Na, Doris Meghji Alhamis Agosti 20, 2015
Singida
Wananchi na wapiga kura wa jimbo la Singida
mjini wametakiwa kuzitembelea ofisi za watendaji wa kata wa jimbo hilo ili
kuhakiki majina yao ya vitambulisho vya
kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu
utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
|
Agizo hilo limetolewa na mratibu Msaidizi wa uchaguzi jimbo la Singida mjini Albert
Kassoga kwa kuwa zoezi hilo la uhakiki wa majina na kubadilisha taarifa ni kwa
muda siku saba kwa mujibu wa shereia na taratibu za tume ya uchaguzi nchini.
|
Mratibu huyo amesema zoezi la uhakiki wa
majina na kubadilisha taarifa limeanza
rasmi Agosti 19 na kutarajiwa kukamilika ndani ya siku saba ambapo Agosti 25
mwaka huu itakuwa mwishi wa hakiki huo
Ni mmoja wa wananchi waliouwa wakiandikishwa kwenye zoezi la BVR liliofanyika mapema mwaka huu kituo cha mtaa shule ya msingi sabasaba kata ya utemini ( Picha na Doris Meghji) |
Kwa upande wa jimbo la singida mjini
Kasoga amaesema ni majina 402 kati ya majina 85 670 yalitoandikishwa kwenye
zoezi la BVR kwenye vituo 91 hayakuwepo kwenye daftari hizo jimbo la
singida mjini
Ni wananchi wa mtaa wa stesheni kata ya Utemini wakivyojitokeza kwenye zoezi la uandikishaji kwenye daftari la kudumu la wapiga kura liliofanyika mapema mwaka huu ( Picha na Doris Meghji) |
hivyo amewakata wapiga
kura waliojiandisha kufika kwenye ofisi za watendaji wa kata kuhakiki majina na taarifa zao kwenye dafatri hilo
ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za kudalisha vituo vya kupigia kura kwa wale
waliohamia baada ya zoezi kufanyika la BVR kufanyika wakiwa na vitambulisho
vyao vya kupigia kura.
Mohamed Kipamila akimuhoji mmoja wa wapiga kura kwenye kituo cha shule ya msingi saba saba wakati wa zoezi la uandikishaji wananchi kwenye daftari la kudum la wapiga kura ( Picha na Doris Meghji) |
Mapema kabla ya kuongea na mratib
msaidizi huo wa uchaguzi jimbo la singida mjini nilifanikiwa kuzitembelea
baadhi ya ofisi za watendaji wa kata kata ya utemini Bi Eva Simon Mbelwa afisa
mtendaji wa kata ya Utemini katika kata hiyo ni majina ya wapiga kura 17 hayapo
kwenye daftari hilo,kata ya Mtaa Mohamed
Rashidi Kipamila afisa mtendaji kata hiyo amesema ni majina 19 hayapo
kwenye daftari la wapiga kura.
Albert Kassoga mratibu msaidizi wa
uchaguzi jimbo la Singida mjini kiongelea suala la Kuhakiki wa majina kwenye
daftri la wapiga kura kwenye vituo vya jimbo la singida mjini ( Picha na Doris
Meghji) |
Zoezi hilo la uhakiki wa daftari hilo
litahusu wapiga kura waliojiandikisha kwenye eneo husika na taarifa zao
kutokuwepo kwenye daftari hilo,taarifa kukosewa jina,umri na za jinsi ikiwa ni
pamoja majina ya waliojiandikisha na kupoteza maisha huku suala la wanaohamia
kwenye kituo toka kituo kingine kutakiwa kufika kwenye ofisi hizo kutoa taarifa
Add caption
|
Jimbo la singida mjini lana jumla ya
kata 18 wakati wa zoezi la BVR kata 16 na vituo 91 vilifanikisha zoezi hilo jimbo
la Singida mjini.
Ni wananchi wa mtaa wa saba saba kata ya Utemini wakivyojitokeza kwenye zoezi la uandikishaji kwenye daftari la kudumu la wapiga kura liliofanyika mapema mwaka huu |
MWISHO
No comments:
Post a Comment