Na, Doris Meghji Jumapili Agosti 02,2015
Singida - UCHAGUZI
Maboksi ya kupigia kura za wabunge na madiwani kwenye uchaguzi wa kura za maoni jimbo la Singida mjini ( Picha na Doris Meghji) |
Uchaguzi wa wabunge wa jimbo na madiwani wa
kata nchini umefanyika jana kwa kupiga
kura za maoni za kuwachagua wagombea wa nafasi
kwa tiketi ya chama cha mapinduzi.
Mwanachama akipiga kura ya mbunge na Diwani katika kituo cha utemeni ( Picha na Doris Meghji) |
Kwa mkoa wa Singida jumla wagombea 68 wamejikotekeza kugombea nafasi ya ubunge
kati ya hao ni wagombea wanne tu wanawake waliojitokeza kugombea nafasi hiyo
mkoani Singida huku Waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu na Mwigulu
Nchemba Naibu waziri wa fedha wakiwa
miongoni wa wagombea wanao tetea nafasi zao kwenye uchaguzi huo mkoani hapa.
wanachama wa CCM tawi la saba saba kata ya utemini wakikagua majina yao katika kituo hicho kwa lengo la kuwachagua viongozi wao wa ubunge na udiwani jimbo la Singida ( Picha na Doris Meghji) |
Mgombea Lazaro Nyalandu anayetetea
nafasi yake ya ubunge wa Singida Kaskazini na naibu waziri wa fedha Mwigulu
Nchemba kwa jimbo la Iramba.
Katika Kinyang’anyiro hicho.
Kwa upande
wa jimbo la Singida mjini ni Mgombea Hassan Philipo Mazala ameshinda kwa kupata
kura 6777 na Mussa Radhamani Sima akimfuatia kwa kura 6357 wakiwa wagombea wa jimbo wawili wanochuana
kwa wingi wa kura kwa jimbo hilo la singda mjini
wasimamizi wa uchaguzi na mawakala wa uchaguzi tawi la uwanja wa ndege wakiwa katika zoezi la uchaguzi wa kura za maoni jimbo la singida mjini (Picha na Doris Meghji) |
Huku wagombea wengine ambao ni Philemon
Kiemi akiwa amepeta kura 2192, Mhandisi Amani Rai kapata kura 1352,Juma Ahmed
Kiduba kura 884 na mgombea pekee wa kike na Mwandishi wa habari aliyebobea
katika upigaji picha za kihabari akiwa Bi Leah Samike amepata kura 636 kwa jimbo hilo la
singida mjini
Hadi majira ya Saa mbili za usiku ndipo matokeo hayo yalipobandikwa na kuzua taaruki miongoni mwa wanachama na baadhi ya wagombea akiweemo mgombea Mussa Ramadhan Sima ambaye hakutarajia kumatokeo hao kwa kuwa yeye aliamini ndiye ameshinda kwenye uchaguzi huo.
Hadi majira ya Saa mbili za usiku ndipo matokeo hayo yalipobandikwa na kuzua taaruki miongoni mwa wanachama na baadhi ya wagombea akiweemo mgombea Mussa Ramadhan Sima ambaye hakutarajia kumatokeo hao kwa kuwa yeye aliamini ndiye ameshinda kwenye uchaguzi huo.
Jimbo la Ikungi Mashariki ni Jonathan Njau
akongoza katika uchaguzi huo akifuatiwa
na Martini Lissu.
Ni wapiga kura kwenye uchaguzi wa kura za maoni kwa wabunge na madiwani jimbo la Singida mjini kituo cha Stesheni kata ya Utemini ( Picha na Doris MeghjI) |
Kwa upande wa jimbo Ikungi Magharibi ni kada Elibariki Kingu
ameongoza kwenye kinyang’anyiro hicho akifuatiwa na Nkambaku DC wa Kishapu
jimbo la Ikungi kusini
jimbo la Ikungi kusini
Singida Kaskazini ni Lazaro Nyalandu
ndiye aanayeogoza kwenye uchaguzi huo alifuatiwa na Justine Monko licha ya malalamiko wagombea wenzake
saba kulalamikia ukiuwakwaji wa kanuni za uchaguzi uliofanywa na mgombea
huyo kwenye kura hizo za maoni ya ccm jimbo la Singida humo.
Mgombea Lazaro Nyalandu wa jimbo la Singida Kaskazzini akiongea na waandishi wa habari nje a ofisi ya chama (Picha na Doris Meghji) |
Aidha jimbo la Iramba mgombea Mwigulu
Nchemba ameogoza kwenye uchaguzi huo akifuatiwa na kada David Jairo kwenye kinyang'anyiro hicho.
Katika ni Mwigulu Nchemba mgombea ubunge jimbo la Iramba ( Picha na Doris Meghji) |
Jimbo la Mkalama kura za maoni zinaongozwa na kada toka makao
makuu ya mamlaka ya mapato Tanzania Allen
Kiula akifuatiwa na Izumbe Mgana Msindai ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Singida na Mwenyekiti wa wenyeviti wote mikoa wa CCM nchini kwenye uchaguzi huo.
Mary Maziku Katibu wa CCM mkoa wa Singida akiongea na waandishi wa habarai jana ofisi ya katibu mkuu msadizi wa chama hicho mkoani Singida ( Picha na Doris Meghji) |
Wilaya ya Manyoni ikiwa na jimbo la
Manyoni mashariki na magharibu taarifa rasmi zitatolewa kesho na katibu wa mkoa
Mary Maziku juu ya matokeo yote ya uchaguzi huo mkoani hapa.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment