Na, Doris Meghji Jumatatu Agosti 31,2015
Singida
Umuhimu wa kutumia bidhaa zenye alama ya ubora uliothibitishwa na shirika la viwango la taifa (TBS) utasaidia zaidi wajasiliamali na wazalishaji
wa bidhaa kuhakikisha wanauza bidhaa zao zenye alama ya ubora uliothibitshwa na
shirika hilo.
Afisa masoko mwandamizi toka shirika la viwango la taifa (TBS) Gladness Kaseka akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda la maonyesho la TBS kwenye maonyesho ya SIDO kanda ya kati yaliohusisha wajasiriamali wadogo na wakatii mkoani Singida kwenye viwanja vya peoples ( Picha na Doris Meghji) |
Imeelezwa
kuwa iwapo wananchi au watumiaji wa
bidhaa wataelewa na kutambua umuhimu wa
kutumia bidhaa zenye alama ya ubora uliothibitishwa na TBS kutasaidiwa wajasiliamali wadogo na wakati kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za shirika la
viwango nchini kwa kuhakisha bidhaa zao wamezisajili na kupewa alama ya bora
toka shirika hilo.
Beatrice Mmbaga mjasiriamali wa usindnikaji wa dagaa toka mkoani Mara Musoma akiongea na karibusingida.blogspot.com kwenye maonyesho ya SIDO kanda ya kati mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na
Doris Meghji) |
Bi Gladness Kaseka afisa masoko mwandamizi wa
shirika la viwango la Taifa ( TBS) ametoa wito huo kwa wananchi na watumuaji wa
bidhaa wa mkoa wa singida na taifa kwa
ujumla kutumia fursa hiyo ya kupata
elimu kwenye Maonyesho ya SIDO banda la TBS
viwanja vya peoples ili kuelewa umuhimu wa kutumia bidhaa hizo katika kuwasaidia
wajasilimali hao kuuza bidhaa zenye alama ya ubora uliotibitisha na TBS nchini.
Ni baadhi ya wajasiriamali wakimpokea
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho
hayo ya SIDO kanda ya kati mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na
Doris Meghji) |
“hapa elimu zaidi ni kwa watumiaji wa
bidhaa hawa wakielewa watakuwa wanauliza mbona hii bidhaa aina alama ya ubora? na
soko la bidhaa zisozokuwa na alama hiyo ya TBS haitauzika sokoni, hii
itawafanya wajasiliamali kuhakikisha wanauza bidhaa zao zenye alama ya ubora
uliothibitisha na TBS kwa sasa wanazalisha
na kuuza wakijua soko lipo atauuza tu.”alisema
Bi Gladness Kaseka Afisa masoko huyo wa TBS.
Katika maonyesho hayo shirika hilo la
viwango linatoa elemu juu ya utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS.
Dkt. Parseko Kone Mkuu wa mkoa wa Singida mgeni rasmi katika ufunguzi wa maeonyesho ya SIDO kanda ya kati akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la SIDO mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na
Doris Meghji) |
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo limetoa
maelezo juu serikali hutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali
wadogo na wakati pale wanapoomba bidhaa zao wanazozizalisha zithibitishwe ubora,
kuwa kati yao wapo wanaosamehewa kulipa ada yoyote kwa sababu ya mitaji kuwa
midogo hivyo ili kupata msamahaa huo mjasiliamali anatakiwa kupata barua ya
uthibitisho toka ofisi ya SIDO iliyokaribu na chama cha wazalishaji kama vile
TAFODA ikiwa ni pamoja na taarifa fupi
toka idara ya Afya iliyopo karibu na mahali pa uzalishaji au cheti cha mamlaka ya taifa ya chakula na dawa (TFDA) kwa wazalishaji wa vyakula ikiwa ni pamoja na
leseni ya biashara.
