Hon.Kassimu Majaliwa Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI - Elimu |
Na, Doris Meghji Jumanne Novemba 19,2013
Singida
Tanzania imejiwekea malengo kuwa ifikapo 2015 asilimia 45 za kaya za miji na asilimia 35 za kaya za vijiji zitumie vyoo bora
kutokana hali isiyoridhisha ya matumizi vya vyoo bora ilivyo sasa kwa takwimu
kuonyesha asilimia 22 tu za kaya mijini
na aslimia 9 za kaya za vijiji ndizo zenye vyoo bora, kwa kupitia awamu ya pili ya mpango wa kukuza na
kupunguza umaskini (MKUKUTA II) nchini
Liana Hassan RAS - singida akimpa maelezo naibu Waziri Kassimu Majaliwa mara baada ya kuingia katika Viwanja vya Peoples - Manispaa ya Singida |
Akifungua maadhimisho ya kitaifa ya siku
ya kunawa mikono duniani,siku ya matumizi ya choo duniani na wiki ya usafi wa
mazingira Mheshimiwa Kassimu Majaliwa
(MB) Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu
tawala za mikoa na serikali za mitaa – Elimu amebainisha hayo Novemba 16 mwaka huu mkoani singida katika viwanja
vya Peoples manispaa ya Singida
Njia mbali mbali za kunawa mikono katika maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani yaliofanyika mkoani Singida Kitaaifa. |
Kwa mujibu wa naibu waziri huyo amesema
serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii,wizara ya maji wizara ya
elimu na mafunzao ya ufundi na wadau wa maendeleo inafanya jitihada mbali mbali
ili kuhakikisha kwa nchi inafikia malengo hayo mojawapo ya jitihada hizo ni
kuadhimisha siku ya kunawa mikono,siku ya matumizi ya choo,na wiki ya usafi wa
mazingira.
Kassimu Majaliwa (MB) Naibu waziri Elimu _ Tamisemi akipata maelezo toka kwa mmoja wa watu toka wizarani katika banda la maonyesho la wizara ya Afya na ustawi wa jamii |
Mjomba Band ikitumbuiza katika maadhimisho hayo ya kunawa mikono na matumizi ya choo bora duniani mkoani Singida |
Washiriki katika mabanda ya maonesho |
Add caption |
Mhe.Kassimu Majaliwa(MB) Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMSEMI(Elimu) akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Mwl.Queen Mlozi |
Awali akitoa maelezo katibu mkuu wa
wizara ya Afya na ustawi wa jamii ndugu Charles Amos Pallangyo katika uzinduzi huo
amesema hali vyoo nchini sio ya kuridhisha ni asilimia 12 kaya pekee ndizo
zenye vyoo bora,suala la kunawa mikono katika nyakati muhimu yaani baada ya
kutoka chooni,kabla ya kula,baada ya kumsafisha mtoto aliyejisaidia na kabla ya
kuandaa chakula, bado lipo chini sana ikiwa ni mara ya saba kuadhimisha siku ya
matumizi ya choo,na mara nne siku siku ya kunawa mikono duniani katika kipindi hiki mwamko kwa jamii
umeongezeka na viongozi kushiriki katika usafi wa mazingira
Charles Amos Palangyo Katibu Mkuu wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akitoa maelezo ya siku ya kunawa duniani
Kasimu Majaliwa Naibu Waziri Elimu Tamisemi katikati Mwl Queen Mulozi DC Singida
hivyo katika kuleta chachu ya ushindani
kwenye suala la usafi wa maznira wizara ya afya kwa kushirikianana ofisi ya
mganga mkuu mkoa wa singida imeendesha zoezi la kushindanisha taasisi na kaya
ilikupata washindi wa usafi katika ngazi hizo washindi watapewa zawadi na cheti
na vifaa vya usafi siku ya kilele cha
maadhimisho hayo Novemba 19,2013 mkoani Singida
Mwl. Queen Mulozi Mkuu wa wilaya ya Singida akitoa salamu za mkoa katika maadhimisho hayo
Kikundi cha sanaa cha Mbalamwezi kikitumbuiza kwenye maandhimisho hayo katika viwanja vya PEOPLES
Msafara wa sabuni ukipita katika viwanja hivyo kuhamasisha wananchi kutumia sabuni katika unawaji wa mikono
Jumla ya wadau wamaendeleo tisa (9)
wameshriki kitika kufanikisha maadhimisho hayo ambao ni UNICEF,WSP GIZ, WSSCC,
Water Aid,SAWA, Colgate,Palmolive, BTC na
BIDCO
mmoja ya maonyesho ya aina ya mabomba yakutiririsha maji katika maeneo ya mkusanyiko wa watu katika kujikinga na magonjwa ya mlipuko kwa kunawa mikono kwa maji na sabuni
Spinderman akiwa kwenye msafara wa sabuni kuhimiza unawaji wa mikono na sabuni ikiwa ni mmoja ya kapeni ya mazingira
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni
“Usafi
ni Ustaraabu, Tumia choo Bora nawa mikono kwa sabuni Okoa maisha ya Watoto.’’
mwanafunzi na watoto mmoja ya walengo wa kampeni sa usafi mashuleni
|
No comments:
Post a Comment