BRASS BAND YA JKT- MAKUTUPORA IKONGOZA MAANDAMANO YA MAHAFARI 11 TIA SINGIDA |
Na, Doris Meghji Ijumaa Novemba 15,2013
Singida
Taasisi ya uhasibu kampasi ya singida
inatarajia kukosa zaidi ya shilling milioni
200,470/= ya mapato kwa kushindwa kudahili wanachuo wengi mwaka huu kutokana na
uhaba wa miundombinu katika kampasi hiyo
ulinganisha na mwaka wa masomo 2012 -2013.
mgeni rasmi katikati Dr. Parseko Kone mkuu wa mkoa wa Singida kulia ni Prof,Faustine Kamuzora mwakilishi wa mwenyekiti wa Bodi ya TIA kulia ni meneja wa tawi la uhasibi Singida Emmanuel Kingu |
Hayo yamebainishwa rasmi na kaimu afisa
mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Ndugu Shah Hanzuruni kwenye
mahafali ya 11 ya kampasi ya Singida yaliofanyika No
Novemba 08 mwaka huu
baadhi ya wahitimu wa TIA mwaka huu |
Kwa mujibu
wa kaimu Afisa mtendaji mkuu huyo ameeleza kuwa katika kipindi cha mwaka wa masomo cha 2012 – 2013 kampasi ya singida
ilikusanya jumla ya shilingi bilioni 2,847,525,000/= ambalo lilikuwa ongezeko
la asilimia 76.23 % liliotokana na ongezeko la wanachuo waliodahiliwa pamoja na
vyanzo vingine vya fedha
wahitimu wa TIA - kwenye mahafari 11 - singida |
Aidha kwa
mwaka huu wa masomo 2013-2014 kampasi ya uhasibu ya singida inatarajia
kukusanya shilingi billion 2,645,050,000/= sababu za upungufu huo ni kkutokana
nakushiindwa kudahili wanachuo wengi na uhaba wa miundombinu katika kampasi ya
singida
Katika kutaja
baadhi ya changamoto zinazoikabili kampasi ya singida ni pamoja idadi ndogo ya wanachuo kutoka mkoa wa singida
wanaojiunga na taasisi hiyo ukilinganisha na mikoa jirani hivyo ameomba
seriakli na mamalaka zake zishrikiane na taasisi hiyo kuhamasisha wananchi na
wakazi wa mkoa wa singida kutumia fursa ya kuwepo kwa taasisi hiyo mkoani hapak,aidha
,suala la upatikanaji wa maji ni tatizo kubwa katika taaisisi hiyo hivyo
ameomba mamlaka ya maji (SUWASA) kuwapatia maji masaa 24 au kuiruhusu kununua
mojawapo ya visima vyake vilivyopo ndani ya eneo la taasisi kwa matumizi ya chuo,kutokuwa na hati miliki
ya chuo ni moja ya changamoto ya kitaasisi ikiwa ni taasisi ya kiserikali hivyo
ameomba serikali ya mkoa wa singida kusaidiwa kupatiwa hati hiyo toka manispaa
Naomi Kapambala katibu wa CCM mkoa wa Singida na wageni waalikwa siku hiyo ya mahafari |
Hata hivyo uhaba wa majengo ya ofisi,madarasa,nyumba za
wahadhiri ,kumbi za mihadhara, samani ,makataba ya kiasasa mighahawa na ofisi
za wafanyakazi
Brass Band toka JKT makutu pora ikisherehesha mahafali 11 - mwaka huu ya TIA |
Naye Mgeni
rasimi katika mahafali hayo ya 11 Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone
katika kujibu baadhi ya changamoto hizo ameitaka mamlaka ya maji safi na maji
taka singida mjini (SUWASA) kuona uwezkanao wakutoa kipaumbele kwa taasisi kama
hiyo ipatiwe maji kwa muda mwingi zaidi kwa kuwa taasisi hizo huwa na mksanyiko
mwingi wa watu na hivyo uhaba wa maji katika taasisi hiyo uweza kuleta mlipuko
wa magonjwa akisisitiza katika suala hilo Mkuu wa mkoa huyo ameagiza jumatatu
novemba 11 mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka singida mjini SUWASA na mkuu wa chuo cha uhasibu kukutana
ofisini kwake kuzungunzia suala hilo.
Dr. Parseko Kone katika mahafali ya 11 chuo cha uhasibu tawi la singida |
huku suala la kupatiwa hati miliki na
kupanua eneo la chuo ameagiza mkurugenzi wa manispaa ya singida na mkuu wa chuo
tawi la singida kukatana ofisini kwake waone tatizo nini mpaka leo tawi hilo
kutopatiwa hati miliki
mwl. Queen Mulozi DC Singida na Prof Faustine Kamuzora katika mahafali ya 11 ya TIA - singida |
ata hivyo
mkuu wa mkoa wa singida ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa singida
kuchangamkia fursa ya kuwepo kwa chuo hico katika kujikwamua kiuchimi kwa kuwa
serikali kupitia sera ya public,private partnership(PPP) kujenga hosteli kwa
ajili ya kuwapangisha wanafunzi kwa kushrikina na taasisi hiyo ya uhasibu “wito
kwenu wnasingida sasa ni wakati wenu aerikalina watu binafsi walewenye maeneo
mjenge hosteli kwa ajili ya wanachuo “alisisitiza Dr. Kone
Dr. Parseko Kone Mgeni rasmi akitoa hobuta yake kwenye mahafali ya 11- TIA singida |
Kwa upande
wake mkuu wa mkoa wa Singida amewaasa wanafunzi kujiendeleza kielemu kwa kuwa
serikali ya Tanzania imeweka mazingira mazuri ya kujiendeleza kielimu hata
wakiwa makazini kwa kwa kupitia chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
mmoja kati ya wahitimu akipokea zawadi toka kwa mgeni rasmi katika mahafali hayo. |
Jumla ya
wahitumu 2,415 wa tawi la singida na Mwanza kati ya hao wahitimu 1258 ni
wanaume na wanawake 1,157 katika kozi mbali mbali za cheti cha
msingi,stashahadana stashahada ya uzamili.
No comments:
Post a Comment