Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Tuesday, July 7, 2015

MHASHAMU ASKOFU EDWARD MAPUNDA KASIMKWA RASMI KUWA KIONGOZI MKUU WA JIMBO KATOLIKI LA SINGIDA

Na, Doris Meghji  Jumanne Julai 07,2015
Singida – ASKOFU KUSIMKWA


Watumikizi wakiwa tarayi kwa maandanamano ya kelekea Mabula stand kwa ajili ya sherehe na misa takatifu ya Kumsimika Mhashamu Askofu Edrwad Mapunda (Picha na Doris Meghji)

Kanisa Katoliki Jimbo la Singida limemsimika rasmi   Mhashamu Askofu Edwad Mapunda Kuwa askofu na kiongozi wa kanisa hilo mkoani Singida akiwa padre kwanza  kusimkwa kuwa askofu toka jimbo katoliki la Singida.

Jopo la Maaskofu toka majimbo zaidi ya 35 wakielekeza Mabula Stand eneo ambalo Misa takatifu ya kumsimika Mhashamu Askofu Edward Mapunda wa Jimbo katolikila Singida 9 Picha na Doris Meghji)

Katika sherehe za kumsika Mhashamu baba Askofu  Edward Mapunda Mhashamu baba askofu Mapunda  ambaye kauli mbiu yake  ya Umoja na Mapendo  amehaidi kushikiana vizuri na maaskofu wenzeke kwa kuomba ushauri kwa viongozi hao wakuu wa kichungaji katika daraja hilo takatifu la Uaskofu.
Padre Francis Limu kushoto katikati Mhashamu Askofu Edward Mapunda wakielekea Mabula Stand katika misa takatifu ya mkusimikwa kwa Mchungaji mkuu huyo jimboni katoliki Singida ( Picha na Doris Meghji)

Aidha kwa upande mwengine amesema atashirikiana vizuri na viongozi mbali mbali wa serikali,vyama vya siasa viongozi wa dini na madhebu mbali mbali katika kuliongoza taifa la Mungu katika nafasi hiyo ya kichungaji jimboni Singida ikiwa ni pamoja na kuendeleza mazuri yote ayalioachwa na Mhashamu Askofu Desiderius Rwoma ambaye kwa sasa ni askofu wa jimbo katoliki la Bukoba.
Brass band toka seminari ya Rubya jimbo katoliki la Bukoba ikitumbuiza katika sherehe hizo za kumsika askofu Edrwad Mapunda ( Picha na Doris Meghji)
Awali Askofu mkuu Franscis Padilla Balozi wa baba Mtakatifu nchini Tanzania amempongeza Askofu Edward Mapunda kwa kusimikwa rasmi kuwa askofu na mchungaji mpya wa jimbo katoliki la Singida kwa kuwa yeye ndio chagulo la Mungu alilomchagua uliongoza kanisa hilo.Hivyo amewataka waumini na kanisa kwa ujumla kumpokea na  kumuombea kiongozi wao na kumkubali na kumtaka Mhashamu askofu Mapunda kuwa kiongozi na sio kujiona yee ni goliati bali awe mfano wa mchugaji mwema
Jopo la Maaskofu toka majimbo zaidi ya 35 wakielekeza Mabula Stand eneo ambalo Misa takatifu ya kumsimika Mhashamu Askofu Edward Mapunda wa Jimbo katolikila Singida 9 Picha na Doris Meghji)
hivyo amemtaka ashrikiane vizuri na viongozi wa serikali na  jamii kwa kuwa wao wanahitaji sana msaada wa kanisa katika kuiongoza jamii amemtaka asililiza pale anapotakiwa kusikiliza na kuongea atakapotakiwa kuongea huku akitakiwa kisimama katika kweli na haki bila ubaguzi wowote.
Kwaya ya shirikisho ya jimbo katoliki la Singida ikitumbuiza katika Misa Takatifu ya kumsimika rasmi Mhashamu Askofu Edward Mapunda ( Picha na Doris Meghji)
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Singida Daktari Parseko Kone  akiwa mgeni mahusisi katika Kusimikwa kwa Mhashamu Askofu Mapunda ameomba kuliomba taifa hili la Tanzania amani usalama na utulivu katika pindi hii cha uchaguzi cha uchagua rais wabunge na madiwani hivo serikali ya mkoa wa Singida itaendelea kutoa ushrikiano nakuomba ushauri pale watakapo hitaji kwa kanisa hilo.
Kwaya ya shirikisho ya jimbo katoliki la Singida ikitumbuiza katika Misa Takatifu ya kumsimika rasmi Mhashamu Askofu Edward Mapunda ( Picha na Doris Meghji)
Mpiga kinanda akikitekenya kindanda kwa madaha wakati wa kumsimika rasmi mhashamu Askofu Edward Mapunda kwenye sherehe za kusimikwa kwake ( Picha na Doris Meghji)
MWISHO. 
Ally Amanzi Mkuu wa wilaya ya Singida, Dr. Titus Kamani waziri wa uvuvi na Mifugo, Dr. Parseko Kone Mkuu wa mkoa wa Singida, Ernest Mangu IGP na Jaji Chocha ( Picha na Doris Meghji)
Kaimu rasmi, Aziza,DC ALLY Amanzi,Titus kamani waziri wa Mifugo na uvuvi katika sherehe za kumsimika Askofu Edward Mapunda ( Picha na Doris Meghji)
Katikati ni DC wa Urambo Queen Mulozi, Hakimu Mfadiwidhi mkazi wa mkoa wa singida Mama Minde,Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya IKUNGI Celestine Iyunde ( Picha na Doris Meghji)
RPC Sodeyeka kushoto katikati nai Mbunge viti maalum  Christowaja Mtinda DC wa Meatu Erasto Sima katika kumsimka Mhashamu Askofu Edward Mapunda ( Picha na Doris Meghji)
Wa pili ni Mhashamu Akofu Edward Mapunda kabla ya kusimikwa rasmi utume huo wa kuwa kiongozi na mchungaji mkuu wa kanisa katoliki Jimbo la Singida( Picha na Doris Meghji)

