Advertssssss

Advertssssss

Menu drop

Wednesday, August 5, 2015

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII LAZARO NYALANDU ASHINDA KWA KISHINDO KATIKA UCHAGUZI WA KURA ZA MAONI NDANI YA CCM JIMBO LA SINGIDA KASKAZINI


 Na, Doris Meghji Jumatano  Agosti 05,2015
Singida
Katibu wa CCM wilaya ya Singida Vijijini Mwanamvua Killo akisoma matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni ya ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Singida kaskazini mbele ya waandishi wa habari (Picha na Doris Meghji)
Matokeo jimbo la Singida kaskazini

 Waziri wa maliasili na utalii  Lazaro Nyalandu aibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kura za maoni  za uchaguzi wa ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi jimbo la Singida Kaskazini Mkoani Singida
 Lazaro Nyalandu Mshindi katika kinyang'anyiro cha nafasi ya ubunge jimbo la Singida kaskazini akijibu  maswali toka kwa waandishi wa habari mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghj
Akitangaza matokeo hayo Katibu wa CCM na Mratibu wa uchaguzi wilaya ya Singida vijijini jimbo la Singida Kaskazini Mwanamvua Killo amemtaja mgombea Lazaro Samweli Nyalandu kuwa mshindi katika uchaguzi huo kwa kupata kura 13,738 kati ya idadi ya kura 25,403 ya kura halili zilizopigwa na kura 43 zilizo halibika  kwenye uchaguzi huo akifutiwa na mgombea Justine Josephat Monko kwa kupata kura 5648 kwenye kinyang’anyiro hicho jimboni humo.
Mgombea Lazaro Nyalandu akipunga mkono mara baada ya kutangazwa mshindi kwenye kinyang'anyiro cha ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Singida kaskazini huu akimshikilia mkewe Faraja K. Nyalandu nje ya jengo la CCM mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji)

 Katibu huyo amemtangaza rasmi Mgombea Lazaro Samweli Nyalandu kuwa ndio mshindi katika uchaguzi huo wa kura za maoni na kuwa ndiye mgombea atakayeipeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu  utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Hii ndio karatasi ya matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni kwa nafasi ya ubunge jimbo la Singida kaskazini ( Picha na Doris Meghji)
 Katika kinyang’anyiro hicho jumla ya wagombea nane walijitokeza kuwania nafasi hiyo Nyalandu akiwa mmoja wa wagombea,  ambao ni Michael Athuman Mpompo aliyepata kura 3,501, Kura 730 zilikuwa za mgombea Mungwe ABC Athuman,Saba saba ni mgombea aliyepata kura 618, wakati mgombea Aron Yesaya Mbogho amepata kura 446,Amos Jilili Makiya amepata kura 425 na mgombea Yohana Elia Sintoo kapata kura 254 kwenye uchaguzi huo wa kura za maoni ya nafasi ya ubunge jimbo la Singida Kaskazini.
 Ni Faraja Kota Nyalandu akipongwezwa na wanaccm mara baada ya mume wake Lazaro Nyalandu alipotangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa kura za maoni ya nafasi ya ubunge jimbo la Singida Kaskazaini ( Picha na Doris Meghji)

 Naye mgombea Lazaro Nyalandu amewashukuru wanachama wa chama hicho kwa kumuamini na kumpa tena ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi huo mkuu wa kumchagua rais, mbunge na diwani katika serikali ya awamu ya tano jimboni humo.
Katibu wa CCM wilaya ya Singida vijijini Mwanamvua Killo akitolea maelezo juu ya utaratibu wa wagombea wakikataa kusaini matokeo wanatakiwa wafanye nini mbele ya waandshi  habari mara baada ya kutangaza matokeo ( Picha na Doris Meghji)
Katika kujibu moja ya swali toka kwa waandishi wa habari juu ya wagombea wenzake kwa kutosaini matokeo ya uchgauzi huo  Nyalandu  amesema suala la kutosaini matokeo ya uchaguzi kwenye uchaguzi huo imekuwa hiyo sio habari mpya bali ni kutokukomaa kisiasa kwa sababu uchaguzi huo umesimamiwa  kanuni na kwa kufuata katiba ya chama hicho.
 Lazaro Nyalandu Mshindi katika kinyang'anyiro cha nafasi ya ubunge jimbo la Singida kaskazini akijibu  maswali toka kwa waandishi wa habari mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji)
“ Mimi nimekuwa mbunge kwa miaka  kumi na mitano hawakuwai  kusaini matokeo na niliendelea kuwa mbunge tu kwa hiyo sio habari mpya ni kutokukomaa kisiasa.” Asema Mgombea Nyalandu
Huyu ni Lazaro Nyalandu Mshindi katika kinyang'anyiro cha nafasi ya ubunge jimbo la Singida kaskazini akijibu  maswali toka kwa waandishi wa habari mkoa wa Singida ( Picha na Doris Meghji)
“sisi sote tumefanya kampeni vizuri na kwa vyovyote vile mshindi ambaye Lazaro Nyalandu ameshinda kididea mtu anayenifuata hata wakiunganisha  kura za wagombea wote wanane wakaamua tumpe mwenzetu mmoja ashinde bado hata shinda naamini aidha watafikiria wasaini au watakomaa kisiasa. lakini  hapa CCM mbele kwa mbele Nyalandu mbele kwa mbele na tunategemea wapinzani waisome namba”.Nyalandu asemea jambo hilo
Mgombea Mh. Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja Nyalandu akiwa tayari kuwasalimia na kuwashukuru wanaccm waliomchagua na kushinda kwenye nafasi hiyo ya ubunge jimbo la Singida kaskazini ( Picha na Doris Meghji)
Hata hivyo jimbo la singida kaskazini  ni moja kati ya majimbo nane ya mkoa wa Singida mengine ni Singida mjini,Ikungi magharibi ,Ikungi mashariki,Iramba, Mkalama Manyoni Magharibi na Manyoni Mashariki

Mwisho.

No comments:

Post a Comment