Na, Doris Meghji Jumatano Agosti 12,
2015
Singida
Wiki ya nenda kwa usalama bara barani yazinduliwa
rasmi jana mkoani singida ikiwa na kauli mbiu ya Endesha salama okoa maisha kwa kuwasii wananchi na watumiaji wa barabara mkoa wa Singida kujitokeza kwa wingi
kutembela maonyesho mbali mbali yatakayoendeshwa katika wiki hilo lengo ni
kuwapatia elimu ya sheria za barabarani kwa
wananchi wa mkoa wa Singida
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa SACP Tobias Sodeyeka amewataka
wanachi hao kufika na kutembelea maonyesho hayo ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ili
waweze kupata elimu itakayoweza kuwasaidia kujua sheria za barabarani kwa wananchi wa mkoa wa Singida na wajibu wa kila mtumia barabara hizo.
Kamanda huyo ametolea maelezo juu ya
ajali za pikipiki zilizoweza kutokea na kupoteza maisha ya wananchi wa mkoa huo, katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu ni vifo 18 na majeruhi 8
vimetokea kwa kuwataka wananchi hao kufika katika maonyesho hayo ili kupata elimu ya sheria za usalama barabarani kwa kuwa waendesha piki piki ndio wanaongoza kwa ajali na
kusababisha vifo mkoani hapo.
Kwa hiyo amewashauri waendesha pikipiki ni vema wafike
hapo na kupata elimu
“We mwendesha piki piki usalama wako kwanza ,ni mambo gani yanasababisha kutokea kwa ajali hasa piki piki? kwanza hatuvai helmet,upakiaji kwa njia ya hatari, unapakia watu wanne na kile kiti cha pikipiki ni kidogo na ninafahamu matatizo Sunlag huwezi kukata kona kwa haraka na kitu kingine ni kupatikia mizigo, unapakia watu huku umebeba mizigo na wakati mwingine ni huwa umelewa asubuhi tu umekwisha kunywa viroba hii ina hatarisha maisha yetu pindi ajali ikitokea ni vyema mje hapa mkapata elimu.” amewashauri wananchi hao kufika katika maonyesha hayo kamanda Sodeyeka.

Hata hivyo katika maonyesho hayo kupitia
kitendo cha usalama barabarani wa jeshi
hilo la polisi afisa G233 PC Phaston
alitolea maelezo juu ya kifaa cha kisasa
cha upimaji wa mwendo kasi ulevi wa
madereva wa magari yakiwa barabarani chenye uwezo wa kupiga picha ya
dereva,gari kwa ujumla na namba ya gari na mwendo kasi kwenye uzinduzi huo
Aidha katika kulezea kifaa hicho kwa
jina la Dragon EYE amesema jeshi la polisi lina jumla ya vifaa hivyo vya kisasa
18 kwa mkoa huo lengo likiwa ni kuondoa utata uliokuwepo wa madereva kukataa
mwendo wa gari lake na kudai kuwa amesingiziwa kwa kuwa kifaa hicho kinauwezo wa
kupima gari liliko umbali wa kilomita moja na mita mia nane. Ameeleza PC Phaston.
Maashimisho hayo ya wiki ya nenda kwa usalama
barabarani yamezinduliwa rasmi na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
mkoani Tanga na ufungaji wa maadhimisho
hayo ni Agosti 18 mwaka huu
No comments:
Post a Comment