Na, Doris Meghji Jumatatu Julai 06,2015
Singida – Manispaa
Mkutano wa pili wa uwasilishaji wa
mpango wa jumla na uhabarisho wa uendelezaji wa mji wa singida (picha na Doris
Meghji) |
Mkuu wa wilaya ya Singida Ally Amanzi amewaasa wenyeviti wa mitaa,na
vijiji wa manispaa ya Singida kutokuwa
wabinafsi kwa kuelekeza maendeleo upande mmoja tukwa kuwa mji huo umekuwa na kuendelea upande mmoja hali ambayo
itachelewesha maendeleo kwa manispaa
yote ya Singida.
Wosia huo umetolewa na mkuu huyo wa
wilaya ya Singida Ally Amanzi wakati akifungua mkutano wa uwasilishaji wa
mpango wa jumla (Master Plan) na uhabarisho wa miradi ya uendelezaji mji wa
Singida (ULGSP) katika ukumbi wa
mikutano VETA ndani ya manispaa ya Singida
Aidha katika kusisitiza jambo hilo Mkuu
wa wilaya huyo amewasisitiza wadau na wajumbe wa mkutano huo kuchangia vizuri
katika mada zilizowasilishwa kwa kuwa fedha za uhabarisho huo ni mkopo toka
banki ya dunia hivyo watumie hivyo fursa vizuri.
Baadhi ya wadau wakifuatailia na
kumsiliza mkuu wa wilaya ya Singida katika ufunguzi wa mkutano huo katika
ukumbi wa VETA ( Picha na Doris Meghji) |
Ameitaja miradi ambayo itatekelezwa
kupitia mpango wa uendeleazji mji ni ujenzi wa barabara ,kituo kikubwa cha
mabasi,soko,vituo vidogo viwili vya mabasi machijio ya kisasa na uandaaji wa
daftari la walipa kodi za majengo ambapo utekelezaji wake utagharimu jumla ya
shilingi billion 16,901, 468, 788/= endapo manispaa hio itakizi vigezo kwa
utekekelezaji wa miradi kwa kipindi cha miaka mitano mfululuzo toka Banki hio
ya dunia.
Mkuu huo wa wilaya ameishauri pia
manispaa hiyo kushirikisha wadau mbali mbali katika upimaji wa viwanja kwa
kuitaka manispaa hiyo kukopa fedha toka banki ya uwekezaji (TIB) ili mji uweze
kupimwa na kuondokana na makazi yasioyopimwa ( Squater)
Naye kaimu Mkurungezi wa manispaa ya
Sigida Angelius Kamara ameeleza jinsi manispaa hiyo kupitia idara ya mipango
miji suala la uthamini wa kodi za majengo na viwango vitakavyotozwa na manspaa
ya singida katika kipindi hichi cha mwaka wa fedha ikiwa ni moja ya maandalizi
ya utekelezaji wa miradi ya uendelezaji mji ambapo jumla ya majengo 16,577
yamefanyiwa uthamini katika manispaa hiyo
Hii ikiwa ni moja ya utekelezaji wa
uandaaji wa daftari la walipa kodi ya majengo utakaosaidi manispaa hiyo
kuongeza mapato ya ndani katika kipindi
hiki cha mwaka wa fedha
Hii ndio ndio ramani ya manispaa ya
Singida iliyotolewa kuonyesha jinsi manispaa ya singida ilivyo katika mkutano
huo ( Picha Doris Meghji) |
Hii ni funguo ya maelezo ya ramani hapo juu inavyooyesha na kusoma katika ramani hiyoya manispaa ya Singida (picha Doris Meghji) |
Katika uboreshwaji na undeleaji wa miji
(ULGSP) lengo la kuu ni kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zilizo bora
katika serikali za mitaa.
manispaa ya singida ni moja kati ya miji 18 inayotekeleza mradi huo ulioanza rasmi mwaka 2012 na kutarajiwa kukamilika 2018
miji mingine ni Morogoro,Tabora,Moshi,Sumbawanga,Shinyanga,Songea Musoma Iringa,Njombe, Bukoba, Kibaha halmashuri ya mji,Babati, geita korogwa mpanda lindi na Bariadi.
Mwisho.
|
No comments:
Post a Comment