Na, Doris Meghji Ijumaa Agosti 2015
Singida
Mtu mmoja afariki dunia na wengine wanne
kujeruhiwa baada ya kugongana basi kubwa la abiria aina ya scania na Noah leo katika kijiji cha Utaho kata ya Puma wilaya
Ikungi mkoani SINGIDA basi mali ya kampuni
PRINCESS ANAAM linalofanya safari zake toka Dar –es salaam kwenda Bariadi
mkoani Simiyu.
Kamanda ACP Sodeyeka akiongea siku ya
ufunguzi wa wiki ya usalama barabarani kwenye viwanja vya standi basi ya kwenda
mikoani manispaa ya Singida Picha na Doris Meghji) |
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida
ACP Thobias Sedoyeka ametoa taarifa hiyo
leo kwa vyombo vya habari kwa kuendelea kutoa wito kwa madereva wote na
watumiaji wengine wa barabara kufuata kanuni ,taratibu na sheraia za usalama
barabarani wanapotumia barabara hizo ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika
Kamanda Sodoyeka amesema ajali hiyo
imetokea leo majira ya saa 12: 45 jioni ambapo abiria Mwanahamisi Omary mwenye umri wa
miaka 48 mkazi wa Singida mjini amefariki dunia katika ajali hiyo na wengine
wanne kujeruhiwa mkoani hapa
Akielezea kutokea kwa ajali hiyo Kamanda
Sodeyeka amesema ajali imetoke kijiji cha Utaho kata ya Puma tarafa ya Ihanga
wilayani Ikungi barabra kuu ya Singida
Dodoma ambapo gari lenye namba za usajiri T.700 DCN scania basi mali ya kampuni
ya PRINCESS ANAAM ikifanya safari zake toka Dar- es salaam kwenda Bariadi
ikiendeshwa na dereva Omary Nassoro (38) iligonga gari yenye namba za usajili
T.703 BJQ Toyota Noah ikitokea Puma kwenda singida mjini ikiendeshwa na
Ismail sima ( 28) mkazi wa Ikungi na
kusababisha kifo cha abiria mmoja na
majeruhi wanne
ambao ni Jane Mushi mwenye umri wa miaka 45 Mchaga
mkazi wa Singida mjini ameumia mguu wa kushoto,Hawa Juma nyaturu mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa Msisi
mkulima aliyepata mauamivu kufuani na michubuko mwilini,huku Tatu Yusuph Mnyaturi
mwenye umri wa mika 40 mkulima na mkazi wa Ughandi amepata maumivu mwili mzima
akiwa pamoja na Juma Said Mwenye umri wa mika 21 mkulima na mkazi wa Matongo kwenye
ajili hiyo
Majeruhi hao wamelezwa katika hospitali
ya Mission Puma na hali zao zianndelea vizuri huku mwili wa marehemu umefanyiwa
uchunguzi na daktari katika hospitali ya mkoa wa Singida na kukabidhiwa ndugu zake tayari kwa mazishi
Wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi rasmi wa wiki ya usalama barabarani mkoani Singida iliyofanika kwenye viwanja vya standi basi ya kwenda
mikoani manispaa ya Singida Picha na Doris Meghji) |
Kwa mujibu wa kamanda huyo wa jeshi la
polisi mkoa wa Singida amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva la basi
ambapo alishindwa kumudu basi na kusababisha ajali hiyo.
Jeshi la polisi limekamata dereva huyo na kumshkiilia kwa uchuguzi baada ya hapo atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
MWISHO
MWISHO
No comments:
Post a Comment