Na, Doris meghji Jumanne Disemba 17,2013
Singida – Sekta ya Madini
Bendera za halmashauri ya wilaya ya Singida (picha na Doris Meghji) |
Halmashauri ya wilaya ya Singida
zinatarajiwa kunufaika kutokana na mpango sera ya ugatuaji (Decentralization by
Devolution) wa sekta ya madini nchini kwa serikali kuzitaka halmashauri kuzingiza
shughuli za uchimabaji wa madini kwenye mipango yako kwa maendeleo ya wilaya hizo
MMWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SINGIDA MH. DIWANI MNYAMPANDA KATIKA WARSHA YA WADAU SEKTA YA MADINI (Picha na Doris Meghji) |
Kunufaika kwa halmashauri ya wilaya ya
Singida kunakuja kutokana mpango wa kuingiza shughuli za madini katika mfumo wa
mpango wa maendeleo ya halmashuri, hivyo kuipa fursa sekta ya madini kushiriki
kikamilifu kutoa mchango wake katika maendeleo ya halmashauri
Dr. Mataro Sabai Mshauri mkuu EBF mwezeshaji wa warsha ya wadau wa sekta ya madini halmashuri ya wilaya singida Picha na Doris Meghji) |
Kijiji cha Mpambaa ndani ya halmashauri
ya wilaya ya Singida kutainufaisha halmashauri hiyo kwa uwepo wa wachimbaji
wadogo wa madini katika eneo hilo kupitia sera ya ugatuaji katika sekta ya
madini nchini
wadau wa sekta ya madini halmashauri ya wilaya ya Singida katika warsha ya ugatuaji wakitoa maoni katika vikundi (picha na Doris Meghji) |
haya yamejitokeza katika warsha ya wadau
wa sekta ya madini wilayani singida yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
halmashuri ya wilaya ya Singida chini ya uwezeshaji wa Dr Mataro Sabai mshauri mkuu toka kampuni ya Economic and Business
Foundation (T) LTD ya jijini Dar- es- salaam ikiwa ni mpango wa maendeleo ya
sekta ya madini katika kipindi cha 2014/15 hadi 2015/16.
mmoja ya kundi la wadau wa sekta ya madini katika warsha ya wadau wa madini halmashuri ya wilaya ya singida wakijadili mambo ya kuandaa mipango na muongozo |
Kwa mujbu wa sera hiyo ya ugatuaji lengo
la serikali kupeleka sera hiyo ya sekta ya madini ni kuhakikisha shughuli
za uchimbaji zinaingizwa kwenye mipango ya halmashauri ili iweze kuchangia kikamilifu
katika maendeleo ya wilaya
kundi lingine la wadau wakijadili mambo muhimu ya kuweka katika mipamgo na muogozo wa ugatuaji (picha na Doris Meghji) |
Aidha ushirikishwaji wa sekta ya madini
katika maendeleo ya wilaya kutaharakisha maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa
huduma hususini zinazotakiwa kwa maendeleo ya wachimbaji wadogo
mmoja wa washiriki katika kundi bajeti akiwasilisha bajeti ya kuendesha sekta ya madini katika mipango ya maendeleo ya halmashauri (Picha na Doris Meghji) |
Kwa upande wa washiriki na wadau wa
warsha hiyo maoni mbali mbali ya ugatuaji ya sera katika sekta ya madini yametoliwa
ni pamoja na malengo ya kuwepo kusajili na kuwatambua wachimbaji wadogo,kuwa
sheria ndogo za kijiji zinazowezesha kijiji na halmashauri husika kunufaika na
shughuli za uchimbaji madini na kuimarisha huduma za jamii katika maeneo ya
wachimbaji madini na inayozunguka migodi.
washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia uwasilishwaji wa mipango mbali mbali katika ugatuaji wa sekta hiyo kwa halmashuri(Picha na Doris Meghj) |
Kwa upande wa mikakati wadau wa sekta ya
madini katika warsha hiyo amependekeza upatikanaji wa huduma za mawasilino za
uhakika katika maeneo ya madini,bara bara za uhakika zinazopitika majira yote
ya mwaka kwenda kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo wa mpambaa na maeneo ya
masoko ya madini ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za afya maeneo ya wachimbaji
Aidha suala la mafunzo kwa wachimbaji
wadogo 70 halikusaulika katika warsha hiyo kwa wachimbaji wadogo kupatiwa
mafunzo juu ya jinsi ya kuendesha shughuli za madini kwa tija na namna ya
kupata mitaji kutoka kwenye vyombo vya fedha
wadau wakifuatila mambo ya kuweka katika mipango na muongozo wa ugatuaji wa sekta ya madini katika halmashauri ya wilaya ya singida (picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo kwa wakati huu shughuli za madini
kwa kiasi kikubwa zinafanyika nje ya mfumo wa mipango halmashuri, na maeneo ya madini kutohudumiwa ipasanyvo kwa
kuwa shughuli hizo kisheria ziko nje ya uwezo wa halmashuri. Hivyo ugatuaji huo
utasidia kusogeza huduma karibu na jamii kwa halmashauri husika kutoa huduma
hizo kwa wadau wa sekta hiyo.
mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya singida Mh. Nyampanda Diwani wa kata ya Mtinko akifunga warsha ya wadau sekta ya madini (picha na Doris Meghji) |
Madini ya dhahabu,shaba,fedha,mchanga mawe
na kokoto yamegundilika katika halmashauri hiyo hasa katika eneo la Mpambaa
Mwisho.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment