Na, Doris Meghji Jumatano Disemba 17,
2013
Singida
Halmashuri
ya Ikungi imepitisha leo jumla shilingi billion 25, 696,823,389/= ikiwa ni makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 ikiwa ni
bajeti ya kwanza tangu kuanzishwa kwa halmashauri hiyo.
Akitoa taarifa hiyo Makamu Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Ikungi Diwani kata ya Mtunduru Mh.Ally Nkanghaa akisoma
taarifa hiyo kwenye baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi
katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Singida
Makamu Mwenyekiti wa halmashuri ya wilaya ya Ikungi Mh. Ally Nkanghaa akisoma taarifa ya makadiriao ya bajeti ya mwaka 2014/2015( Picha na Doris Meghji) |
Makamu mwenyeikiti wa halmashauri hiyo
ya Ikungu ametaja makadirio hayo kuwa ni shilingi billion 15,426,684,431/= kwa
ajili ya mishahara ya watumishi wa halmashuri hiyo i,shilingi billion 1,992,180,869/=ikiwa
ni ruzuku ya matumizi ya kawaida,shilingi billion 7,544,787,045/= ruzuku ya
miradi ya maendeleo huku vyanzo ya ndani ikiwa shilingi milioni 723,171,044/= na
kufanya jumla shilingi billion 25,696,823,389/= kwa kipindi cha mwaka 2014/2015
Baadhi ya madinwani wa halmashuri ya wilaya ya Ikungi wakisikiliza hoja za kikao hicho cha bajeti Halmashauri ya wilaya ya Ikungi (Picha na Doris Meghji) |
Kwa mujibu wa Makamu mwenyekiti huyo
amesema “bajeti hii ni nzuri tatizo ni fedha kuchelewa kufika kwa wakati kama
kipindi cha fedha kilichopita tulipitisha bajeti ya billion 16 fedha hazikuja
na zilikuja billion 4 tu tena kwa kuchelewa husababisha kutotekelezwa miradi ya
wananchi hivyo tunaomba serikali kuu
kuleta fedha kwa wakati”alisisitiza Mh. Nkanghaa.
baadhi ya wataalam wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi katika kikao hicho cha Bajeti (Picha na Doris Meghji) |
Aidha katika kuleza juu ya mapato ya
ndani amesma halmashauri ya wilaya ya
Ikungi imebuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani ikiwa ni pamoja na asilimia
000.3% ya mapato toka katika migodi ya madini iliyopo kwenye halmashauri ya
wilaya ya Ikungu,mnara ya simu ya kampuni za simu za Voda com,Aitel,na Tigo
vyanzo vingine ni toka katika mazao ya misitu kama mkaa,mbao huku asilimia 3%
ya kodi za ardhi ya michango ya kodi ya viwanja na mashamba
Christana Mughwahyi mbunge viti Maalum Chadema akifuatilia kikoa cha bajeti cha halmashauri ya wilaya ya Ikungi(Picha na Doris meghji) |
Naye mbunge wa jimbo la Singida
Mashariki Mh. Tundu Lissu amesema suala la kuchangia miradi ya maendeleo kwa
wananchi ni hiari hivyo amewataka wananchi wake kutolazimishwa kuchangia miradi
hiyo ya maendelo kwa kuwa wanalipa kodi. “kwa kuwa mmeita michango maana yake ni
hiari ukilazimisha sio michango hiyo ni kodi na kodi zina sheria zake za kuongoza."alisema
Mbunge Lissu
Mh. tundu Lissu akichangia hoja ya bajeti ya halmashuri ya wilaya ya Ikungi katika baraza la madinaini (picha na Doris Meghji) |
Christowaja Mtinda mbunge wa viti Maalum
(CHADEMA) naye ameendelea kusisitiza
suala la wananchi kutolazimishwa kuchangishwa michango mbali mbali ya miradi ya
maendeleo kwa kuwa wananchi wanalipa kodi, hivyo serikali inawajibu wa
kutekeleza miradi hiyo kupitia kodi wanazolipa wananchi wa halmashauri hiyo.
Mbunge Viti maalum Chadema Mh.Christowaja Mtinda akichanjia bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya Ikungi (Picha na Doris Meghji) |
Hata hivyo baraza hilo limebitisha zaidi
ya shilingi billion 25, 696/= kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 kwa ombi la fedha
hizo kufika kwa wakatia lengo likiwa ni utekezaji wa miradi ya wananchi kwa
wakati.
diwani wa viti maalum Hellena Hamisi Misughaa akichangia bajeti hiyo ya halmashuri ya Wilaya ya Ikungi (Picha na Doris Meghji) |
Mwisho
No comments:
Post a Comment