Waziri
Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amesema kwamba Rais Kikwete amekubali kutengua
nyadhifa za mawaziri wanne kufuatia ripoti ya 'Operesheni Tokomeza' iliyotolewa
mapema leo bungeni.
Mawaziri hao waliotenguliwa nyadhifa zao ni: Mhe. David Mathayo David
alyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki
aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Emmanuel Nchimbi aliyekuwa
waziri wa Mambo ya ndani ya nchi na Mhe. Shamsi Vuai Nahodha aliyekuwa waziri wa Ulinzi.
Mhe. Hamis Kagasheki alitangaza kujiuzulu mapema kabla uamuzi huo uliotangazwa
na Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment