Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Monday, August 17, 2015

UCHAGUZI WA MWAKA HUU SIO KAMA UCHAGUZI WA MWAKA 2010 WANACCM MKOA WA SINGIDA WAASWA KUTOBWETEKA - NAOMI KAPAMBALA

Na, Doris Meghji Jumatatu Agosti 17,2015
Singida
Wanachama wa CCM mkoa na baadhi ya viongozi wakati wa sherehe za kumuaga Katibu Naomi kapambala ukumbi wa Rafiki Resort manispaa ya Singida 
Viongozi na wanachama wa chama cha Mapinduzi wameaswa kutolala kwa kuwa uchaguzi wa mwaka huu sio uchaguzi wa kawaida hivyo wametakiwa kufanya kampeni kwa hali na mali ili CCM ishinde kwenye uchaguzi mkuu huo Oktoba 25 mwaka huu.
Huyu ni Mussa Sima Mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la singida mjini aliyeteuliwa na chama hicho mara baada ya utata mwingi kugubigwa matokeo ya uchaguzi huo jimbo la singida mjini akiwa na Bi Yagi Kiaratu Mgombea pekee mwanamke wa nafasi ya udiwani kata ya majengo manispaa yas ingida  akiwa kwenye hafla ya kumuaga aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa singida na Kuhamishiwa mkoani Kigoma ( picha na Doris Meghji)
Kauli hiyo imetolewa na Naomi Kapambala katibu wa CCM mkoa wa Kigoma wakati wa sherehe za kuagwa na wanaccm mkoa wa Singida alipokuwa akifanya kazi kabla ya kuhamia mkoani Kigoma
“upinzani uliopita miaka 10 sio upinzani wa leo hivyo tusibweteke watendaji tuendelee kuwa na ushirikiano kwa kuwa uchaguzi wa miaka hii kushinda  ni kwa kijipanga na kufanya kazi bila kulala” kapambala aliwaasa wanaccm hao
Huyo ni Martha malata akisalimia na kutoa neno kwa wanachama na kumshukru Katibu Kapamabala kwa uongozi wake pindi alpokuwa mkoani Singida kwenye ukumbi wa Rafii Resort katika sherherhe ya kumuaga  iliyoandaliwa na wanachama na viongozi wa chama hicho mkoani Singida ( Picha na Doris Meghji)
Katika kusisitiza jambo hilo amewataka wabunge na madiwani viti maalum kufanyakazi na kuhakikisha ushindi kwa chama hicho kwa kuwa ushindi wa chama hicho katika majimbo na kata ndio itawapa fursa ya wao kuwa wabunge na madiwani nchini.
Wanachama wa CCM mkoa na baadhi ya viongozi wakati wa sherehe za kumuaga Katibu Naomi kapambala ukumbi wa Rafiki Resort manispaa ya Singida.

“Wale watakaofanya kazi vizuri na kuhakikisha CCM inashinda ndio watakaoteuliwa kwa nafasi hizo za udiwani na ubunge mkoani hapo”
Ni mgombea Magareth Malecela,akifuatiwa na Rehema Shilla wagombea wa viti maalum kushoto na mgombea Valelian Kimambo mgombea udiwani Kata ya Muhanga kulia ni Angela Milembe mgombea udiwani viti maalum akiwa na mgombea ubunge jimbo la Singida mjini Mussa Sima  kwenye hafla ya kumuaga katibu Naomi Kapambalaa kumbi wa Rafiki Resort manispaa ya Singida. ( Picha na Doris Meghji)
Katibu Kapambala amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho wae macho na makundi ya urais hasa kwa kushawishiwa kupigia mbunge wa CCM, diwani wa CCM ila kwa nafasi ya urais kupigia upinzani.
Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Bi Naomi Kapambala alikuwa akiagwa juzi katika ukumbi wa Rafiki Resort ndani ya manispaa ya Singida ( Picha na Doris Meghji)

 amewataka wasifanye hivyo kwa kuwa kauli mbiu ya chama hicho ni mafiga matatu ya kuwachagua wagombea wa nafasi ya udiwani, ubunge, na urais wote kuwa wa chama cha Mapinduzi.
Huyo ni Mary Maziku Katibu wa CCM mkoa wa Singida aliyehamia mkoani hapa kutoka makao makuu a chama cha Mapinduzi na kushika nafasi ya Mary Chatanda ambaye ni mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la korogwa mjini ( Picha na Doris Meghji)
Naye katibu Mary Maziku katibu wa CCM mkoa wa Singida anayekaribishwa mkoani humo ameomba ushirikiano miongoni mwa Viongozi wa ngazi zote za wilaya na mkoa ikiwa ni pamoja na wanchama wa chama hicho mkoani humo  kufanya kazi ili kuhakikisha chama cha mapinduzi kinashinda kwa kishindo na kuhakikisha hawapotezi jimbo hata moja kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu
Huyo ni Martha malata akisalimia na kutoa neno kwa wanachama na kumshukru Katibu Kapamabala kwa uongozi wake pindi alpokuwa mkoani Singida kwenye ukumbi wa Rafii Resort katika sherherhe ya kumuaga  iliyoandaliwa na wanachama na viongozi wa chama hicho mkoani Singida ( Picha na Doris Meghji)
 Hata hivyo katika hafla hiyo ya kumuaga Katibu huyo walimtangaza Mgombea Mussa Ramdhani Sima kuwa ndio mgombea aliyeteuliwa kuipeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu jimbo la Singida mjini
Huyu ni Mussa Sima Mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la singida mjini aliyeteuliwa na chama hicho mara baada ya utata mwingi kugubigwa matokeo ya uchaguzi huo jimboni  akiwa kwenye hafla ya kumuaga aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa singida na Kuhamishiwa mkoani Kigoma ( picha na Doris Meghji)
Kutangazwa kwake kumekuja mara baada ya mizengwe ya matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni wa CCM uliofanya na katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini  kwa kubandika matokeo hayo Agosti 02,  majira saa tatu usiku mwaka huu matokeo ambayo yalimuonyesha  mgombea Hassani Philipo Mazala akiongoza kwenye matokeo hayo hali iliyoleta sintofahamu miongoni wa mgombea Musa Sima  na wanachama wa chama hicho wilaya ya Singida mjini.
Hao ni wanachama na viongozi akiwemo Martha Mlata Mbunge mteule wa CCM viti maalum mkoa wa Singida wakiselebuka kwenya hafla ya kumuaga Naomi Kapambala aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Singida na Kuhamia Mkoani Kigoma ( picha na Doris Meghji)
katibu Kapambala alikitumikia chama hicho kwa kipindi cha miaka saba toka 2007 hadi 2014 mkoani singida  ndipo alipohamishwa kwenda mkoani kigoma.
Huyo ni Margaret Malecela diwani wa viti maalum mteule kwa ccm kwa manispaa ya Singida na Mwl Lilian Mrua kada wa chama cha mapinduzi katika sherehe a kumuaga Katibu wa CCM mkoa wa Singida Bi Naomi Kapambala na kuhamia Kigoma kwenye ukumbi wa Rafiki Resort ndani ya manispaa ya Singida ( Picha na Doris Meghji)
 Mkoa wa singida unajumla ya majimbo 8 ya uchaguzi ambayo ni jimbo la  Ikungi Mashariki, Ikungi Magharibi,Manyoni Mashariki,Manyoni Magharibi ikiwa ni pamoja na Jimbo la Singida Kaskazini,jimbo la Iramba,Mkalama na Singida mjini.
Huyo ni Martha Mlata na Aisharose Matembe wabunge wateule wa Viti maalum toka mkoa wa Singida baada ya kushinda kwenye kinag'aniro cha ubunge kupitia CCM toka UWT picha na Doris Meghji)
huku wateueliwa wa ubunge viti Maalum ni Aisharose Matembe na Martha Mlata kupitia chama cha Mapinduzi toka UWT.
Mwisho.





1 comment:

  1. uchaguzi mwaka huu ni wa CCM dhidi ya CCM kazi ipo. same techniques.Tunachoomba tu ni Amani miongoni mwa watanzania.

    ReplyDelete