Na, Doris Meghji Jumamosi Agosti 29,2015
Singida
Shirika la la viwango la Taifa (TBS)
limewataka wananchi kukutumia fursa zilizopo ili kupata elimu juu ya faida ya
kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na shirika hilo
Akitoa maelezo hayo Bi Gladness Kaseka
afisa masoko mwandamizi toka shirika la viwango la Taifa (TBS) kwenye maonyesho
ya SIDO kanda ya kati yanayofanyika viwanja vya Peoples mkoani Singida
Afisa Masoko Kaseka amesema kwa kutumia
maonyesho hayo (TBS) imejipanga kutoa elimu juu ya shirika hilo, hasa ni kuhusu
suala la utaratibu wa kupata alama za ubora wa TBS kwa bidhaa zinazozalishwa na
wajasiliamali wadogo na wa kati huku elimu ya ukaguzi wa bidhaa zinazotoka
nje ya nchi haikuachwa katika maonyesho hao.
Bi Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akiwasilili kwenye viwanja vya peoples maoyesho ya SIDO
kanda ya kati yalitofanyika mkoani Singida(Picha na
Doris Meghji) |
“ kwa upande wa wajasiriamali watumie fursa ya
bure iliyopo ya kupatiwa alama ya ubora ili waweze kuuza zaidi bidhaa zao katika soko la
ushindani ndani na nje ya nchi” alisema Bi Kaseka
Shirika la viwango Taifa (TBS) lilianzishwa kwa sheria ya bunge sheria ya viwango namba 3 ya mwaka 1975 iliyofanyiwa marekebeshao na sheria namba 1 ya mwaka 1977 sheria hiyo ilifutwa na nafasi yake kuchuliwa na sheria ya viwango namba 2 ya mwaka 2009 ambayo inalipa shirika hilo uwezo mkubwa zaidi kwa kutekeleza majukumu yake.
Baadhi ya maafisa walioudhuria katika maonyesho hayo ya SIDO ya wajasiliamali kanda ya Kati kwenye viwanja vya peoples mkoani Singida kwenye viwanda vya Peoples (Picha na
Doris Meghji) |
Nao wajisiriamali waliofika kwenye maonyesho
hayo kupitia risala yao kwenye uzinduzi wa maonyesho hayo wameziomba taasisi za fedha kuzipunguza riba kubwa
na urasimu wa mikopo ya fedha zinazotozwa na taasisi hizo,
bajeti ya SIDO kuongezwa na huduma zake kuombwa zishuke hadi wilayani ili ziweze kuwafikia wananchi walio wengi
bajeti ya SIDO kuongezwa na huduma zake kuombwa zishuke hadi wilayani ili ziweze kuwafikia wananchi walio wengi
Ni wafanyakazi wa TTCL mkoa wa Singida wakiwa tayari kwenye maonyesho ya SIDO ya wajasiriamali kanda ya kati yalitofanyika mkoani Singida kwenye viwanda vya Peoples (Picha na
Doris Meghji) |
Aidha wajasiriamali hao wameomba serikali kupitia taasisi zake na sekta binafsi kueendelea kutoa elimu, ushauri na hata kutoa
ruzuku kwa wajasiriamali ili kukuza
biashara zao na sekta hiyo kwa ujumla.
Baadhi ya wajasiriamali wakitembelea banda la wakala wa vipimo kwenye maonyesho ya SIDO kanda ya kati yalitofanyika mkoani Singida kwenye viwanda vya Peoples (Picha na
Doris Meghji) |
Maonyesho hayo ya SIDO kanda ya kati yamehusisha wajasiriamali 205 toka mikoa kumi kati ya mikoa hiyo mikoa inayounda SIDO kanda hiyo ni mkoa wa Dodoma, Kigoma Singida, Shinyanga na Tabora.
MWISHO
No comments:
Post a Comment