Dr. Titus Kamani waziri wa uvuvi na Mifugo, Dr. Parseko Kone Mkuu wa mkoa wa Singida, Ernest Mangu IGP na Jaji Chocha ( Picha na Doris Meghji)
Askofu mkuu wa jimbo katolii la Tabora Paulo Ruzoka,katikati kushoto ni Askofu Desiderius Rwoma askofu wa jimbo katoliki la Bukoba na kulia ni Asofu mkuu Ngalekumtwa wa jimbo Iringa katika kuanza taratibu za kumsimika Askofu Mapunda ( Picha na Doris Meghji)
Askofu Edward Mapunda akipakwa mafuta baada ya kusaliwa litania ya watakatifu wote tayari kwa kusimikwa  rasmi daraja la uaskofu ( picha na Doris Meghji)
Askofu Edward Mapunda akiwekewa mikono ya Baraka na Maaskofu waliofika katika sherehe za kusimikwa kwake ( Picha na Doris Meghji)
Askofu Edward Mapunda  akijiandaa kulala kifudi fudi kwa ajili ya kusaliwa litania ya watakatifu wote kabla ya kusimikwa rasmi kuwa Kiongozi na mchungaji mwema wa Kanisa hili ( Picha na Doris Meghji)

Zawadi ya gari jipya aina ya Toyota Prado aliyokabidhiwa katika kusimikwa kwake (picha na Doris Meghji)

Monday, July 6, 2015

KODI YA MAJENGO KUSAIDI ONGEZKO LA MAPATO YA NDANI YA MANISPAA YA SINGIDA PINDI ITAPITISHA TOZO HILO,LA KODI IKIWA MOJA YA MATOKEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA ENDELEZAJI MIJI CHINI MFUKO WA BANKI YA DUNIA UTAKAOTEKELEZWA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO


Na, Doris Meghji Jumatatu Julai 06,2015

Singida – Manispaa

Mkutano wa pili wa uwasilishaji wa mpango wa jumla na uhabarisho wa uendelezaji wa mji wa singida (picha na Doris Meghji)

Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Singida Angelius Kamara akifafanua jambo katika mkutano huo mara baada ya kuwasilisha mada toka idara ya mipango miji akiwa ndio mkuu wa idara ya mapango miji ya manispaa a Singida katika ukumbi wa VETA (Picha na Doris Meghji)
Mkuu wa wilaya  ya Singida  Ally Amanzi amewaasa wenyeviti wa mitaa,na vijiji wa manispaa ya Singida  kutokuwa wabinafsi kwa kuelekeza maendeleo upande mmoja  tukwa kuwa mji huo umekuwa  na kuendelea upande mmoja hali ambayo itachelewesha  maendeleo kwa manispaa yote ya Singida.

