Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Saturday, January 31, 2015

CCM KUANZIMISHA MIAKA 38 TANGU KUZALIWA KWAKE






HABARI KATIKA PICHA LEO KATIKA MADHIMISHO YA KUZALIWA CCM 


Kijana mmoja akipewa kadi ya chama cha mapinduzi leo katika viwanja va peoples akipewa na Mbunge wake Mohamed Dewji (picha na Doris Meghji)


Mohamed Dewji  akimkabidhi mmoja wa wanacnhi wa manispaa ya Singida(Picha na Doris Meghji)

Baadhi ya wananchi  waliofika katika viwanja va peoples kumsiliza mbunge wao Mohamed Dewji (picha na Doris Meghji)

Baadhi a wanachama wapya wakiapa katika viwanja va peoles mara baada a kukabidhiwa kadi cha uanachama wa ccm na jumuhia zake (picha na Doris Meghji)

MIAKA 38 A KUZALIWA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI- WILAYA SINGIDA MJINI


HABARI KATIKA PICHA  ZA SIKU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 38 YA KUZALIWA KWA CCM- WILAYA YA SINGIDA MJINI LEO JANUARI 31,2015



Mh. Mbunge Mohamed Dewji akihutubia wananchi na wakazi wa manispaa ya singida leo katika viwanja vya peoples kwenye maadhimisho ya sikuku za kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi wilaya ya Singida Mjini(picha na Doris Meghji)
Mohamed Dewji akihutubia wananchi na wakazi wa manispaa ya singida leo (picha na Doris Meghji)

Baadhi a wananchi ya wananchi wakimsikiliza mbunge wao katika maadhimisho ya sherehe za mia 38 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi manispaa ya Singida (picha na Doris Meghji)

Mbunge wa viti Maalum Mh. Diana Chilolo akiongea na Meya wa manispaa ya singida leo katika viwanja va peoples ndani a Manispaa ya singida(Picha na Doris Meghji)
Mheshimiwa Mohamed Dewji akihutuhia wananchi wa manispaa ya singida akiwa ameumia mguu wa kushoko katika viwanja vya manispaa ya Singida (picha na Doris Meghji)

BARAZA LA MADIWANI LA MAISPAAA SINGIDA LAPITISHA OMBI MAALUM LA ZAIDI A BILIONI 3 KATIKA BAJETI YAKE YA MWAKA 2015/2016



Na, Doris Meghji  Jumamosi Januari 31,2015
Singida – Manispaa
Mchumi Nurfus Azizi Ndee  wa Manispaa ya Singida akiwakilisha ombi maalum la bajeti katika baraza la madiniwani liliofanyika katika ukumbi wa Mabula Standi kanisa la katoliki manispaa ya Singida( picha na Doris Meghji)

Zaidi ya shlingi bilioni tatu zinahitajika katika halmashauri ya manispaa ya singida ikiwa ni ombi maalum la bajeti ya manispaa katika kuzikabiri changamoto mbali mbali  zinazoikumba manispaa hiyo kwa sasa.
Madiwani wa manispaa wakimsikiliza Mkurugenzi wa manispaa ya Singida (picha na Doris Meghji)

Akiwasilisha ombi hilo maalum kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa  mbele ya kikao cha  baraza la madiniwani wa manispaa ya singida Mchumi wa manispaa hiyo  Nurfus Ndee amesema ombi hilo limekuja kwenye bajeti hiyo kutokakana na changamoto mbali mbali zinazikabili manispaa ya Singida zikiwemo changamoto za kuongezeka kwa uhitaji wa huduama za kijamii ,uhitaji wa uboreshaji wa wa miundo mbinu mbali mbali zikiwemo barabara, masoko na kuongezeka shughuli za kiutawala kwa manispaa hiyo

Baadhi ya madiwani wa manispaa ya singida wakimsikiliza mchumi wa manispaa ya singida wakati akiwakilisha ombi hilo maalum kwenye kikao cha baraza la manispaa ya Singida(picha na Doris Meghji)


Aidha ametaja jumla ya shilingi billion 3,059 821,150/= zinahitajika kwa ajili ya kuzikabili changamoto hizo  ambapo shilingi bilioni 2,700,000 zitatumika katika ujenzi wa jengo jipya la  utawala la halmashauri ya manispaa ya singida na shilingi milioni 359 821 150,000/= ni kwa ajili ya ukamilishaji wa mabaoma ya shule za msingi ndani ya manispaa hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Shekhe Mahami akiongea neno katika baraza la madiwani wa manispaa ya Singida katika kikao cha baraza la bajeti la manispaa hiyo( picha na Doris meghji)

Hata hivyo dira ya manispaa ya singida inaonyesha kuwa ifikapo mwaka 2015 itakuwa manispaa yenye kutoa huduma bora kwa wananchi wa manispaa hiyo.


Mwisho.

Friday, January 30, 2015

MANISPAA YA SINGIDA YATARAJIA KUTUMIA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 32 KATIKA KIPINDI CHA MWAKA WA FEDHA 2015/ 2016

Na, Doris Meghji   Ijumaa Januari 30,2015
Singida – Manispaa

Kushoto ni Mkurugenzi wa manispaa a Singida Joseph Mchina,Katikati ni Mstahiki Meya wa manispaa ya Singida  Shekhe Mahame kulia ni  Naibu meya wa manispaa hii (picha na Doris Meghji)


Zaidi ya shilingi bilioni 32.25 zinatarajia kutumika katika halmashauri ya manispaa ya singida ikiwa ni makisio ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2015- 2016 mkoani singida
Mchumi wa manispaa ya Singida  Nurfus Azizi Ndee  akiwakilisha makisio ya mpango na bajeti ya mwaka 2015-2016 katika baraza la madiwani( picha na Doris meghji)

Akisoma  kwa niaba ya mkurugenzi wa manspaa ya Singida makisio ya mpango na bajeti ya mwaka fedha 2015/2016 mbele ya kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Singida  mchumi wa Manispaa hiyo Nurfus Azizi Ndee amesema jumla ya shilingi bilioni thelathini na mbili, milioni mia mbili hamsini na saba,laki tatu sabini na nne  elfu  mia nne sabini na mbili zinatarajiwa kutumika katika kipindi hicho cha mwaka wa fedha.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida akifungua kikao cha baraza la madiniwani katika kupitisha makisiao na mpango wa bajeti ya manispaa hiyo 2015- 2016 (Picha na Doris Meghji)

Aidha ametaja jumla ya shilingi 20,883,349,248/= kwa ajili ya mishahara ya na matumizi mengine ya manispaa hiyo,shilingi  bilioni 1,780,450,000 zikiwa ni fedha za matumizi ya kawaida, fedha za rukuzu ya  miradi ya maendeleo toka serikali kuu  ni shilingi bilioni 6,403,326,223.62/= huku shilingi bilioni 2,986,364,000/= ni mapato ya ndani ya manispaa ya singida katika kipindi hicho cha mwaka wa fedha.
baadhi ya madiwani wa manispaa ya singida wakisikiliza taarifa ya makisio ya bajeti ya manispaa yao (picha na Doris Meghji)
Kwa mujibu wa mchumi Ndee amezitaja changamoto mbali mbali zinazoikabili manispaa hio kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa uhitaji wa huduma za kijamii,uhitaji wa maafisa ugani,uhitaji na uboreshaji wa miundombinu mbali mbali  hasa za barabara,masoko na shughuli za kuitawala hii ni kutokana na changamoto ya ukuaji haraka wa manispaa ya Singida.
Mh. Yagi Kiaratu diwani wa viti maalum ccm akiunga mkono makisio ya mpango na bajeti ya manispaa hiyo kwa niaba ya madiwani wa manispaa ya singida (picha na Doris Meghji0

Mwisho




Tuesday, January 27, 2015

TUME YA RAMANI NA MADINI DUNIANI YAMTEUA PROF SOSPETER MUHONGO KUWA MTENDAJI MKUU WA TUME HIYO




Breaking News: Siku Mbili Baada ya Prof. Muhongo Kujiuzulu Tume ya Ramani na Madini Duniani Yamteua Kuwa Mtendaji Mkuu wa Tume Hiyo



Siku Mbili tu. Baada ya profesa Sospeter Muhongo kujihuzuru nafasi ya waziri wa nishati na madini hii JanaTume ya Ramani na Madini Miamba na Mawe Duniani yenye makao makuu nchini Uingereza imemteua profesa Muhongo kuwa mtendaji mkuu wa tume hiyo pia atafanya kazi kwenye kampuni inayopasua miamba diniani kama mwenyekiti.

~Source: William Malecela Blog

Saturday, January 24, 2015

RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AWAAPISHA RASMI MAWAZIRI NANE NA MANAIBU WAZIRI WATANO LEO JIJINI DAR- ES- SALAAM

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Awaabisha leo Jijini Dar-es salaam  jumla ya mawaziri nane wa baraza la mawaziri  na manaibu waziri watano kushika nafasi hizo katika wizara hizo.

Kuapishwa kwa mawaziri hao na manaibu waziri  ni baada ya  kujiuzulu kwa mawaziri wawili  wa wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi  Prof.Anna Kajumulo Tibaijuka na pamoja na wizara ya Nishati na madini  Prof. Sosepeter Muhongo kufuatia sakata la Akaunti ya Tegeta Eskro
Mabadiliko ya baraza hilo la Mawaziri limetangazwa leo na Katibu mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar-es- salaam.

Na mawaziri walioteuliwa na kuapishwa leo kuwa ni

1.    George Simbachawene – Waziri wa Nishati na Madini
2.    Mary Nagu – Waziri wa Nchi mawasiliano na uratibu
3.    Christopher Chiza Waziri uwezeshaji na uwekezaji
4.    Harrison Mwakembe – Ushirikiano wa Afrika Mashariki
5.    William Lukuvu – waziri ya Ardhi numba na maendeleo ya Makazi
6.    Steven Wassira – Waziri wa Kilimo chakula na ushirika
7.    Samwel Sitta -  Waziri wa Uchukuzi
8.    Jenista Muhagama – Sera na uratibu wa Bunge


Huku manaibu waziri walioteuliwa na kuapishwa leo kuwa ni
1.    Stephen Masele – Naibu waziri ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira
2.    Anjela – Jasmini Kairuki Naibu waziri wa Ardhi
3.    Ummy Ally Mwalimu – Naibu waziri Katiba na Sheria
4.    Anna Kilango Malecela – Naibu waziri wa Elimu
5.    Charles Mwijage – Naibu waziri wa Nishati na Madini.

Kati ya manaibu hao manaibu waziri wapya ni
Anna Kilango Malecela – Wa elimu
 na
Charles Mwijage wa Nishati na Madini.
Mwisho.


BREAKING NEWS - MINISTER OF ENERGY AND MINERALS RESIGNED TODAY IN DAR- ES - SALAAM


BREAKING NEWS
ESCROW SAGA: The Minister for Energy and Minerals, Prof Sospeter Muhongo resigns this morning in Dar es Salaam following Escrow saga.

More details! Don’t miss to;
 Watch NEWS ON 

 TBC1, STARTV, ITV, CHANNEL 10, CAPITAL TV and listen to TBC TAIFA, RADIO ONE, RADIO FREE AFRICA