Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Thursday, November 7, 2013

MJUMBE WA NEC - ASISITIZA WANANCHI KUJIUNGA KATIKA VIKUNDI VYA WAJASILIAMALI

MNEC  - Singida mjini  Hassan Mazala akisalimiana na wanachama wa ccm kata ya Mtamaa
Na, Doris Meghji Alhamis  Novemba 07,2013
Singida

Mjumbe wa halmashuri kuu ya  (CCM) taifa wilaya Singida mjini Hassan Mazala  ametawaka wanachama  wa chama hicho kujiunga kwenye vikundi vya ujasiliamali ili chama kiweze kuwasaidia kwa urahisi wakiwa kwenye vikundi  kuinua maisha yao kiuchumi.
Hassan Mazala - Mjumbe wa NEC akisikiliza wananchi na wanachama wa ccm kata ya Mtamaa
Mjumbe huyo wa NEC Hassan Mazala  amewataka  wanachama wa chama hicho jana wakati akifanya ziara za kuzindua matawi mapya ya chama cha mapinduzi na kusikiliza kero za wanachama wa chama hicho katika kata ya Mtamaa manispaa ya singida
MNEC wa singida mjini - akizindua mmoja ya tawi jipya la ccm kata ya Mtamaa 
Aidha amewakata wanchama hao kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali ili ikiwa ni moja ya njia ya wanachama hao kusaidika kiuchumi na sio mtu mmoja moja
Hata hivyo ziara hiyo ilifanywa kwa lengo la kuzindua matawi mapya ya chama cha mapinduzi,kusikiliza kero za wanachama ikiwa ni moja ya wajibu wa mjumbe wa halmashauri ya CCM taifa wilaya ya Singida mjini
MNEC - akicheza ngoma ya asili  ya kinyaturu
Jumla ya matawi manne mapya yalizundiliwa na mjumbe huyo wa NEC wilaya ya Singida mjini ambayo ni Mbuyuni, wajasiliamali Mtamaa “A ”,kikundi cha wauza matunda Mtamaa “B” na shina la wakereketwa Mtisi
MNEC - akihutubia wananchi na wanachama wa kata ya Mtamaa





No comments:

Post a Comment