Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Tuesday, November 5, 2013

WANNE WASIMAMISHWA KAZI MANISPAA YA SINGIDA

Na, Doris Meghji Jumanne Novemba 05,2013
Singida

Jumla ya watumishi wanne(4)  wa manispaa ya singida wamesimamishwa kazi kutokana tuhuma mbali mbali zinazowakabili ikiwemo ya uuzaji  viwanja (double allocation)  katika manispaa ya singida



Akitoa azimio hilo mara baada ya kukaa kama mkamati kwa baraza la  madinwani wa manispaa ya Singida Oktoba 31 mwaka huu katika ukumbi wa RC Mission, Naibu Meya wa manispaa ya Singida Mh. Hassan Mkata amesema watumishi wanne wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbali mbali zinazowakabili ili wapishe uchungu ufanyike juu ya tuhuma hizo.




Kwa mujibu wa naibu Meya huyo amewataja watumishi hao kuwa ni Afisa ardhi daraja la pili wa manispaa hii bwana Richard Makupe kwa tuhuma za kugawa viwaja mara mbili mbili (double allocation),Bwana Jafari Dule afisa mtendaji wa kijiji cha Unyambwa kata ya Unyambwa manispaa ya Singida kwa kukutwa na vitabu viwili vya risiti vya bandia, Bi Teckla Mwiko mkusanya ushuru wa soko la ukombozi kwa tuhuma za kukuwa na vitabu vya risiti viwili  hali inayokosesha mapato manispaa hiyo na Jumanne Ng’imba afisa mtendaji wa kata ya Kindai kwa tuhuma ya kutotimiza majukumu yake kama afisa mtendaji wa kata hiyo.


Akifunga kikao hicho cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo Naibu Meya Mh. Hassan Mkata awataka kila mmoja awajibike katika nafasi yake na kutofanya kazi kwa mazoea, wafanye kazi kama mikataba ya kazi inavyowaelekeza.

mwisho


No comments:

Post a Comment