Beatrice Mmbaga Mjasiriamali mdogo wa kusindika dagaa toka mkoa wa mara Musoma akitoa maelezo yake juu ya changamoto ya kupata alama za uthibitisho wa ubora wa bidhaa toka TBS na vifungashio toka SIDO kunako mgarimu mlaji wa bidhaa zao kwa kuwa bei inakuwa kubwa kutokana na gharama hizo ( Picha na Doris Meghji) |
Nao baadhi ya wajasiriamali walioshiriki katika
maonyesho hayo mjasiriamali Beatrice Mmbaga kutoka Musoma msindikaji wa dagaa ameeleza
changamoto ya wao kuhusu jengo hasa katika suala la kupata alama hizo za ubora toka TBS ni mpaka kibali toka TFDA, hivyo ameimba SIDO iweze
kuwapatia majengo au vyumba kwa ajili ya
wajasiriali hao kuwa na maeneo ya kuzalishia na kusindika bidhaa zao lengo la
kuwawezesha wajasiriamali hao kupata alama hizo za ubora toka TBS ili waeze
kukubalika katika soko la ndani na nje ya nchi.
Bwana Henrick Mdede meneja masoko wa SIDO makao mkuu ya SIDO taifa akiongelea suala la changamoto za wajasiriamali kuhusu usogezwaji wa huduma karibu na wajasiriamali ikiwa ni pamoja na vifungashio kwenye maonyesho ya SIDO kanda ya kati mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na
Doris Meghji)
|
Katika kulitolea maelezo suala hilo la
wajasiriamali Meneja Masoko toka SIDO makao makuu Henrick L. Mdede amekiri wajasiriamali kuwa na
changamoto nyingi hasa suala kusogeza huduma kwenye maeneo yao kwa kushirikiana
na halmashauri za wilaya nchini kwa
ajili ya kujenga kongano mbali mbali za uzalishaji kwa wadogo huko wilayani
amesema wilaya nyingi zimeweza kutoa
maeneo mbali mbali,
Ni baadhi ya wajasiriamali walioshiriki kwenye maonyesho hayo wakati wa wakimsubiri mgeni rasmi kuhutubia kwenye uzinduzi rasmi wa maonyesho
hayo ya SIDO kanda ya kati mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na
Doris Meghji) |
suala la ufinyu wa
bajeti limeokena kuwa ni moja ya changamoto kubwa hasa ufinyi wa bajeti ya serikali kwa shirika hilo la kuhudumia
viwanda vidogo vidogo (SIDO) kupitia
wizara ya viwanda na biashara kuhusu
suala fedha ya kulipia upimaji wa ardhi kwenye viwanja au maeneo, kulipa fidia
kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kongano za uzalishaji wa bidhaa kwa wajasiliamali
wagodo wanaozalisha bidhaa hizo imekuwa ni tatizo katika utatuzi wa changamoto
hiyo nchini.
Ni mjasiriamali Bi Beatrice Mmbaga toka Musoma Msindikaji wa dagaa akiongea na karibu Singida Blogspot kwenye maonyesho hayo ya SIDO kanda ya kati akielezea juu ya changamotozo zinazowakabili juu ya suala la vifungashio vya bidhaa zao hasa katika kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi ndani viwanja vya Peoples leo ( Picha na
Doris Meghji) |
Huku suala la vifungashio ameiomba
serikali kuwavutia wawekezaji wengi kuwekeza kwenye viwanda kwa kufufua viwanda
na kuanzisha viwanda vipya nchini ili kulitatua tatizo hilo ambalo kwa sasa
vifungashio huagizwa nje ya nchi hali ambayo umuumiza mlaji na mtumiaji wa
bidhaa hizo nchini.
Ni baadhi ya wajasiriamali wakimpokea
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone wakati wa uzinduzi rasmi wa maonyesho
hayo ya SIDO kanda ya kati mkoani Singida kwenye viwanja vya Peoples ( Picha na
Doris Meghji) |
Maonyesho hayo ya SIDO kanda ya kati
ambayo wajasiriamali 205 wamefanikiwa kushiriki toka mikoa kumi (10) kati mikoa
hio ni mkoa wa Dodoma, Kigoma,Singida,Shinyanga na Tabora ndio mikoa inayounda
SIDO kanda ya kati nchini.
MWISHO.