Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Thursday, November 7, 2013

UWEZO NA TATHIMINI YA KKK TATU KWA WATOTO WENYE UMRI WA MIAKA 7 HADI 16

Na, Doris Meghji Alhamisi Novemba 07,2013
Singida
Ikiwa  tatizo la watoto kutojua kusoma kuandika na kuhesabu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini Tanzania,zoezi la kupima uwezo wa watoto katika kujifunza limekwenda vizuri ndani ya manispaa ya singida ambapo  maeneo ya kuhesabia (EA) 30 yamefanyiwa tathimini hiyo mkoani Singida
Bi Zuhura Karia Mratibu wa UWEZO wa Mansipaa ya Singida
Hayo yamebainishwa leo  na mratibu wa UWEZO manispaa ya Singida Bi Zuhura Karia ambaye ni afisa ustawi wa jamii mkoa wa Singida
Valantia wa zoezi hilo la sensa ya tathimini ya UWEZO

Bi Karia amesema zoezi katika kufanya zoezi hilo jumla ya maeneo 30 yalifanyiwa utafiti wa kupima uwezo wa mtoto katika kujifunza ambapo kila eneo moja la kuheasabiwa linakuwa na kaya 20 na 5 za ziada
Bi Zuhura Karia akiwa ofisini 
Bi Karia amesema zoezi katika kufanya zoezi hilo jumla ya maeneo 30 yalifanyiwa utafiti wa kupima uwezo wa mtoto katika kujifunza ambapo kila eneo moja la kuheasabiwa linakuwa na kaya 20 na 5 za ziada


Aidha amesema katika utekelezaji wa zoezi hilo upimaji wa uwezo wa mtoto katika kujifunza, wenyeviti wa mitaa,vijiji,wakuu wa shule za msingi wazazi na watoto wenye umri kati miaka 7 hadi 16 walihusishwa katika dodoso hilo


mmoja ya kipimo cha kujua kusoma  lugha ya kiswahili
Kwa mujibu wa Mratibu Karia amesema katika kujaza dodoso suala la kumpima uwezo wa mtoto katika kujifunza wameandaa Aya za kiswahili,na kiingereza, Aya kubwa na ndogo,silabi na maneo ya kusoma ili kujua uwezo

wa mtoto katika kujua kuisoma lugha ya kiswahili,kiingereza na kuhesabu namba.

Katika upimaji huo wa uwezo wa mtoto katika kujifunza silabasi ya darasa la pili ndio iliyotumika katika kumpima mtoto

mmoja ya kipimo cha kujifunzia  kuhesabu


Hata hivyo zoezi hilo limefayika kwa muda wa siku mbili (2) jumla ya valantia 60 walifanikisha zoezi hilo kwa hisani ya UWEZO  manispaa ya Singida ambapo valantia 2 walifanyakazi katika eneo la kuhesabia mmoja.(EA 1)
Valantia wa UWEZO waakipatiwa mafunzo ya kuifanya sensa manispaa ya Singida

MWISHO




No comments:

Post a Comment