Na, Doris Meghji Jumatano Novemba
20,2013
Singida
Manispaa ya singida imeendelea kuwataka
wafanyabiashara wa nyama katika mabucha 32 nyama yalioko soko kuu singida
kutekeleza amri ya manispaa hiyo kwa
kuhakiksha wanafanya usafi wa mabucha yao ikiwa ni pamoja na kupima afya zao katika
kutoa huduma hiyo ndani ya manispaa
Singida
Baadhi ya Mabucha ya soko kuu la Singida yakiwa yamefungwa |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Joseph Mchina amesema hayo alipotembelewa na karibu
Singida Blog kutaka kupata maelezo ya kufunga mabucha hayo 32 ya soko kuu la manispaa ya singida kwa kipindi
cha wiki mbili sasa
Joseph Mchina Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida - akiwa Ofisini kwake akiongea na karibusingida.blog |
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mchina amesema
wamefunga mabucha hayo kutokana hali ya uchafu wa mazingira uliokithiri kwenye mabucha hayo alisema “manispaa
ilitoa siku 7 kwa wafanyabiashara hao
wanyama wafanye usafi katika mabucha yao kwa kuweka maru maru (Tiles) kwenye
sakafu na kuta za bucha zao,dirisha la kioo, kupata rangi,kuvaa sare nyeupe na
kupima afya zao kwa wafanyabiashara hiyo ya nyama kwenye soko hilo baada ya
siku saba kuisha na wao kukaidi amri na agizo la manispaa ikabidi tufunge
mabucha ” kwa kuokoa afya za walaji na wakazi wa manispaa alisisitiza
Mkurugenzi Mchina
Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Ndg.Joseph Mchina akiwa ofisini kwake |
“Baada ya kufunga sasa ndio unaona
malalamiko sisi tunachokitaka ni wao kufuata tulichoagiza atakayeweza kufanya
hivyo nitatuma wataalam wangu wakakague na wakiridhika anaruhusiwa kuchinga na
kuuza nyama kwenye mabucha hayo”alisema Mkurugenzi Mchina
mabucha - soko kuu singida yakiwa yamefungwa na kutoa huduma |
Aidha kwa upande wa watumiaji wa
kitowewo hicho ikiwa pamoja na wajasiliamali wanaouza chakula (Mama ntilie) katika
maeneo mbali mbali ya manispaa hiyo amesema
kuna mabucha mnne ambayo wameyakaguliwa mitaani ndio yanayotoa huduma
hiyo ya kuuza nyama kwa wakazi wa manispaa yake kwa sasa na kuwa ongezoko la
uchinjaji wa ng’ombe umeongezeka ukilinganisha na kipindi cha nyuma kabla ya
mabucha kufungwa
Mkurugenzi huyo amewataka wafanyabiashara
hao kuzingatia kanuni na taratibu za usafi wa mazingira na kanununi za usafi wa
vyakula kwa kuvaa sare kupima afya zao na kujikinga magonjwa ya kuambukiza kwa biashara hiyo katika manispaa yake ikiwa
ni pamoja na kulipa ushuru wa manispaa
baadhi ya wamiliki wa mabucha soko kuu manispaa ya Singida |
Awali wakitoa malalamiko yao baadhi ya
wafanyabiashara akiwemo bwana Zuberi
Haji mfanyabiasha wa nyama katika kibanda namba 1 amesema kufungiwa mabucha
kumewaathiri kwa kiasi kubukwa kwa kuwa yeye huuza ngombe wawaili kwa siku
hivyo ameomba kuruhusiwa kufanyabiashara kwa kuwa yeye amekwisha karabati bucha
lake.
Zuberi Haji mmiliki wa Bucha namba 1 soko kuu Singida |
Wakati huo huo bwana Omary Ghambuna
miliki wa mabucha mawili katika soko hilo amesema yeye ameathirika sana hasa
katika suala la kipato kwa kufungwa mabucha hayo, kwakuwa kipato chake
kinategemea shuhuli hiyo ya uuzaji wa nyama
Omary Ghambuna kulia akiwa na wenzake katika mabucha ya soko kuu Singida |
Hata hivyo wameomba manispaa iwaruhusu
watu waliokwisha karabati vibanda vyao na kufuata mashariti ,kuendelea na
biashara kuliko kusubiri vibando vyote vikarabatiwe na kufanyiwa usafi kwa kuwa
sio wote wenye uwezo wa kufanya hivyo
akionyesha jinsi alivyokarabati bucha lake Zuberi Haji soko kuu manispaa ya Singida |
Kwa upande wa manispaa kukosa mapato wafanyabiashara
hao wamesema manispaa itakosa mapato kwa kuwa wao hulipa shilingi 10,000/= ya ushuru
wa manisapaa kwa mwezi na uwepo wao urahisha wakazi na wajasiliamli kama akina
mama ntilie kuendesha biashara zao kwa kutumia kitoweo cha nyama kama suala la mtori,ndizi hutegemea kitoweo
hicho ambacho ni bei rahis ukilinganisha na samaki, kwa kuwa bei ya kilo moja
ya nyama ni shilling 5000/= huku bei ya kilo moja ya samaki ni shilingi 8000/=
Omary Ghambuna na wenzake akielezea juu ya suala hilo la kufungiwa mabucha na manispaa |
Wiki mbili sasa tangu mabucha hayo 32
kufungwa, mabucha yamefungwa rasmi Novemba 8 mwaka huu kwa uchafu uliokithiri kwa kuwataka wamiliki
wa mabucha hayo kufanya usafi ikiwa ni pamoja na kukarabati vibanda hivyo kwa
kuzingatia kanununi na taratibu za usafi wa mazingira na kanuni za afya ya vyakula
ndani ya manispaa ya Singida.
Bucha namba 1 ukarabati wa kuweka vyoo katika bucha hilo |