Wajumbe na wadau wakiwa katika vikundi wakijadili moja ya mada zilizotolewa kujadili katika mkutano huo wa uwasilishaji wa mpango wa jumla na uhabarisho wa endendelezaje mji wa singida katika ukumbi wa VETA ( Picha na Doris Meghji)
Wosia huo umetolewa na mkuu huyo wa wilaya ya Singida Ally Amanzi wakati akifungua mkutano wa uwasilishaji wa mpango wa jumla (Master Plan) na uhabarisho wa miradi ya uendelezaji mji wa Singida (ULGSP) katika  ukumbi wa mikutano VETA ndani ya manispaa ya Singida

Wajumbe na wadau wakiwa katika vikundi wakijadili moja ya mada zilizotolewa kujadili katika mkutano huo wa uwasilishaji wa mpango wa jumla na uhabarisho wa endendelezaje mji wa singida katika ukumbi wa VETA ( Picha na Doris Meghji)
Aidha katika kusisitiza jambo hilo Mkuu wa wilaya huyo amewasisitiza wadau na wajumbe wa mkutano huo kuchangia vizuri katika mada zilizowasilishwa kwa kuwa fedha za uhabarisho huo ni mkopo toka banki ya dunia hivyo watumie hivyo fursa vizuri.

Baadhi ya wadau wakifuatailia na kumsiliza mkuu wa wilaya ya Singida katika ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa VETA ( Picha na Doris Meghji)

Ameitaja miradi ambayo itatekelezwa kupitia mpango wa uendeleazji mji ni ujenzi wa barabara ,kituo kikubwa cha mabasi,soko,vituo vidogo viwili vya mabasi machijio ya kisasa na uandaaji wa daftari la walipa kodi za majengo ambapo utekelezaji wake utagharimu jumla ya shilingi billion 16,901, 468, 788/= endapo manispaa hio itakizi vigezo kwa utekekelezaji wa miradi kwa kipindi cha miaka mitano mfululuzo toka Banki hio ya dunia.
Mohamed Kipamila Mtendaji wa kata ya Mtamaa manispaa ya Singida akiwasilisha moja ya mada zilizotolewa katika mkutano huo wa uwasilishaji wa mapago wa jmla na uhabarisho wa miradi a uendelezaji mji wa singida katika ukumbi wa VETA (Picha Doris Meghji)
Mkuu huo wa wilaya ameishauri pia manispaa hiyo kushirikisha wadau mbali mbali katika upimaji wa viwanja kwa kuitaka manispaa hiyo kukopa fedha toka banki ya uwekezaji (TIB) ili mji uweze kupimwa na kuondokana na makazi yasioyopimwa ( Squater)

Juliana Munishi mtendaji kata ya kindani manispaa ya Singida akiwasilisha mmoja ya mada katika mkutano wa uwashishaji wa mpango wa jumla na uhabarisho wa uendelezai miji wa Singida katika ukumbi wa VETA ( Picha na Doris Meghji)
Naye kaimu Mkurungezi wa manispaa ya Sigida Angelius Kamara ameeleza jinsi manispaa hiyo kupitia idara ya mipango miji suala la uthamini wa kodi za majengo na viwango vitakavyotozwa na manspaa ya singida katika kipindi hichi cha mwaka wa fedha ikiwa ni moja ya maandalizi ya utekelezaji wa miradi ya uendelezaji mji ambapo jumla ya majengo 16,577 yamefanyiwa uthamini katika manispaa hiyo

