Na, Doris Meghji Jumatatu Agosti 17 2015
Singida
Padre Vicant Alute Mlezi wa chama cha Lejio Maria Jimbo katoliki la singida akihubiri kwenye misa takatifu ya kupalizwa mama Bikira maria mbinguni ( Picha na Doris Meghji) |
Waumini wa kanisa katoliki jimbo la
Singida wameombwa kuendelea kumuomba mama Birkia Maria ili nchi yao ibakie katika amani hasa katika kipindi hiki
cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais
wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Kuaswa kwa waumini hao kumefanyika jana na Padre Vincent Alute mlezi wa Lejio Maria kanisa katoliki jimbo la Singida katika maadhimisho
ya Misa Takatifu ya Kupalizwa Mbinguni kwa Mama Bikira Maria katika kanisa la
Moyo Mtakatifu wa Yesu.
Ni wanalejio Maria wa Kanisa katoliki jimbo la Singida kwenye sherehe za kupalizwa Mama bikira Maria Mbinguni ( Picha na Doris Meghji) |
Padre Alute amewataka waumini hao kumshika
mkono mama bikira Maria awaombee kwa Mwanae ili nchi yao ibaki katika Amani kwa
kuwa wao hawakushudia vita hivyo amewataka wasijibweteke waumini hao wakasahau kushika mkono Mama Bikira Maria
awafundishe na kuelekeza namna ya kupendana na kumpenda mwanae Yesu Kristu.
Kwaya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ikiimba kataika misa tafakifu ya kupalizwa mbinguni kwa mama bikira Maria jimbo katoliki la Singida ( Picha na Doris Meghjii) |
Katika kulisistiza jambo hilo Mlezi
Alute amewataka waumini hao kusali kweli, kuwa makini na kuwa na msimao thabiti kama ilivyokuwa
mama Bikira Maria mtu mwenye imani kwa Mungu ,wamuamini Mungu wasije wakabweteka wakayubishwa na
kusahau ukweli mama Bikira Maria alikuwa anapenda watu na majirani kwa kuwajali
na kuwathamini
Kwaya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ikiimba kataika misa tafakifu ya kupalizwa mbinguni kwa mama bikira Maria jimbo katoliki la Singida ( Picha na Doris Meghjii) |
Hivyo amewataka wasiviombe vita kwa kuwa
vita havina macho kwa kuwataka waendelee kuiombea nchi yao amani katika kipindi
hiki cha uchaguzi mkuu kwa msaada wa mama kanisa mama Bikira Maria
Ni wanalejio Maria wa Kanisa katoliki jimbo la Singida kwenye sherehe za kupalizwa Mama bikira Maria Mbinguni ( Picha na Doris Meghji) |
Katika kuadhimisha sherehe hizo jumla ya
wanachama wapya 117 wa chama cha Lejio Maria wamejiunga na kufikia idadi ya wanalejio 900
jimboni Singida.
Ni wanalejio Maria na watumikizi wa Kanisa katoliki jimbo la Singida kwenye sherehe za kupalizwa Mama bikira Maria Mbinguni ( Picha na Doris Meghji) |
Mwisho.
No comments:
Post a Comment