Na, Doris Meghji Ijumaa Agosti 14, 2015
Singida
Baadhi ya Viongozi wa vyama vya Siasa
ndani ya manispaa ya Singida wameiomba tume ya uchaguzi wa taifa (NEC) kuhakikisha wanalishughulikia mapema
suala la majina ya wapiga kura kutokuwepo kwenye daftari hiyo kabla ya uchaguzi
mkuu huo kufanyika nchini.
Kwa mujibu wa katibu mwenezi wa Siasa wa
chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) wilaya ya Singida mjini Bwana
Samwel Malow ameiomba na tume hiyo kuhakikisha inashughulikia tatizo hilo jimbo
la singida mjini kwa kuwa idadi kubwa ya wapiga kura waliojiandikisha haipo
kwenye daftari hizo.
Huyo ni Shaban Omary Kiranga mgombea wa
nafasi ya udiwani kwa tiketi ya CHADEMA akipokea kadi ya uanachama wa chama
hicho baada ya kurudisha kadi ya CCM mapema wiki huu.( Picha na Doris Meghji) |
Kauli hiyo ameitoa mapema wiki hii
katika mkutano wa chama hicho kilipokuwa kikiwapokea baadhi ya wanachama wa
chama cha Mapinduzi waliohamia chama cha Demokraisa na Maendeleo wakiwa ni
pamoja na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya udiwani kata ya Mandewa Shaban Omary
Kiranga wa toka CCM kushindwa kwenye
uchaguzi wa kura za maoni uliofanyika
Agosti Mosi mwaka huu na kuhamia CHADEMA.
Moja wa wanachama waliohama CCM na kuwa
wanachama wa CHADEMA mara baada ya mgombea wao kutoteuliwa kuwa mgombea wa
nafasi ya udiwani kata ya Mandewa kwenye ukumbi wa Samaki ( Picha na Doris
Meghji) |
Kwa mujibu wa katibu Mwenezi huyo amesema
katika zoezi la uandikishaji wananchi kwenye daftari la kudumu la wapiga kura
kata ya Madewa ilifanikiwa kuandika wapiga kura 10566 huku idadi ya majina
yalioko kwenye daftari hilo baada ya kuandikishwa ni 2034 tu ndio iliyoko
kwenye daftari hizo katani hapo.hivyo ameiomba tume hiyo kulishugulikia mapema
tatizo hilo
"mandewa ni waliojiandikia 10566 idadi a majina yaliopo 2034 zaidi ya 8000 hawapo kwenye daftari hii inatisha tunaiomba tume ilishughulikia suala hili"alisistiza Malow katibu mwenezi CHADEMA Singida mjini.
Hata hivyo kwa upande wa kata ya Utemini
ilifanikiwa kuandikisha kwenye zoezi hilo la daftari la kudumu la wapiga kura
ni 5267 na idadi ya walioko kwenye daftari hilo ni 2460 huku idadi ya wapiga
kura 2807 haipo kwenye daftari hilo
Moja ya daftari la kudumu la wapiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais mbunge na diwani utakao fanyika Oktoba 25 mwaka huu( Picha na Doris Meghji) |
Kutokana na tatizo hilo nilifanikiwa
kuongea na Mkurugenzi wa manispaa ya Singida Joseph Mchina juu ya suala hilo akasema ofisi yake kwa kwa
kushrikiana na NEC wanalisghulikia suala hilo hivyo amewaomba wananchi
wajitokeze kwenda kuhakiki majina yao kwenye mbao za matangazo kwenye ofisi za
kata za manispaa hiyo jimbo la Singida mjini.
Katika mkutano huo zaidi ya wanachama 13 wamehamia chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kata ya mandewa wilaya ya Singida mjini
Katika mkutano huo zaidi ya wanachama 13 wamehamia chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kata ya mandewa wilaya ya Singida mjini
Jimbo la Singida mjini lina jumla ya kata 18 ambapo uchaguzi wa madiwani wa kata hizo wanatarajiwa kuchaguliwa kwenye uchaguzi huo mkoani Singida
MWISHO.
No comments:
Post a Comment