Na, Doris Meghji Ijumaa Agosti 14,2015
Singida
Zoezi la uchukuaji wa fomu za kuwania
nafasi ya ubunge na udiwani kutoka vyama mbali mbali vya siasa nchini umeanza
kwa wagombea wa nafasi hizo kuchukua fomu katika ofisi za watendaji wa kata na manispaa ya Singida mara baada ya
kuteuliwa na vyama vyao kupeperusha bendera za vyama hivyo vya siasa kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Katika zoezi hilo ambalo kwa mujibu wa
ratiba ya Tume ya taifa ya uchaguzi
(NEC) zoezi hilo la uchukuaji wa fomu hizo za kugombea nafasi za ubunge
na udiwani zimeanza rasmi Agosti nane mwaka huu,huku manispaa ya Singida katika
kata ya Utemini mgombea wa nafasi ya udiwani kupitia chama cha Mapinduzi Bartazary
Lessio Kimario amechukua rasmi fomu ya
kugombea nafasi hiyo kwa kata ya utemini
Mgombea huo mara baada ya kuchukua fomu
hiyo ya kuwania kinyang’anyiro hicho amewaahidi wanachama na wananchi wa kata
hiyo kumuunga mkono kwa kumdhanini na kumchagua kwenye nafasi hiyo ya udiwani
kwenye uchaguzi mkuu kwa kuhakikishia utekelezaji wa ilani ya CCM kutekelezwa
vizuri katika sekta mbali mbali hasa ya miundombinu elimu, maji na maendeleo ya
jamii.
Baadhi ya wanachi wa kata ya utemini wakiwa kweny moja ya mikutano ya kampeni za kura za maoni ndani ya CCM katika tawi la Stesheni (Picha na Doris Meghji) |
Katika suala la miundombinu Mgombea
Kimario amewahadi wananchi hao kuwa barabara za kata hiyo zitatekelezwa hasa
kupitia mradi wa banki ya dunia kwa kata hiyo ujenzi wa barabara mbili
zitajengwa ndani ya mradi huo wa banki ya dunia kwa manispaa ya Singida
kwa mujibu wa mratibu msaidizi wa uchaguzi kata ya utemii Afisa mtendaji wa
kata ya utemini Bi Eva Simon Mbelwa
amesema utaratibu wa uchukuaji wa fomu za wagombea baada ya uteuzi kwenye vyama vyao ambazo ni fomu ya ugombea na fomu ya maadili ambazo
kila mgombea anachukua nakala nne.
Afisa mtendaji huyo wa kata ya Utemini
amesema zoezi la uchukuaji wa fomu hizo umeanza rasmi Agosti 08 mwaka huu na kutarajiwa kukamilika Agosti
21 mwaka huu majira ya saa 10 jioni kwa kila mgombea kutakiwa kudhaminiwa na
wananchi wasiopungua 10 wenye
vitambulisho za kupigia kura za uchaguzi mkuu huo wako kwenye daftari la kudumu
la kupigia kura za uchaguzi huo kata ya Utemini.
Hata hivyo katika zoezi la kutafuta
wadhamini watakao mdhanini mgombea huo kwa nafasi ya udiwani kwa CCM kata ya Utemini
Daftari limeonyesha ni wapiga kura 2460 ndio walioko kwenye daftari hilo la
kudumu la wapiga kura huku wapigakura
2807 hawako kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.Kata ya utemini
iliandikisha jumla ya wapiga kura 5267 katika zoezi hilo mwaka huu.
Hili
ni moja la daftari la kudumu la wapiga kura kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika
Oktoba 25 Mwaka huu ( Picha na Doris Meghji) |
MWISHO
No comments:
Post a Comment