ujumbe wa mbio za marathoni( Picha na Doris Meghji) |
Na, Doris Meghji Jumatatu Novemba
11,2013
Singida
Nchi ya Tanzania inaweza kupoteza zaidi
ya aslimia 17 ya mapato kutoka sekta ya
utalii nchini kutokana na ujangili wa wa tendo na upunguaji wa wanayapori unaofanyika nchini imefahamika
Kijana Patik Patel mmilki wa kampuni la
AFRICAN WILDLIFE TRUST ambaye ni mdhanini wa mashindano hayo ya marathoni kwa
kushirikina na Mbunge wa jimbo la Singida kaskazini ambaye ni Naibu waziri wa Maliasili na utalii ametoa
tahadhari hiyo mkoani Singida wakati akitoa maelezo ya kuendesha mashindano ya
mbio za nusu marathoni mkoani Singida
baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakiwa tayari kwa kuanza mbio hizo ( Picha na Doris Meghji) |
Kwa mujibu wa Kijana Patik Patel
amesema jumla ya tembo 30 kati ya tembo
10,000 uwawa kwa mwaka na asilimia 50 ya wanyamapori wanapungua kwenye hifadhi
nchini wakati sekta ya utalii uchangia asilimia 17 ya pato la taifa
Patik Patel akiongea na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Singida ( Picha na Doris Meghji) |
Aidha amesema watalii wengi nchini huja
kutalii katika mbuga zetu za wanyamapori hivyo kupungua kwa wanayama na kuwawa
tembo hao kutapoteza pato hilo kwa kukosa wa watalii kutembelea mbunga hizo.
baadhi ya wasichana walioshiriki katika mashindano ya mbio hizo za nusu marathoni ( Picha na Doris Meghji) |
Washiriki 400 wameshiriki katika mbio hizo za marathoni
yaliyofanyika Jumamosi Novemba 9 mwaka huu ambapo mshindi wa kwanza alipata zawadi ya shilingi 300,000/= mshindi wa pili alipata shilingi 200,000/= na mshindi wa tatu katika mbio za kilomita 21 alipata 100,000/=
Mmoja wa washiriki wa shindano hilo ( Picha na Doris Meghji) |
kwa upande wa mbio za kilomita 5 mshindi wa kwanza alipata 200,000/= mshindi wa pili 100,000/= na mshindi wa tatu 50,000/= wakati kwa upande wa mbio za kilomita 2.5 shindi wa kwanza alipata 100,000/= mshindi wa pili 50,000/= na mshindi wa tatu 25,000/=
mshindi wa nusu marathoni Paulo Itambu akiwa na madiwani wa viti maalum mara baada ya kumaliza mbio hizo kwa kutumia saa 1:10:22 ( Picha na Doris Meghji) |
washiriki wengine walipewa shilingi10,000/ kwa kushiriki mashindano hayo
mbio hizo zilianzia kijiji cha Mitula kata
ya Kinyangigi na kumalizikia katika kijiji cha Ntunduu kata ya Kinyeto mkoani
Singida
Fabiola Willum John mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake katika mbio hizo za nusu marathoni mkoani Singida (Picha Doris Meghji) |
Hii ni starting Point ( Picha na Doris Meghji_ |
Hata hivyo mkoa wa singida
una hifadhi ya misitu mbali mbali ikiwemo misitu ya Mgori, Minyughe na Rungwa
mkoani hapa
Mwisho
Mwisho
No comments:
Post a Comment