Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Tuesday, November 5, 2013

MABANGO YA BIASHARA KUINGIZIA PATO LA NDANI MANISPAA YA SINGIDAA



Na, Doris Meghji Jumanne Novemba 05, 2013
Singida

manispaa ya Singida

Halmashauri  ya manispaa ya Singida inatarjiwa kuongeza mapato kwa kutumia vyanzo mbali mbali vya ndani ya mapato ya manispaa hiyo kwa kupitisha bei za biashara za mabango ya matangazo mbali mbali katika manispaa hiyo kwa kuongeza mapato ya ndani ili kuleta ufanisi katika kuongeza kasi ya kuiletea maendeleo halmashuri ya manispaa ya Singida




Akiwasilisha kwenye baraza la madiwani Mkurugenzi wa manispaa hiyo bwana Joseph Mchina ametaja  bei za ushuru mbali mbali zikiwemo za ushuru wa matangazo ya biashara na leseni mbali mbali za biashara kwenye kikao hicho kilichofanyika oktoba 31 katika ukumbi wa RC mission
mmoja ya aina ya mabango ya matangazo  ya biashara manispaa ya singida

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo ametaja ushuru wa matangazo ya biashara utangazaji wa biashara za ndani  kuwa ni shilingi 100,000/= kwa kila tangazo na matangazo ya biashara za nje dola za kimarekani 100 kwa kila tangazo huku ada ya mabango mbali mbali ya matangazo kwa matangazo au alama yoyote ya tangazo iltakalo tangazwa katika kuta paa na mbao za nyumba au jengo lolote kutozwa shilingi 3000/= kwa futi moja ya mraba kwa mwaka huku mabango ya biashara na huduma yasiyowaka taa na mabango ya matangazo ya biashra yanayowaka taa kutoza shilingi 10,000/= kwa futi moja ya mraba kwa mwaka 
                                              

                                                  

Hata hivyo kabla ya kuridhia bei za ushuru juu ya mabango ya matangazo ya biashara Mh. Diwani wa kata ya Ipembe Hassan Kihara amemtaka mkurugenzi kutoongeza kwango cha bei ya ushuru wa mabango ya matangozo ya biashara kutoka 3000/= hadi kufikia 8500 kama alikvyoiwasilisha katika kikao hicho akiilinganisha na hali ya uchumi wa wananchi wa manispaa hiyo na kubaki 3000/= kwa futi mmoja ya mraba kwa matangazo ya biashara.

  katika kuta,paaa mbao za nyumba au jengo lolote ,nao mh. Hadija Simba diwani wa viti Maalum na Moses Ikaku  diwani wa kata ya Unyamikumbi walimkata mkurugenzi kusimamia vizuri chanzo hicho cha mapato kuwa kinaweza kuwa moja ya chanzo kizuri cha mapato ya ndani ya manispaa ya singida kwa hakikisha hayo mabango ya matangazo ya mitandao ya kampuni za simu zinalipa ushuru huo.



Kupitisha bei hizo za mabango ya biashara kunapata baraka kupitia marakebishao ya sheria ya ada ya ushuru yanayolenga kurekebisha viwango  vya ada na ushuru mbalimbali kwa kuongeza vyanzo vya mapato ya ndani, kupitia kifungu cha 89 cha sheria ya serikali za mitaa(mamlaka za miji) sura ya 288 toleo la 2002 na kifungu cha 16(1) cha sheria ya fedha za serikali za mitaa sura ya 290 toleo 2002 vinavyotoa mamlaka kwa halmashauri kuweza kutunga,kurekebisha pamoja na kuweka na kurekebisha viwango vya ada na ushuru katika eneo lake la utawala.




 

No comments:

Post a Comment