Na Doris Meghji Jumanne Disemba 17,2013
Singida
Ajali imetokea leo majira ya saa 6 mchana katika eneo la Manguanjuki takribani km 3 karibu na mzani wa kupimia magari katika Manispaa ya Singida, ajali hiyo imehusisha gari la kubeba mizigo aina ya VOLVO lenye namba za usajili T 477 BDX ambapo mmiliki wake hakujulikana mara moja. Shuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa ajali hiyo imetokana na mwendokasi na hivyo kupoteza mwelekeo na kupinduka, katika ajali hiyo hapakuwa na majeruhi.
|
Gari aina ya VOLVO lenye namba za usajiri T477 BXD likiwa limepinduka eneo la Manguanjuki karibu na eneo la mizani katika Manispaa ya Singida(Picha na Doris Meghji) |
|
Shuhuda wa ajali hiyo Ndg Njiku akiongea na karibusingida.blogspot |
|
Baadhi ya mashuhuda wakitazama ajali hiyo leo 17/12/2013(Picha na Doris Meghji) |
No comments:
Post a Comment