cape

Jeneza lililobeba mwili wa Raisi wa kwanza wa Afrika kusini likiwa linawasili eneo la maziko katika kijiji cha Qunu

Jeneza likiwa limepambwa kwa bendera ya Afrika kusini pia chini pakiwa pametandikwa ngozi ya ng'ombe
Hapa ndipo ilifanyika sala kabla ya kuelekea makaburini

Mizinga ishirini na moja ilipigwa kuonesha heshima kwa Rais wa kwanza mzalendo Nelson Rolihlahla Mandela

Rais mstaafu wa Afrika kusin Thabo Mbeki akisalimia na Askofu mstaa na mshindi na tuzo yz amani ya Nobel Desmond Tutu

Muombolezaji akifuatilia maziko kijijini Qunu

Mjane wa Nelson Rolihlahla Mandela,Graca Machael akiwa na majonzi wakati wa mazishi

Hapakuwa na tofauti, Winnie Madikizela Mandela akimshika Graca Michael kuaga jeneza na Rais mzalendo wa kwanza Nelson Rolihlahla Mandela

Mandle Mandela kiongozi wa kimila wa ukoo wa Mandela

Rais Jacob Zuma akihutubia waombolezaji

Winnie Madikizela Mandela,Rais Jacob Zuma na mjane wa Rais mstaafu wa Afrika kusini Nelson Rolihlahla Mandela Graca Michael wakiwa na nyuso za huzuni
R.I.P TATA NELSON ROLIHLAHLA MANDELA
1918-2013