Mmoja ya washiriki akiwasilisha mada zilizojadiliwa katika vikundi kwenye mkutano wa uwasilishaji wa mpango wa jumla na uhabarisho wa uendelezaji wa mji wa singida katika ukumbi wa VETA (Picha na Doris Meghji)
Hii ikiwa ni moja ya utekelezaji wa uandaaji wa daftari la walipa kodi ya majengo utakaosaidi manispaa hiyo kuongeza  mapato ya ndani katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha
Hii ndio ndio ramani ya manispaa ya Singida iliyotolewa kuonyesha jinsi manispaa ya singida ilivyo katika mkutano huo ( Picha Doris Meghji)
 
Hii ni funguo ya maelezo ya ramani hapo juu inavyooyesha na kusoma katika ramani hiyoya manispaa ya Singida (picha Doris Meghji)
Katika uboreshwaji na undeleaji wa miji (ULGSP) lengo la kuu ni kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zilizo bora katika serikali za mitaa.
manispaa ya singida ni moja kati ya miji 18 inayotekeleza mradi huo ulioanza rasmi mwaka 2012 na kutarajiwa kukamilika 2018 
Wajumbe na wadau wakiwa katika vikundi wakijadili moja ya mada zilizotolewa kujadili katika mkutano huo wa uwasilishaji wa mpango wa jumla na uhabarisho wa endendelezaje mji wa singida katika ukumbi wa VETA ( Picha na Doris Meghji)
miji mingine ni Morogoro,Tabora,Moshi,Sumbawanga,Shinyanga,Songea Musoma Iringa,Njombe, Bukoba, Kibaha halmashuri ya mji,Babati, geita korogwa mpanda lindi na Bariadi.
Mwisho.

Monday, June 29, 2015

WAZIRI NYALANDU AWASILI SINGIDA - KUTAFUTA WAHDAMINI WA KUMDHAMINI KWA NAFASI YA URAIS - MKOANI SINGIDA



Ni ndege ndogo imewasiri katika kiwanja cha ndege cha mkoa wa Singida iliyokuwa imembeba  Mh. Waziri wa maliasili na Utalii  Lazaro Nyalandu mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM- kwa lengo la kutafuta wadhamini wa kudhamini katika kinyang’anyiro hicho.(Picha na Doris Meghji)


Wananchi wakimsubiri Mh.Lazaro Nyalandu katika viwanja vya Ndege mkoani  Singida (Picha na Doris Meghji) 

Mh. Lazaro Nyalandu akiwasalimia wananchi waliofika katika viwanja vya ndege vya mkoa wa Singida kwa kwa lengo la kudhaminiwa nafasi ya urais akiwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM (Picha Doris Meghji)

Mh. Lazaro Nyalandu akiwasalimia wananchi waliofika katika viwanja vya ndege vya mkoa wa Singida kwa kwa lengo la kudhaminiwa nafasi ya urais akiwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM (Picha Doris Meghji)

JANUARY MAKAMBA APATA WADHAMNINI 8300 WALIOMDHAMINI KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS KWA TIKETI YA CCM - MKOANI SINGIDA


Na, Doris Meghji Jumatatu Juni 29, 2015
Singida



Mh. January Makamba akiwasalimia wanachama wa CCM mkoa wa Singida wakati akipita mkoani hapo kutafuta wadhamini wa kudhamini kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM (Picha na Doris Meghji)
Watanzania wanataka mabadiliko wasipoyapata CCM watayapata nje ya CCM ni kauli ya Mwl Julias Kambarage Nyerere mwasisi wa CCM inaraudiwa tena na January Yusuf Makamba  mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM mkoani Singida

Katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini Madgalena Ndwete akimkabidhi Mh. Makamba fomu ya wadhamini waliodhamini katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)
Mh. Makamba (MB) mgombea wa nafasi ya urais amesema hayo wakati akitafuta wadhamini wanachama CCM kumdhamini kwa  nafasi hiyo ya urais kwa kuwataka wanaccm kumchagua yeye kijana katika kinyang’anyiro hicho pale atakapo chaguliwa kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi hiyo.
Mgombea nafasi ya urais Mh. January Makamba akinyanyua fomu ya udhamini mbele ya wanachama wa CCM waliofika kudhamini katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji)
Aidha amesema amejipima na kuona nafasi hiyo anaiweza vizuri. Katika kuelezea nia yake ya kugombea nafasi hiyo amesema “nchi  imekuwa na uongozi wa kizazi cha  kilichopita kwa miaka 50  kazi kubwa imefanyika ya maendeleo kwa miaka 50 iliyopita  na imefanya vizuri lakini sasa na miaka hamsini ijayo inahitaji viongozi wa kiazazi kipya,inahitaji uongozi wa kisasa na sio uongozi wa kisiasa uongozi wenye mtazamo mpya, fikra mpya na uongozi wa majawabu mapya ya changamoto zinazoikabili nchi yetu yeye ndio mwenye majawabu ya changamoto hizo alisistiza Mgombea Makamba.
Mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM akiwa pamoja na mkewe Bi Ramona Makamba kabla ya kuwashukuru wanachama wa CCM waliojitokeza katia zoezi la kudhamini mgombea Makamba (Picha na Doris Meghji)
Katika kurudia kauli ya  Mwl Julius Kambarage Nyerere alipohutubia mkutano mkuu mwaka 1995   Chimwaga mkoani Dodoma kwamba watanzania wanataka mabadilio wasipoyapota CCM watayatafuta nje ya CCM hadi sasa ni miaka 15 tangu Mwl atoe kauli hiyo na bado watanzania wanataka mabadiliko, 
Msafara wa Mh. Janaury Makamba ukiwasili katika viwanja vya ofisi ya CCM mkoa wa Singida katika zoezi la kutafuta wadhamnini wanachama wa ccm kumdhamini katika kinyang’a nyiro hicho cha urais mkoa wa Singida(Picha na Doris Meghji)
 vijana wanataka mabaliko na kila siku wanayasema na wanayadai  mabadiliko  wasipoyapata  ccm  watayatatufa nje ya ccm hivyo ccm inayonafasi ya kufanya madadiliko ni  kwa kumteua mgombea ambaye akisimama ataashiria mabadiliko na mgombea wa namna hiyo ni yeye alisisiza Mh. Makamba
Baadhi ya wakinamama wa chama cha mapinduzi waliojitokeza  kudhamini mgombea wa nafasi ya urais Mh. Makamba kwa tiketi ya CCM mkoani Singida ( Picha na Doris Meghji)
Katika zoezi hilo la kutafuta wadhamini jumla ya wadhamini 8300 wanachama wa ccm waliojitokeza kudhamini mgombea huyo ambapo wilaya ya singida mjini wadhamini 6500,Singida vijijini 600 huku wilaya ya mkalama wagombe 1200 na kufanya idadi hiyo ya wadhamini nje ya wadhamamini 45 wanaohitajika kwa mujibu wa taratibu za chama hicho.
MWISHO.

Ni Joram Alute mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Singida akiwa pamoja na viongozi wa dini  ndani ya viwanja vya ofisi ya CCM mkoa wa Singida wakimsubiri mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya ccm Mh. Janauary Makamba awasili maeneo ya viwanja hivyo(Picha na Doris Meghji)

Wanachama wa CCM wakimlaki Mh. Makamba mara alipowasili katika maeneo ya viwanja vya  ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)

Wanachama wa CCM mkoa wa Singida wakimsubiri mgombea wa nafasi ya urais Mh. January Makamba kuingia katika viwanja vya CCM tayari kwa leongo la kumdhamini na kumsikiliza mgombea huyo (Picha na Doris Meghji)

Kikundi cha sanaa cha Misake cha Manispaa ya Singida kikitoa burundani wakati wanaccm wakimsubiri mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM katika viwanja vya ofisi ya chama hicho mkoani Singida (Picha na Doris Meghji)

Wanachama wa CCM mkoa wa Singida wakimsubiri mgombea wa nafasi ya urais Mh. January Makamba kuingia katika viwanja vya CCM tayari kwa leongo la kumdhamini na kumsikiliza mgombea huyo (Picha na Doris Meghji)

Shekhe akifungua mkutano huo kwa dua kabla ya Mh. January Makamba mgombea wa nafasi ya urais wa CCM kuhutubia wanachama wa ccm waliofika eneo hilo kumdhamini kwenye nafasi hiyo ya urais (Picha na Doris Meghji)

Mchungaji akifungua pia kwa sala na kuomba uwepo wa Mwenyezi Mungu mkutano huo kabla Mh. January Makamba kuhutubia wanachama wa CCM waliojitokeza kudhamini katika nafasi hiyo ya urais (Picha na Doris Meghji)

Bi Ramona Makamba mke wa Mgombea urais kwa tiketi ya CCM akiwasalimia wanachama wa CCM waliofika kumdhamini mume wake ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)

Bi Ramona Makamba mke wa Mgombea urais kwa tiketi ya CCM akiwasalimia wanachama wa CCM waliofika kumdhamini mume wake ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)

Mzee Salehe Msule mzee maarufu mkoani singida na Joraum Alute wakimnadi mh. Makamba mbele ya wanaccm walofika kudhamini na kumsikiliza mgombea makamba katika viwanja vya ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha Doris Meghji)

Jorum Alute mwenyeiti Mstaafu akimsemea neno Mh. Makamba mbele ya wanaccm  mkoa wa Singida waliofika kudhamini mgombea huyo kwa nafasi ya urais wa CCM ( Picha na Doris Meghji)

Saturday, June 27, 2015

MH. MIZENGO PETER PINDA AMEWAASA WANACCM KUTOBAGUANA KWA MISINGI YA HUYU WA FULANI NA HUYU WA FULANI KATIKA LA KUFATUTA WADHAMINI - MKOANI SINGIDA




Na, Doris Meghji Jumaosi Juni 27,2015
Singida


Mh.Mizengo Peter Pinda akiwachekesha wanachama  wa  CCM mkoa wa Singida wakati akitoa shukrani kwa wadhamini waliomdhamini kwenye kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM (Picha na Doris Meghji)
Mh. Mizengo Peter Pinda amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuepuka kishawiwshi cha kubaguana kwa msingi wa huyu ni fulani na huyu ni wa fulani kwa kuwa  kishawishi hicho haina tija kwa wanachama hao.
Mh. Mizengo Peter Pinda (MB)  ambaye ni waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  akiwasalimia baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM mara alipowasili kwenye viwanja vya ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)

Kauli hiyo ameitoa juzi majira ya saa sita adhuhuri katika viwanja vya ccm mkoa wa Singida kwenye zoezi la kuwatafuta wadhamini wa kumdhamini kwenye kinyang’anyiro cha uombea wa nafasi ya urais  wa chama hicho.
Mh. Mizengo Peter Pinda (MB) waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Katibu wa UWT mkoa wa Singida Angela Milembe mara alipowasili katika viwanja vya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)
Aidha amewataka wanachama wa chama hicho kutobaguana kwa misingi ya  huyu ni wa fualani na huyu wa fualani “mimi nita mwendea tu hata kama yeye ni wa fualni kwangu mimi naamini wote ni wanaccm tu” alizitiza Mh. Pinda 

Mh. Mizengo Peter Pinda (MB)  ambaye ni waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  akiwasalimia baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM mara alipowasili kwenye viwanja vya ofisi ya CCM mkoa wa Singida (Picha na Doris Meghji)
Hivyo katika kuwatafuta wadhamini wa kudhamini kugombea nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM jumla ya wadhamini 45 wamejitokeza kumdhamini katika nafasi hiyo mkoa wa Singida 

Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi  waliojitokeza kudhamini na kumsikiliza Mh. Mizengo Peter Pinda katika kinyanganiro cha urais (Picha na Doris Meghji)
Mh. Pinda amewashukru wanachama waliojitokeza kudhamini akisema kama ccm itamuona anafaa na kutaka apeperushe bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25  mwaka huu  atashukuru na kazi yake itakuwa ni kuitekeleza ilani ya chama hicho ambayo ndio muongozo mkuu.
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi  waliojitokeza kudhamini na kumsikiliza Mh. Mizengo Peter Pinda katika kinyanganiro cha urais (Picha na Doris Meghji)

Mh. Mizengo Peter Pinda ni mmoja kati ya watia nia 39 ya wagombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM.